Local News

DK. SHEIN: TOFAUTI ZA KISIASA ZISIVURUGE AMANI
Local News

RAIS wa  Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dokta  Ali Mohamed Shein  ametaka tofauti za kisiasa zilizopo Visiwani humo zisitumike kuvuruga amani na utulivu ambayo ndiyo siri kubwa ya maendeleo yaliyopatikana katika visiwa vya Unguja na Pemba.   Dokta Shein ambaye alikuwa akizungumza na wananchi wa Wete waliokwenda kumsalimia mara baada ya kukagua ujenzi wa soko na Ofisi ya Baraza la Mji wa Wete, amesema kuwa suala la amani halina mbadala huku akiahidi kuendelea kuisimamia amani ya Zanzibar na...

Like
140
0
Thursday, 07 January 2016
BODI YA UTALII IMETAKIWA KUTUMIA VYOMBO VYA HABARI VYA KIMATAIFA KUITANGZA TANZANIA
Local News

WAZIRI wa Maliasili na Utalii Profesa Jumanne Maghembe ameitaka Bodi ya Utalii Tanzania- TTB, kuendelea kutumia vyombo vya habari vya Kimataifa kama vile CNN na BBC  kuitangaza Tanzania kama eneo la Utalii duniani sambasamba na kuweka makala na matangazo ya utalii katika majarida ya Kimataifa yanayoandika habari za Utalii na usafiri (Travel Magazine) ambayo ndiyo husomwa na watalii wengi duniani. Waziri Maghembe amesema hatua hiyo itasaidia kuongeza idadi ya watalii nchini.   Waziri Maghembe ameyasema hayo alipotembelea Bodi ya Utalii...

Like
192
0
Thursday, 07 January 2016
IRINGA: VIONGOZI WA VYAMA VYA USHIRIKA VYA ZAO LA TUMBAKU WASIMAMISHWA
Local News

WAZIRI wa kilimo,mifugo na uvuvi mheshimiwa Mwigulu Nchemba amewasimamisha viongozi wa vyama vya ushirika vya zao la tumbaku mkoani Iringa. Akizungumza kwenye mkutano uliofanyika katika ukumbi wa siasa na kilimo, Mheshimiwa Mwigulu amemuagiza mrajisi wa mkoa kuivunja bodi hiyo na kuwachunguza viongozi wa vyama hivyo. Aidha, ameiomba serikali ya mkoa kufuatilia na kutathimini ubadhirifu uliofanywa na viongozi hao na kuwachukulia hatua ili kukomesha vitendo...

Like
363
0
Thursday, 07 January 2016
TRA YAKUSANYA TRILIONI 1.4 KATIKA KIPINDI CHA MWEZI DESEMBA 2015
Local News

JUMLA ya shilingi trilioni 1.4 zimekusanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) katika kipindi cha mwezi Desemba mwaka uliopita wa 2015.   Kiasi hicho ni sawa na ongezeko la wastani wa shilingi  bilioni 490 kwa mwezi ikilinganishwa na wastani wa makusanyo ya kuanzia Julai hadi Novemba ambapo ,TRA ilikuwa imekusanya wastani wa shilingi bilioni 900 kwa mwezi.   Takwimu hizo zimetolewa leo jijini Dar es salaam na Kaimu Kamishna Mamlaka ya Mapato  Tanzania (TRA) Alphayo Kidata wakati wa mkutano na...

Like
203
0
Wednesday, 06 January 2016
RAIS MAGUFULI ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA KIFO CHA INSPECTA GERALD RYOBA
Local News

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta. John Pombe Magufuli amemtumia salamu za rambirambi Mkuu wa Jeshi la Polisi hapa Nchini IGP Ernest Mangu kufuatia kifo cha msaidizi wake Inspekta – Gerald Ryoba aliyepoteza maisha katika ajali ya kusombwa na mafuriko ya maji wakati akikatiza katika eneo la Kibaigwa, Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma.   Katika ajali hiyo iliyotokea Januari 3 mwaka huu, Inspekta Ryoba akiwa na Mkewe na watoto wake wawili, pamoja na watu wengine wawili walikuwa wakisafiri...

