Local News

SERIKALI YAAGIZA HALMASHAURI KUHAKIKISHA ELIMU INATOLEWA BURE
Local News

WIZARA ya Elimu Sayansi Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi  imewataka wakuu wa wilaya na Wakurugenzi wa Halmshauri za Wilaya, Miji na Manispaa zote nchini kufuatilia kwa karibu utekelezaji wa agizo la utoaji wa elimu bure kwa shule za awali, msingi na sekondari kama lilivyotolewa na  rais. Hatua hiyo imetokana na Wizara ya Elimu kupokea taarifa mbalimbali kutoka kwa wadau wa elimu kuwa kuna baadhi ya walimuu wakuu wa shule za msingi na sekondari kuendelea kutoza fedha za uandikishaji wa wanafunzi...

Like
302
0
Monday, 21 December 2015
DNA YATOA UKWELI WA MAMBO
Local News

ASILIMIA 49 kati ya asilimia 100 ya matokeo ya uchunguzi wa makosa ya vinasaba (DNA)  yanayowasilishwa katika ofisi ya Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kwa mwaka yanaonyesha kuwa baba si mzazi halali wa mtoto katika kesi hizo.   Hayo yamesemwa na Mkemia Mkuu wa Serikali, Profesa Samwel Manyele alipokuwa akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kufungua mkutano wa wadau wa wakala wa afya ya mazingira leo jijini Dar es Salaam.   Profesa Manyele aliongeza kuwa...

Like
268
0
Monday, 21 December 2015
KAMATI BORA ZA KUDHIBITI UKIMWI ZAZAWADIWA PANGANI
Local News

SHIRIKA lisilo la kiserikali Wilayani Pangani la-UZIKWASA linalojishughulisha na kuziwezesha kamati za kudhibiti Ukimwi, limetoa zawadi kwa kamati bora za kudhibiti ukimwi Wilayani humo.   Katika sherehe zilizofanyika kijiji cha Jaira, kata ya Madanga wilayani Pangani na kuhudhuriwa na watu mbalimbali wakiwemo viongozi kutoka halmashauri ya Wilaya ya Pangani mgeni rasmi alikuwa Kaimu Afisa Maendeleo wa Wilaya hiyo, Bi.Patricia Kinyange.   Akizungumza katika hadhara hiyo Bi. Kinyange amelipongeza shirika hilo kwa kuzijengea uwezo kamati hizo...

Like
450
0
Monday, 21 December 2015
VYUO NA TAASISI ZA ELIMU ZIMETAKIWA KUTOA MAFUNZO YANAYOENDANA NA SOKO LA AJIRA
Local News

KATIBU Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue amevitaka vyuo na taasisi za elimu nchini kuhakikisha vinatoa mafunzo bora yanayoendana na mahitaji ya soko la ajira.   Akizungumza Jijini Dar es Salaam katika mahafali ya kwanza ya Shahada ya Takwimu Rasmi katika Chuo Cha Takwimu Mashariki mwa Afrika (EASTC), Balozi Sefue amesema ni vyema vyuo na taasisi za elimu zikahakikisha zinafanya tafiti ili kujua mahitaji ya wataalamu wanaotakiwa.   Hata hivyo serikali imekuwa mstari wa mbele kupitia Wizara ya Fedha kuhakikisha inakisaidia...

Like
253
0
Monday, 21 December 2015
CHADEMA YAITAKA NEC KUONDOA VIKWAZO MAJINA YA MADIWANI
Local News

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kimeitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi Nchini –NEC,  kuhakikisha inaondoa vikwazo vyote  katika mchakato wa kutangaza majina ya madiwani wa viti maalumu . Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dae Es Salaamu leo,  Kaimu Katibu Mkuu wa chama hicho SALIMU MWALIMU,  ameitaka tume hiyo kutenda haki katika kugawanya viti maalumu vya udiwani kwa kufuata kanuni na taratibu za ugawaji .  ...

Like
230
0
Friday, 18 December 2015
DK KIGWANGALLA ATUMBUA MAJIPU YA WACHELEWAJI WIZARA YA AFYA
Local News

NAIBU  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dokta. Hamisi Kingwangalla amefanya ukaguzi wa kushtukiza katika ofisi za wizara hiyo kwa kusimama getini kuzuia wafanya kazi wote wa wizara ambao walikuwa wamefika ofisini baada ya saa 1:30 asubuhi muda ambao ndiyo mwisho wa wafanyakazi kuingia ofisini.   Awali Dkt. Kingwangalla alifika ofisini saa 1:05 asubuhi huku akiingia ofisini kwa kutembea mwenyewe bila kutumia usafiri wa gari na kwenda moja kwa moja ofisini kwake ambapo alitoka ilipofika saa...

