Local News

TCRA YAKUTANA NA WAMILIKI WA BLOG DAR
Local News

MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania-TCRA wamekutana na Wamiliki wa Blog nchini, jijini Dar es salaam kwenye mkutano wenye lengo la kujadili namna ya kuwashirikisha Wamiliki wa Blog kutoa Maoni Juu ya Kanuni zinazotengenezwa kwa ajili ya kusambaza Taarifa muhimu za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi wa Madiwani, Wabunge na Urais. Akizungumza na Waandishi wa Habari Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Profesa JOHN NKOMA amesema Maendeleo ya Teknolojia yameleta Muingiliano wa Mawasiliano na Kukuza matumizi ya Internet na ndio sababu Wamiliki...

Like
406
0
Tuesday, 11 November 2014
WANANCHI WENYE UWEZO WAHIMIZWA KUWEKEZA KWENYE VINU VYA MAZAO YA KILIMO
Local News

WANANCHI wenye uwezo wamehimizwa kuwekeza kwenye vinu vya mazao ya kilimo ili kuweza kuwasaidia wakulima kuwapa uhakika wa masoko yao.   Ushauri huo umetolewa na Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji DOKTA MERRY NAGU katika ziara yake ya kutembelea viwanda mbalimbali nchini, na kusema uwekezaji huo utawasaidia wakulima walime zaidi kwakuwa viwanda vinauwezo wakutunza vyakula kwa utaalam na usalama wa kutosha.   DOKTA NAGU amesema uzalishaji wa nafaka umeongezeka kutokana na serikali kutoa zana za kilimo...

Like
455
0
Tuesday, 11 November 2014
KUTOKUJUA SHERIA KWA WAZEE WA MABARAZA YA KATA KUNACHANGIA MIGOGORO KATIKA JAMII
Local News

KUTOKUJUA masuala ya Sheria kwa Wazee wa Mabaraza ya Kata kunachangia migogoro katika jamii na kusababisha kuwa na mlundikano wa Kesi Mahakamani jambo ambalo linapaswa kumalizwa katika Mabaraza hayo.   Hayo yamebainishwa na Ofisa Utumishi wa Halmashauri ya Rungwe CHRISTOPHER NYAMBAZA alipokuwa akifunga mafunzo ya Wiki Moja ya Wasaidizi wa Kisheria kwa Niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo yaliyotolewa na Shirika la la House of Peace.   NYAMBAZA amebainisha kuwa Halmashauri itaangalia uwezekano wa kuwaingiza kwenye Mabaraza ya Kata...

Like
393
0
Tuesday, 11 November 2014
OPERESHENI YAKUPAMBANA NA MAJAMBAZI SUGU YAANZA TEMEKE
Local News

JESHI la polisi Mkoa wa kipolisi Temeke wameanza kufanya operesheni mbalimbali za kupambana na majambazi sugu pamoja na kuondoa vyanzo vya uhalifu hasa katika kipindi hiki cha kuelekea mwisho wa mwaka.   Hayo yamebainishwa jijini Dar es Salaam na kamanda wa polisi mkoa wa kipolisi  Temeke RPC Kihenya kihenya alipokuwa akizungumza na kituo hiki kuhusiana na changamoto za uhalifu zinazokuwa zinatokea katika kuelekea mwisho wa mwaka.   Mbali na hilo Kamanda Kihenya amesema kuwa kuna taarifa zinazotolewa na wananchi kuhusiana...

Like
337
0
Monday, 10 November 2014
NDUGAI: DENI LA MSD LIPO KATIKA UTEKELEZAJI
Local News

NAIBU SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  JOB NDUGAI, amewataka wabunge kuliacha suala la deni la Serikali inalodaiwa na Bohari ya Dawa nchini-MSD, kwakuwa lipo katika hatua za utekelezaji utakaoenda sanjari na utoaji wa ripoti juu ya suala hilo.   NDUGAI amelazimika kutoa ufafanuzi huo baada ya hoja iliyoibuliwa na mbunge wa Nkasi mashariki mheshimiwa ALLY MOHAMED KESSY alipohitaji kujua nini utekelezaji na mikakati ya serikali katika suala hilo sanjari na suala la Rais kutibiwa nje ya...

Like
270
0
Monday, 10 November 2014
VYETI VYA KUZALIWA KUTUMIKA KUTOA VITAMBULISHO VYA TAIFA
Local News

WATANZANIA wametakiwa kuwa na vyeti vya kuzaliwa ili waweze kuwa na sifa za kupewa vitambulisho vya Taifa. Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Usajili, Ufilisi,na udhamini nchini-RITA PHILIP SALIBOKO ameeleza hayo alipokuwa akiongea na Waandishi wa Habari mjini Moshi Kilimanjaro. Amebainisha kuwa ni vyema Watanzania wakawa na vyeti vya kuzaliwa kwani ni muhimu na vina mifumo inayotakiwa. Aidha amewataka wananchi wa mkoa huo kushiriki katika mpango ulioanzishwa na RITA wa kugawa vyeti vya kuzaliwa...