Like
299
0
Wednesday, 06 January 2016
PANGANI: SERIKALI YATOA MIEZI 3 KWA WALIOHODHI VIWANJA KUVIENDELEZA
Local News

SERIKALI wilayani Pangani imewapa miezi mitatu baadhi ya watu waliohodhi viwanja vikiwemo vile vilivyopo pembezoni mwa bahari ya hindi kuviendeleza la sivyo haitasita kuwanyang’anya kwa mujibu wa sheria ili kuendeleza mji wa pangani ambao sehemu kubwa ya makao makuu ya wilaya imezungukwa na mapori. Akizungumza na efm kuhusu baadhi ya wafanyabiashara kuhodhi maeneo kwa makusudi kwa lengo la kuyafanyia biashara, mkuu wa wilaya ya pangani Regina Chonjo amemuagiza Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Pangani kwa kushirikiana na...

Like
208
0
Wednesday, 06 January 2016
WAZIRI MKUU ATEMBELEA KIWANDA CHA KUSINDIKA TUMBAKU MKOANI RUVUMA
Local News

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametembelea kiwanda cha kusindika  tumbaku  cha mkoani Ruvuma na kuwasimamisha kazi viongozi wa Chama Kikuu Cha Ushirika cha SONAMCU.   Alikuwa akizungumza  katika ukumbi wa mikutano wa Ikulu Ndogo ya Songea, wakati alipokutana na wakulima wa zao la tumbaku wa Wilaya ya Namtumbo, Wananchama wa Vyama Vya Ushirika vya Mkoa wa Ruvuma, viongozi wa Mkoa pamoja na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Edwin Ngonyani ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Tunduru Kaskazini.   Waziri...

Like
260
0
Wednesday, 06 January 2016
KIPINDIPINDU BADO TISHIO GEITA
Local News

VIONGOZI wa Mkoa wa Geita wametakiwa wasiwaonee aibu kuwafungia wafanyabiashara wasiofuata kanuni za usafi wa mazingira na hivyo kupelekea mlipuko wa kipindupindu.   Hayo yamesema na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu wakati alipotembelea kambi ya wagonjwa ya kipindupindu iliyopo kwenye kituo cha afya Nyankumbuli mjini Geita.   Waziri Ummy amesema mlipuko wa kipindupindu upo hivyo kuwafumbia macho wale ambao wanafanya biashara katika mazingira yasiyo safi na salama lazima watu hao wafungiwe.  ...

Like
273
0
Tuesday, 05 January 2016
MHANDISI RONALD LWAKATARE ATEULIWA KUWA KAIMU WA DART
Local News

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. George Boniface Simbachawene, amemteua Mhandisi Ronald Lwakatare kuwa Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka Dar es salaam –DART, uteuzi ambao umeanzia jana.   Uteuzi huo unafuatia kusimamishwa kazi kupisha uchunguzi kwa aliyekuwa Mtendaji Mkuu Bibi Asteria Mlambo aliyesimamishwa tarehe...

Like
454
0
Tuesday, 05 January 2016
WAZIRI MKUU AFUNGUA TAWI LA BENKI YA POSTA SONGEA
Local News

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amefungua tawi la Benki ya Posta iliyopo mjini Songea, wakati akiwa katika ziara mkoni Ruvuma inayotarajiwa kumalizika kesho, jumatano.   Akizungumza  na uongozi  na wafanyakazi wa  Benki ya Posta pamoja na wateja waliohudhuria ufunguzi  wa tawi hilo uliofanyika  nje ya benki hiyo, Waziri Mkuu  amesema amefarijika kuona benki hiyo  iliyokua imekumbwa na matatizo sasa imezaliwa upya na kumpongeza Mkurugenzi wa Benki ya Posta  nchini Bwana. Sabasaba Mushindi kwa jitihada zake za kuifufua....

Like
359
0
Tuesday, 05 January 2016
BOMOA BOMOA: MAHAKAMA KUTOA MAAMUZI YA LEO
Local News

MAHAKAMA kuu ya Tanzania kitengo cha Ardhi leo inatarajia kutoa maamuzi juu ya ombi la dharura la kutaka zoezi la bomoabomoa kusitishwa katika kipindi ambacho kesi  hiyo ipo Mahakamani.   Wakili wa mshitaki Abubakari Salim amesema kutokana na uwepo wa kesi mahakamani juu ya wananchi kutotendewa haki katika zoezi la kubomoa nyumba za mabondeni iliyofunguliwa na Mbunge wa Jimbo la Kinondoni Maulidi Mtulia waliamua kupeleka hati ya dharura ya kutaka zoezi hilo kusitishwa wakati kesi hiyo ikiendelea mahakamani.   Jaji...

Like
342
0
Tuesday, 05 January 2016