Local News

MIAKA MINNE (IV) E-FM YAANZA NA MSIMU WA SHIKA NDINGA.
Local News

  Katika kusherekea Miaka minne ya uwepo wa E Fm radio tunayo furaha sana na tuna kila sababu za kusherekea uwepo wetu. Wakati tunaanza tulikuwa na wafanyakazi 10 tu lakini leo hii E-fm imeajiri wafanyakazi zaidi ya 100 moja, wakati tunaanza tulikuwa tunasikika Dar-es-alaam pekee lakini leo hii E-fm inasikika kwenye mikoa 6 pia tumeweza kuwawezesha wadau wetu na mdau wetu mkubwa ni msikilizaji wa E-fm tukiwa na bidhaa kama SHIKA NDINGA ambapo tumefanikiwa kutoa magari ya biashara pamoja pikipiki...

Like
657
0
Tuesday, 27 March 2018
Rais Magufuli atoa rai hii kwa wawekezaji wazawa
Local News

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametoa rai kwa wawekezaji wazawa na wafanyabiashara nchini kujenga viwanda vya dawa na vifaa vya tiba hapa nchini ili kuongeza kasi ya ujenzi wa uchumi wa viwanda na kukuza ajira. Rais Magufuli ametoa rai hiyo leo Jijini Dar es Salaam, kwenye hafla ya uzinduzi wa magari 181 yenye thamani ya shilingi bilioni 20.7 ya kusambaza dawa na vifaa vya tiba yaliyotolewa msaada na Shirika la Global Fund kwa Serikali...

Like
596
0
Monday, 26 March 2018
YANGA WAENDA MOROGORO KUIWEKEA KAMBI SINGIDA UNITED
Local News

KIKOSI cha mabingwa wa Tanzania, Yanga SC kinatarajiwa kuondoka leo Dar es Salaam kwenda Morogoro kuweka kambi ya kujiandaa na mchezo wa Robo Fainali ya Azam Sports Federation Cup (ASFC) dhidi ya wenyeji, Singida Aprili 1, mwaka huu. Robo Fainali za Azam Sports Federation Cup zitaanza Machi 30, Singida United wakiikaribisha Njombe Mji FC Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga na Machi 31 kutakuwa na mechi mbili, Tanzania Prisons wakiwa wenyeji wa JKT Tanzania Uwanja wa Namfua mjini Singida na Azam...

Like
1024
0
Monday, 26 March 2018
Ajali ya gari yaua watu 24 Pwani
Local News

Imeelezwa kuwa watu 24 wamefariki dunia huku wengine 10 wakijeruhiwa vibaya baada ya Hiace iliyokuwa ikitokea Dar es Salaam kwenda Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani, kugongana uso kwa uso na lori lililokuwa likitokea Mtwara kuelekea Dar es Salaam. Taarifa hiyo imethibitishwa na Kaimu kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Kibiti, Mohamed Likwata ambapo amesema majeruhi wote wamepelekwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) jijini Dar es Salaam. Kamanda Likwata amesema ajali hiyo imetokea usiku wa kuamkia leo Jumapili Machi 25,...

Like
570
0
Sunday, 25 March 2018
WAZIRI MKUU AWATAKA VIJANA WAFANYE KAZI KWA BIDII NA MAARIFA
Local News

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka vijana wafanye kazi kwa bidii na maarifa kwa sababu kazi ndiyo msingi wa maendeleo yao na Taifa kwa ujumla.   Pia amewasihi wananchi wanaoishi katika maeneo ya mipakani wahakikishe suala la kulinda mipaka hiyo linapewa kipaumbele ili kuimarisha amani na utulivu nchini.   Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Jumamosi, Machi 24, 2018) wakati akizungumza na wananchi alipowasili katika uwanja wa ndege wa Nachingwea.   Waziri Mkuu ambaye yuko wilayani Ruangwa kwa ziara ya kikazi...

Like
531
0
Sunday, 25 March 2018
Fatma Karume apata ridhaa ya Tundu Lissu
Local News

Uchaguzi wa Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS) wa nafasi ya urais unatarajiwa kufanyika April 14, 2018, na wakili wa kujitegemea Fatma Karume amesema Jumamosi ana baraka zote za Rais wa chama hicho Tundu Lissu. Tundu Lissu, ambaye ni mwanasheria na mbunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) muda wake wa uongozi utapomalizika. Vyanzo vya habari nchini Tanzania vimesema kuwa Lissu aliye kwenye matibabu nchini Ubelgiji, hatagombea tena baada ya kumaliza mwaka mmoja wa uongozi wake. Kutokana na shambulizi la...

Like
492
0
Saturday, 24 March 2018
Waziri Mwigulu awataka walimu kutosita kutumia fimbo mashuleni
Local News

Waziri wa Mambo ya ndani, Dkt. Mwigulu Nchemba amewataka walimu nchini kuendelea kutoa elimu bora kwa wanafunzi kwa kuwafundisha maadili mema na pale inapobidi matumizi ya fimbo yatumike wasisite kufanya hivyo. Waziri wa Mambo ya ndani, Dkt. Mwigulu Nchemba amewataka walimu nchini kuendelea kutoa elimu bora kwa wanafunzi kwa kuwafundisha maadili mema na pale inapobidi matumizi ya fimbo yatumike wasisite kufanya hivyo. Akizungumza katika harambee ya ujenzi wa mabweni ya Shule ya Sekondari Lulumba Wilaya ya Iramba mkoani Singida, Dkt....

Like
484
0
Saturday, 24 March 2018
Mama Anna Makinda awafunda madiwani uongozi wa kijinsia
Local News

SPIKA wa Bunge la Jamhuri wa Tanzania mstaafu, Mama Anna Makinda ametoa elimu wa uongozi wa Kijinsia kwa madiwani wanawake wa Mkoa wa Dar es Salaam katika warsha ya siku moja iliyoandaliwa na TGNP Mtandao ikiwa na lengo la kuwajengea uwezo madiwani hao. Akizungumza katika warsha hiyo, Bi. Makinda alisema suala la kuwajengea uwezo wanawake linapaswa kuanza mapema mara baada ya kumalizika kwa uchaguzi ili kupata muda zaidi wa viongozi hao kupata elimu stahiki, kwani mara nyingi elimu hiyo hucheleweshwa...

Like
488
0
Friday, 23 March 2018
Makamu wa Rais Mama Samia akutana na Mkurugenzi Mtendaji wa Bill & Melinda Gates Foundation
Local News

Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan leo (Ijumaa) amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Bill & Melinda Gates Foundation, Rodger Voorhies. Mhe. Samia amekutana na Voorhies kwenye makazi ya Makamu wa Rais, Kilimani mjini...

Like
451
0
Friday, 23 March 2018
POLISI YAKAGUA MAGARI YA WAFANYAKAZI EFM
Local News

Kikosi cha Usalama barabarani kikiongozwa na Kamanda J.T.Gwau kilifika ofisi za Efm redio Pamoja na tve kwa ajili ya kutoa elimu juu ya Usalama barabarani pamoja na Ukaguzi wa Magari ya Wafanyakazi wake. Ikiwa ni pamoja na Ubandikaji wa stika za siku ya Nenda kwa Usalama barabarani. Zoezi hilo lilikwenda vizuri bila matatatizo yoyote, wafanyakazi wa EFM Redio pamoja na TV E wamelishukuru Jeshi la Polisi kwa kuwapatia elimu hiyo, na kuhadi wataitumia vizuri pindi wawepo barabarni ili kupunguza...

Like
778
0
Friday, 23 March 2018