Local News

KATIBU MKUU WIZARA YA HABARI, UTALII, UTAMADUNI NA MICHEZO WA SERIKALI YA MAPINDUZI AAHIDI KUTOA HUDUMA BORA
Local News

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Omar Hassan Omar amesema atahakikisha anasimamia na kutekeleza adhima ya Serikali hiyo ya kuwapatia wafanyakazi wake huduma bora ili waweze kutekeleza kazi zao kwa ufanisi. Mheshimiwa Omar Hassan Omar ameyasema hayo baada ya kukabidhiwa rasmi ofisi na Katibu mkuu aliyemaliza muda wake Ali Mwinyikai katika ukumbi wa Wizara iliyopo Mnazi mmoja visiwani. Amesema utendaji kazi wa Serikali ni wa pamoja  na sio mtu mmoja mmoja hivyo amewaomba viongozi...

Like
266
0
Friday, 22 April 2016
WATENDAJI WA MAMLAKA ZA SERIKALI ZA MITAA WATAKIWA KUTEMBELEA MAENEO YAO YA KAZI
Local News

NAIBU waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mheshimiwa Selemani Jafo amewataka watendaji wa mamlaka za serikali za mitaa kuwa na utaratibu wa kutembelea maeneo yao ya kazi ili kujua changamoto zilizopo na kuzitatua. Akizungumza na walimu wa shule ya msingi Nzuguni B mkoani Dodoma wakati wa ziara aliyoifanya Mheshimiwa Jafo amesema kuwa watumishi hawawezi kufanya kazi kwa ubora iwapo hawatakuwa wakitembelea na kukagua maeneo yao ya kazi. Katika ziara yake amewataka walimu wa...

Like
243
0
Friday, 22 April 2016
UCHAGUZI MKUU 2015: WADAU WAIPONGEZA NEC
Local News

WADAU mbalimbali kutoka vyama vya Siasa vilivyoshiriki katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Octoba 25 mwaka jana wameipongeza Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kwa kuendesha zoezi hilo kwa Uwazi, Haki, Amani na kwa kuzingatia Sheria na Kanuni. Hayo yamesemwa leo na Katibu Mkuu wa Chama cha NRA Hassan Kasabya alipokuwa akitoa pongezi kwa Tume hiyo kwa kutoa vyeti vya shukrani kwa washiriki hao kutoka vyama vya siasa na wadau...

Like
269
0
Thursday, 21 April 2016
MKUU WA WILAYA YA KINONDONI AAPISHWA RASMI LEO
Local News

MKUU wa mkoa wa Dar es salaamu mheshimiwa PAUL MAKONDA leo amemuapisha rasmi mteule mkuu wa wilaya ya kinondoni ALY SALUM HAPI ambapo amemtaka kuhakikisha anakuwa mstari wa mbele kutimiza matakwa ya mheshimiwa rais ikiwemo kupinga ufisadi na rushwa . Awali akizungumza mbele ya watendaji ,wakuu wa wilaya na wakuu wa ulinzi na usalama, mheshimiwa PAUL MAKONDA amesema licha ya kuwa na umri mdogo inatakiwa atumie nafasi alio aminiwa na mheshimiwa rais kutekeleza majukumu hasa kuhakikisha kunakuwepo na haki kwa...

Like
368
0
Thursday, 21 April 2016
2 WACHOMWA MOTO ZAMBIA KWENYE VURUGU
Local News

POLISI nchini Zambia wamesema watu wawili wamechomwa moto mjini Lusaka katika vurugu ya ubaguzi wa wenyeji dhidi ya wageni. Watu Zaidi ya 250 wamekamatwa baada ya maduka mengi yanayomilikiwa na wanyarwanda kuvamiwa. Uvamizi huo umetokea baada ya wanyarwanda hao kushutumiwa kuua watu na kutumia viungo vyao kuvutia wateja....

Like
341
0
Thursday, 21 April 2016
MHANDISI MANISPAA YA ILALA NA WASAIDIZI WAKE WATUMBULIWA
Local News

MANISPAA ya Ilala Jijini Dar es salaam imemvua madaraka mkuu wa Idara ya ujenzi mhandisi Japhery Bwigane na wasaidizi wake wawili kwa tuhuma za kusimamia ujenzi wa barabara za manispaa hiyo kujengwa chini ya kiwango.   Akizungumza na waandishi wa Habari wakati akitoa taarifa hiyo, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Charles Kuyeko amewataja maofisa wengine wa idara hiyo waliosimamishwa kuwa ni Siajali Mahili na Daniel Kirigiti ambao wamehamishwa idara hiyo ili kupisha uchunguzi.   Kuyeko amesema baraza la madiwani...