Like
316
0
Friday, 18 December 2015
KIWANDA CHA NYUZI TABORA KURUDISHWA MIKONONI MWA SERIKALI
Local News

SERIKALI Mkoani TABORA imewataka wawekezaji katika kiwanda cha Nyuzi cha TABORA kurejesha kiwanda hicho mikononi mwa serikali kutokana na kushindwa kukiendesha kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa na kuwakosesha wananchi ajira.   Akizungumza katika ziara ya kushitukiza kiwandani hapo, Mkuu wa Manispaa ya TABORA, Bwana SULEIMAN KUMCHAYA amesema kufuatia wamiliki wa kiwanda hicho kutoka INDIA kushindwa kukiendesha,iko haja ya kukirudisha mikononi mwa serikali.   Kwa upande wake, Mbunge wa Jimbo la TABORA mjini, Mheshimiwa EMMANUEL MWAKASAKA...

Like
345
0
Friday, 18 December 2015
WITO UMETOLEWA KWA WATANZANIA KULINDA AMANI YA NCHI
Local News

WITO umetolewa kwa Watanzania kuungana kwa pamoja na kufuata mafundisho yanayo jenga amani katika nchi na  kuacha mafundisho ambayo yana weza kuleta mfalakano ili kuilinda amani ya nchi iliyopo. Wito huo umetolewa  Jijini Dar es salaam na Mkuu wa Usalama wa jeshi la wananchi wa Tanzania -JWTZ Meja Jenerali VENANCE MABEYO  wakati wa  uzinduzi wa utafiti uliofanywa na taasisi isiyo ya kiserikali ya TWAWEZA  ambao ulilenga kuangalia matukio ya kiitikadi ambapo amesema kuwa  sababu kubwa  inayo sababisha vitendo hivyo kuwepo...

Like
216
0
Friday, 18 December 2015
MAPENDEKEZO YA ILANI YA VIJANA YA MWAKA 2015 KUJADILIWA
Local News

SHIRIKA la Maendeleo ya Vijana nchini (RESTLESS) linatarajia kukutana na viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa wakiwemo wabunge na madiwani kutoka vyama tofauti pamoja na viongozi wa Serikali ili kujadili  mapendekezo yaliotokana na ilani ya vijana ya mwaka 2015 -2020. Akizungumza jijini dare s Salaam kwenye semina iliyoandaliwa na shirika hilo na kuwakutanisha vijana kutoka mikoa mbalimbali nchini walioshiriki kuandaa ilani hiyo,  Mkurugenzi wa Restless development Margaret Mliwa, amesema kuwepo kwa viongozi hao kesho kutawasaidia vijana...

Like
315
0
Thursday, 17 December 2015
BOMOABOMOA YAANZA BONDE LA MTO MSIMBAZI
Local News

IMEELEZWA kuwa, ili kuhakikisha kwamba wananchi wanaishi kwa raha na amani kipindi chote cha mwaka  hasa kipindi cha masika,  serikali ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania  leo imeanza kubomoa baadhi ya maeneo yanayo zunguka bonde la mto msimbazi. Efm imetembelea maeneo ambapo zoezi la bomoa bomoa limetekelezwa na kushuhudia  katapila la serikali likivunja nyumba hizo ambapo mpaka efm inaondoka zaidi ya nyumba 30  zilikuwa zimevunjwa . Wakizungumza na e fm huku zoezi likiwa linaendelea baadhi ya viongozi wanao simamia zoezi...

Like
519
0
Thursday, 17 December 2015
MAFURIKO: WAZIRI  JENISTA MHAGAMA AFANYA ZIARA BOKO BASIHAYA
Local News

KUFUATIA eneo la boko Basihaya  kuwa na tatizo la kujaa maji kwa wingi pindi mvua inapo nyesha  hali inayo pelekea mafuriko, Waziri ofisi ya waziri mkuu sera ,bunge vijana ,ajira na walemavu mheshimiwa JENISTA MHAGAMA leo amefanya ziara katika eneo hilo  ili kujionea hali ilivyo  . Akizungumza mara baada ya kutembelea maeneo yalio athiriwa na maji mheshimiwa Waziri amemtaka Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni pamoja na watendaji wake kuhakikisha wanaripoti Wizarani leo saa kumi jioni wakiwa na maelezo ya...

Like
494
0
Wednesday, 16 December 2015