Local News

BARAZA LA TAIFA LA UJENZI LAPOKEA MIGOGORO 41 NA KUIPATIA UFUMBUZI 2015
Local News

BARAZA la Taifa la Ujenzi limepokea migogoro 41 na kufanikiwa kuitafutia ufumbuzi katika kipindi cha mwaka 2015 kwa kushirikiana na wadau wa sekta ya Ujenzi nchini.   Hayo yamesemwa leo na Mtendaji Mkuu wa Baraza hilo,  Mhandisi Dokta Leonard Chamuriho  wakati wa mkutano na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam.   Akizungumzia majukumu ya Baraza hilo katika kutatua Migogoro inayojitokeza katika Sekta hiyo, Mhandisi Chamuriho amebainisha kuwa migogogoro iliyojitokeza imekuwa ikitegemea Ukubwa wa mradi, Hali ya eneo la mradi,...

Like
180
0
Wednesday, 30 December 2015
KESI YA WAFANYAKAZI TRA KUSIKILIZWA JANUARY 2016
Local News

KESI inayowakabili wafanyakazi wa Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) inatarajiwa kusikilizwa  tena January 13, mwaka  2016   Akizungumza katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini dar es salaam Wakili wa Serikali Bi.Dianna Lukondo amesema kuwa kwa leo Kesi ilikuja kwa ajili ya kusikilizwa na kutoa dhamana kwa washtakiwa na hivyo imeshindikana kusikilizwa kutokana na upelelezi kutokamilika.   Washtakiwa hao wanatuhumiwa kwa kosa la uhujumu uchumi, wakidaiwa kuhusika na upotevu wa makontena 329 katika Bandari ya Dar es Salaam...

Like
174
0
Wednesday, 30 December 2015
KAMPUNI ILIYOPEWA TENDA YA KUKUSANYA UCHAFU UPANGA MAGHARIBI KUVUNJIWA MKATABA
Local News

KUFUATIA kukithiri kwa uchafu katika kata ya Upanga Magharibi licha ya kuwepo kwa kampuni ya TIRIMA iliyochukuwa tenda ya kufanya usafi katika kata hiyo,  Uongozi  umekusudia kuvunja mkataba na kampuni hiyo.   Diwani wa kata ya Upanga Magharibi Adinani Kitwana Kondo amesema eneo lililopo hospitali ya Muhimbili limekithiri kwa uchafu kitendo ambacho kinahatarisha maisha ya watu wengi wanaoishi na wanaotembelea maeneo hayo.   Kondo  amesema  kampuni hiyo  ya TIRIMA imekuwa ikikusanya shilingi elfu kumi na tano kwa kila mkazi wa...

Like
389
0
Wednesday, 30 December 2015
MAPIGANO YA WAKULIMA NA WAFUGAJI YAPELEKEA VIFO VYA NG’OMBE SABINI NA TISA MVOMERO
Local News

JUMLA ya ng’ombe sabini na tisa zimeuawa kwa kipindi kinacho ishia mwezi Desemba mwaka huu   kutokana na mapigano kati ya wakulima na wafugaji yaliyotokea kwenye kijiji cha Dihinda  Tarafa ya Turiani Wilaya ya Mvomero  Mkoani Morogoro. Mkuu wa kitengo cha Habari na Mawasilano kutoka Wizara ya Mifugo ,Kilimo na Uvuvi ,JUDITH MHINA amesema kuwa kumekuwa na ukiukwaji wa haki za wanyama hususani  ng’ombe katika wilaya hiyo kwani wanyama hao wamekuwa wakiuawa bila sababu maalum. JUDITH ameeleza  kuwa kutokana na...

Like
297
0
Wednesday, 30 December 2015
FEDHA ZA MKESHA WA KUOMBEA AMANI KUTUMIKA KUSAIDIA WATU WENYE MAHITAJI HASA AFYA YA MAMA NA MTOTO
Local News

IMEELEZWA kuwa Fedha zitakazopatikana katika Tamasha la mkesha wa kuombea amani  nchini zitatumika kuwasaidia watu wenye mahitaji  hasa afya ya mama na mtoto. Hayo yamesemwa na Mwenyekiti  wa Jumuiya  wa Makanisa ya Pentekoste , ambaye pia ni Askofu wa huduma ya Tanzania Fellowship TFC,  Askofu  Godfrey  Malassy  alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam.   Askofu Malassy amesema kwamba, fedha zitakazopatikana katika tamasha hilo zitanunua vifaa vinavyotumia nishati ya jua ili kuwasaidi wamama...