Like
283
0
Thursday, 21 April 2016
MUHIMBILI YAFANYA UPASUAJI WA PUA, MASIKIO LEO
Local News

MADAKTARI Bingwa wa Upasuaji kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa kushirikiana na timu ya Madaktari wanne kutoka nchini Hispania wameendesha zoezi la upasuaji wa masikio, pua, pamoja na upasuaji wa shingo na kichwa.   Akizungumzia kuhusu zoezi hilo Daktari Bingwa wa magonjwa ya masikio, Pua na koo Martin Mushi amesema katika upasuaji huo madaktari hao wanatumia teknolojia kubwa na ya kisasa zaidi ambapo pamoja na mambo mengine ujio wao utawawezesha madaktari wa Muhimbili kujifunza zaidi matumizi ya teknolojia mpya ya upasuaji....

Like
455
0
Thursday, 21 April 2016
KOREA KASKAZINI YASHINDWA KURUSHA KOMBORA
Local News

KOREA Kaskazini imefanya jaribio la kufyatua kombora katika pwani yake ya mashariki, lakini dalili zinaonesha jaribio hilo halikufanikiwa, kwa mujibu wa maafisa wa Marekani na Korea Kusini. Bado haijabainika roketi iliyotumiwa ilikuwa ya aina gani lakini inadhaniwa majaribio hayo yalikuwa ya kombora la masafa ya wastani kwa jina “Musudan” ambalo taifa hilo lilikuwa halijalifanyia majaribio. Shughuli hiyo ilikuwa ikifanyika siku ambayo ni ya kuadhimisha siku ya kuzaliwa kwa mwanzilishi wa taifa la Korea Kaskazini Kim...

Like
277
0
Friday, 15 April 2016
SEKTA YA VIWANDA INAWEZA KULETA MABADILIKO YA UCHUMI
Local News

IMEELEZWA kuwa endapo sekta ya viwanda itasimamiwa na kuwekewa mazingira bora, ina nafasi kubwa ya kuleta mabadaliko na kuweza kuharakisha ukuaji wa uchumi na kuliwezesha Taifa kufika pale linapokusudia kufika kama inavyoainishwa na dira ya Taifa ya maendeleo ya mwaka 2025. Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa REPOA Dokta Donald Mmari katika mahojiano maalum na Efm juu ya namna sekta ya viwanda inavyoweza kutumika kuleta mageuzi ya kiuchumi yanayoenda sanjari na mabadiliko ya mtu mmoja mmoja. Dokta Mmari amesema kuwa licha...

Like
300
0
Friday, 15 April 2016
SALVA KIIR AWASILI NCHINI LEO
Local News

RAIS wa Sudan Kusini Salva Kiir ambaye amewasili nchini leo, anatarajiwa kutia saini mkataba wa kuiingiza rasmi nchi hiyo kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki. Rais Kiir atatia saini mkataba huo jijini Dar es Salaam mbele ya mwenyeji wake, Rais wa Tanzania John Magufuli, ambaye kwa sasa ndiye mwenyekiti wa jumuiya hiyo. Sudan Kusini itakuwa nchi ya sita kujiunga na jumuiya hiyo iliyoanza kwa nchi tatu Tanzania, Kenya na Uganda. Rwanda na Burundi zilijiunga na jumuiya hiyo...

Like
251
0
Friday, 15 April 2016
KUBENEA AHUKUMIWA KIFUNGO CHA NJE MIEZI MITATU KWA KUMTUSI PAUL MAKONDA
Local News

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuhukumu mbunge wa Jimbo la Ubungo kupitia chama cha (CHADEMA) Saeed Kubenea kifungo cha nje cha miezi mitatu kutokana na kosa la kutumia lugha ya matusi dhidi ya aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mheshimiwa Paul Makonda ambaye kwa sasa ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.   Akisoma hukumu hiyo jana Jijini Dar es Salaam Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu Thomas Simba amesema kuwa mahakama imeamua kumpa mshitakiwa adhabu ya kifungo hicho kwa kuwa ndilo kosa lake la...

Like
371
0
Thursday, 14 April 2016