Like
301
0
Monday, 10 November 2014
WADAU WA MAENDELEO WAMEOMBWA KUISAIDIA TAASISI YA TEEN GIRLS SUPPORTIVE
Local News

WADAU mbalimbali wa Maendeleo wameombwa kushiriki ipasavyo katika kuisaidia Taasisi isiyo ya kiserikali ya TEEN GIRLS SUPPORTIVE ili kufanikisha lengo la kuwapatia Wasichana maarifa katika masuala ya Afya na Uchumi. Wito huo umetolewa jijini Dar es salaam na MARIAM JOSHUA ambaye ni mmoja wa Wanataasisi hiyo wakati wakifanya kampeni katika shule ya Sekondari ya King’ong’o juu ya Afya ya Uzazi na Maamuzi ya Kuchagua Kazi ya Kusomea. MARIAM amebainisha kuwa kampeni hiyo ni endelevu na wanatarajia kuyafikia maeneo yote ya...

Like
295
0
Monday, 10 November 2014
MECK SADIQ AZINDUA JARIDA LA SAUTI YA SITI
Local News

MKUU wa Mkoa wa Dar es saalam SAID MECK SADIQ leo amezindua rasmi Jarida la Kitabu cha Sauti ya Siti lenye maandishi ya Nukta Nundu lililoandaliwa na Chama cha wanahabari wanawake-TAMWA kwa kushirikiana na Sauti ya wanawake wenye ulemavu-SWAUTA kwa lengo la kuifikia jamii ya watu wasioona. Akizungumza na wadau mbalimbali Jijini Dar es Salaam, Mkuu huyo wa Mkoa wa Dar es Salaam, ameeleza kuwa jarida hilo litawasaidia wanawake wasioona kuweza kusoma yaliyoandikwa na kutambua haki zao muhimu pamoja na...

Like
341
0
Friday, 07 November 2014
JESHI LA POLISI TEMEKE KUFANYA MKUTANO NA WAMILIKI WA NYUMBA ZA KULALA WGENI
Local News

JESHI la polisi mkoa wa Kipolisi Temeke limesema kuwa wanatarajia kufanya mkutano mkubwa na wamiliki wa nyumba za kulala wageni zilizopo katika mkoa huo ili kuweka mikakati mbalimbali ya kuzuia mauaji ya wanawake yanayotokea  katika baadhi ya nyumba hizo.   Hayo yamebainishwa leo jijini Dar es Salaam na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa kipolisi Temeke Kehenya Kehenya wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.   Amebainisha kuwa wanawake hao waliuwawa katika matukio tofauti na vifo vyao wote vimefanana kwani wameuwawa kwa...

Like
337
0
Friday, 07 November 2014
TANZANIA KUPAMBANA NA UHALIBIFU WA TABAKA LA OZONE
Local News

TANZANIA imesema ipo tayari kuendeleza juhudi za kimataifa za kupunguza kuendelea kuliwa kwa tabaka la ozone kwa kuhakikisha kwamba inatunza misitu na kuwaelimisha wananchi juu ya menejimenti ya misitu hiyo. Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Mazingira , Mheshimiwa Binilith Mahenge wakati wa kufungua kikao cha 13 cha wadau wanaotekeleza program ya kutunza misitu ya Umoja wa Mataifa kinachofanyika Ngurdoto mjini Arusha. Amesema ingawa Tanzania kwa sasa ina hekta milioni 48.1 za misitu...

Like
368
0
Friday, 07 November 2014
BAADHI YA VIONGOZI TANZANIA KUSHIRIKIANA NA MAJANGILI CHINA!!!
Local News

SERIKALI ya Tanzania imesema imeshtushwa na Ripoti inayoelezea biashara haramu ya meno ya tembo kati ya baadhi ya viongozi wa nchi hiyo na China Serikali imesema imesikitishwa na ripoti iliyotolewa na taasisi ya uchunguzi ya mazingira inayodai kwamba majangili wa Kichina wakishirikiana na baadhi ya viongozi wa serikali ndio wanaoangamiza idadi ya tembo kutokana na biashara haramu ya meno ya tembo. Inadaiwa kwamba raia wa China walitumia ziara ya Rais wao nchini kusafirisha kimagendo maelfu ya kilo za pembe za...

Like
338
0
Friday, 07 November 2014