Local News

RAIS MAGUFULI ATENGUA UTEUZI WA MKURUGENZI MTENDAJI WA TIC
Local News

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dokta John Pombe Magufuli, ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania-TIC, Bi Juliet Kairuki. Kwa mujibu wa Taarifa kwa vyombo vya Habari iliyotolewa leo na kusainiwa na Katibu Mkuu, Biashara na Uwekezaji, Profesa Adolf Mkenda, Uteuzi wa Bi Kairuki umetenguliwa kuanzia April 24 mwaka huu. Taarifa hiyo imeeleza kuwa, hatua hiyo imechukuliwa na Mheshimiwa Rais baada ya kupata taarifa kwamba Mkurugenzi huyo amekuwa hachukui mshahara wa Serikali tangu alipoajiriwa mwezi April...

Like
308
0
Thursday, 28 April 2016
VODACOM YACHANGIA ASILIMIA 2% YA PATO LA TAIFA 2012/2015
Local News

IMEBAINISHWA kuwa kwa mwaka 2012/2015 kampuni ya  simu za mkononi ya Vodacom imechangia zaidi ya  shilingi bilioni 3  katika  pato la taifa ambayo ni sawa na asilimia 2 ya pato la Tanzania. Hayo yamebainishwa leo jijini Dar es Salaam katika   tathmini iliyofanywa na  KPMG juu ya mchango mpana wa kiuchumi na kijamii ikiwamo ukuzaji wa uchumi,ajira,na kupunguza umaskini,tathmini iliyofanyika kuhusu mtaji na shughuli za uwekezaji kwa kipindi cha mwaka wa fedha  wa  2012/...

Like
307
0
Wednesday, 27 April 2016
RAIS MAGUFULI AWAAPISHA MAAFISA TAWALA WAPYA 10 LEO
Local News

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dokta John Pombe Magufuli,  amewaapisha Maafisa Tawala wapya kumi aliowateua April 25, mwaka huu na kuwapangia vituo vyao vya kazi. Makatibu Tawala hao wapya, wameapishwa leo Ikulu jijini Dar es salaam na kuweka saini ya ahadi ya uadilifu kwa Viongozi wa Umma, Zoezi lililoendeshwa na kamishna wa maadili Sekretarieti ya maadili ya Viongozi wa Umma, Mheshimiwa Jaji Salome Kaganda mbele ya Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John...

Like
318
0
Wednesday, 27 April 2016
MARA: WANANCHI WATAKIWA KUSHIRIKI KUCHANGIA MAENDELEO
Local News

WANANCHI katika halmashauri zote  mkoani mara wametakiwa kushiriki katika kuchAngia maendeleo na kuachana na dhana zinazoendelezwa na baadhi ya  viongozi katika serikali wanaotoa kauli zakuwapinga wananchi kuchangia maendeleo ya elimu na kulitumia vibaya neno Elimu bure. Yamesemwa hayo na mwenyekiti wa halmashauri ya BUTIAMA Magina Magesa alipokuwa akizungumza katika uhamasishaji wa kuchangia maendeleo ya elimu hususani ujenzi wa maaabara na madawati katika wilaya hiyo ....

Like
297
0
Wednesday, 27 April 2016
KONGAMANO LA UWEKEZAJI KATI YA WATANZANIA NA WARUSI KUFANYIKA IJUMAA WIKI HII
Local News

KITUO cha Uwekezaji Tanzania –TIC, kwakushirikiana na Russian Export Club kimeandaa Kongamano la Uwekezaji kati ya Watanzania na Warusi litakalofanyika siku ya Ijumaa katika Ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.   Mbali na TIC kongamano hilo limeandaliwa pia kwa ushirikiano na Mfuko wa Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Ubalozi wa Tanzania nchini Urusi na Ubalozi wa Urusi nchini Tanzania, kwa usimamizi wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji nchini Tanzania, Wizara ya Biashara na Viwanda ya Urusi na...

Like
258
0
Wednesday, 27 April 2016
MTOTO WA MWAKA MMOJA APOTEZA MAISHA BAADA YA KUTUMBUKIA SHIMONI
Local News

MTOTO mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi kumi na moja aliye tambulika kwa jina la  Waziri Kashinje amefariki dunia baada ya kutumbukia katika shimo la maji wakati akicheza na wenzake katika nyumba ya jirani yao eneo la igoma Jijini Mwanza.   Akizungumza na E Fm katika eneo la tukio mjumbe wa serikali ya mtaa huo Amosi Shirangi amesema tukio hilo limetokea wakati mtoto huyo alipokuwa akicheza na wenzake lililopo katika nyumba ya jirani.   Nao Wazazi wa mtoto huyo Kashinje...

Like
359
0
Monday, 25 April 2016
RAIS WA MAGUFULI AFANYA UTEUZI WA MAKATIBU TAWALA WA MIKOA 26 YA TANZANIA BARA
Local News

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dokta John Pombe Magufuli, leo amefanya uteuzi wa Makatibu Tawala wa Mikoa 26 ya Tanzania bara. Taarifa iliyotolewa leo na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, imeeleza kuwa kati ya Makatibu tawala hao 10 ni wapya, wawili wamebadilishiwa vituo na 13 wamebakishwa katika vituo vyao vya sasa. Makatibu tawala wa Mikoa 10 ambao wameteuliwa kwa mara ya kwanza, wataapishwa siku ya Jumatano April 27, Ikulu saa tatu...

Like
341
0
Monday, 25 April 2016
WAPINZANI WA TRUMP WAUNGANISHA NGUVU KUMZUIA
Local News

WAPINZANI wawili wakuu wa Donald Trump katika kinyang’anyiro cha kumteua mgombea urais wa chama cha Republican nchini Marekani wametangaza mipango ya kuungana kukabiliana na mgombea huyo. Ted Cruz na John Kasich wanataka kushirikiana kupunguza uwezekano wa mfanyabiashara huyo tajiri kutoka New York kushinda mchujo katika majimbo zaidi. Cruz, ambaye ni seneta wa jimbo la Texas, amesema atapunguza kampeni zake katika majimbo ya Oregon na New Mexico, Kwa upande wake John Kasich, ambaye ni gavana wa Ohio, naye amesema atamwachia Cruz katika...

Like
313
0
Monday, 25 April 2016
WANANCHI KUNUFAIKA NA UVUVI KWENYE BWAWA LA MTERA
Local News

WANANCHI wanaoishi kando ya bwawa la mtera mkoani Iringa wataendelea kunufaika na shughuli za uvuvi kutokana na bwawa hilo kujaa maji. Wakizungumzia kujaa huko kwa maji baadhi ya Wavuvi wamesema hali ya uchumi wao imeanza kutengemaa tofauti na ilivyokuwa awali kwa kuwa Samaki wameanza kupatikana kwa wingi. Nao wafanyabiashara wa Samaki wamesema bei ya samaki inaendelea kushuka kutokana na Samaki kupatikana kwa...

Like
551
0
Monday, 25 April 2016
23% YA WATOTO NCHINI WANASUMBULIWA NA UGONJWA WA MATUNDU YA MOYO
Local News

IMEELEZWA kuwa asilimia 23 ya watoto nchini wanasumbuliwa na ugonjwa wa matundu ya moyo ambao umekuwa ni moja kati ya magonjwa yanayoongoza kwa kusababisha vifo vingi vya watoto. Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini dar es salaam leo Daktari bingwa wa Magonjwa ya moyo kutoka kitengo cha moyo cha Jakaya Kikwete, Peter Richard amesema kuwa dalili zinazoashiria uwepo wa ugonjwa huo kwa mtoto ni pamoja na kushuka kwa kiwango cha ukuaji na homa kali za mapafu zinazojitokea mara kwa mara....

Like
372
0
Friday, 22 April 2016
TCRA: SIMU BANDIA CHANZO CHA KUUNGUZA NYUMBA
Local News

MAMLAKA ya Mawasiliano Nchini-TCRA-imesema kuwa asilimia 79 ya simu za mkononi zilizofanyiwa utafiti kwa kipindi cha mwezi disemba mwaka jana hadi Februari mwaka huu sio bandia wakati asilimia 18 ya simu hizo ni bandia. Aidha imeeleza kuwa asilimia kubwa ya nyumba zinazoungua kwa umeme kunatokana na simu bandia ambazo betri zake au vifaa vyake hushindwa kuhimili mionzi wakati zinapokuwa zinachajiwa hivyo kusababisha moto. Hayo yamesemwa na meneja uhusiano wa mamlaka hiyo Innocent Mungi wakati akizungumza katika semina ya mfumo wa...

Like
294
0
Friday, 22 April 2016