Like
161
0
Tuesday, 29 December 2015
TANZANIA YAJIPANGA KUACHA KUTEGEMEA WAHISANI
Local News

WAZIRI wa Fedha na Mipango Dokta Philipo Mipango amesema kuwa wizara yake haitakuwa tayari kuona nchi ya Tanzania ikiendelea kujiendesha kwa kutegemea misaada kutoka nchi wahisani, bali itajiendesha kwa  kukusanya mapato yakutosha yaliyopo ndani ya nchi ili jamii iweze kufaidika na matumizi ya mapato hayo. Dokta mipango ameyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam  baada ya kukabidhi ofisi aliyokuwa akikaimu ya Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) kabla ya kuapishwa kuwa waziri wa fedha na mipango kwa kamishna mkuu mpya wa...

Like
180
0
Tuesday, 29 December 2015
WATUMISHI WA WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO WAASWA KUFANYA KAZI KWA WELEDI
Local News

WATUMISHI Wizara ya Fedha na Mipango wameaswa kufanya kazi kwa weledi na kuwekeza nguvu zaidi katika ukusanyaji mapato ili kukuza uchumi wa nchi na kuifanya nchi iwe kitovu cha uchumi Barani Afrika.   Hayo yamesemwa na Waziri wa Fedha na Mipango Mheshimiwa. Dokta. Philip Mpango alipokuwa akiongea na watendaji wa Wizara hiyo.   Katika mazungumzo yake na watendaji hao,  Dokta. Mpango, aliuagiza uongozi wa Wizara yake kuunda  na kusimamia sera za mfumo wa ukusanyaji  kodi ambao utabaki kuwa rafiki kwa wafanyabiashara...

Like
154
0
Tuesday, 29 December 2015
RAIS MAGUFUFULI KUHUDHURIA MKESHA WA KUIOMBEA AMANI TANZANIA
Local News

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  dokta John Pombe Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Mkesha wa kuiombea amani  Tanzania  utakaofanyika Disemba 31 mwaka huu katika uwanja wa Taifa. Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Makanisa ya Pentekoste nchini (TFC) Godfrey Malassy Cmaandalizi yote yamekamilika ikiwemo kibali kutoka polisi. Askofu Malassy ameongeza kuwa mkesha huo  utakuwa ni kwa ajili ya kumshukuru Mungu kwa kuijalia Tanzania kumaliza Uchaguzi Mkuu uliofanyika mwezi Oktoba mwaka huu kwa Amani na utulivu, pamoja...

Like
283
0
Tuesday, 29 December 2015
MAGEMBE AWASILI WIZARANI BAADA YA KUAPISHWA
Local News

WAZIRI Wizara ya Maliasili na Utalii Mhe. Prof. Jumanne Maghembe amewasili wizara kwake leo mara tu baada ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ikulu Jijini Dar es salaam. Waziri Profesa Maghembe ni miongoni mwa Mawaziri wanne walioteuliwa hivi karibuni na rais kukamilisha baraza jipya la Mawaziri katika Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dokta John Pombe Magufuli. Kufuatia hafla hivyo, hivi sasa Wizara zote zimekamilika kwa ajili ya utekelezaji wa kauli mbiu ya awamu hii ya...

Like
232
0
Monday, 28 December 2015
UFINYU WA WODI WAWALAZA KITANDA KIMOJA WAZAZI NA WATOTO
Local News

AKINAMAMA wajawazito na watoto   katika hospitali ya wilaya ya maswa  Mkoani Simiyu, wamekuwa wakilazimika kulala kitanda kimoja watu wawili na muda mwingine kupeana zamu kutokana na ufinyu wa wodi, na upungufu wa vitanda   suala ambalo linaweza kusababisha maambukizi ya magonjwa.   Kufuatia hali hiyo, wakizungumza na Efm wameiomba  serikali kuyafungua majengo  mapya  ambayo tayari yameshakamilika ili kuweza kupunguza adha hiyo.   Kituo hiki kimeshuhudia akinamama hao wakiwa wamelala wawili wawili wodini, huku baadhi...

Like
185
0
Monday, 28 December 2015
WAZIRI NAPE AKANUSHA KATAZO RASMI LA MAVAZI YA NGUO FUPI
Local News

WAZIRI wa wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye amekanusha taarifa ambazo kwa takribani siku mbili zilizopita zilienea juu ya katazo rasmi la mavazi ya nguo fupi ambalo ilisemekana limetolewa na Wizara hiyo. Akizungumza na EFM kwa njia ya simu, Mheshimiwa Nnauye amesema  Wizara imesikitishwa na Taarifa hizo na kwamba sheria zinazosimamia makosa ya kimtandao ziko wazi, hivyo anaamini mamlaka zinazohusika zitatekeleza wajibu...

Like
295
0
Monday, 28 December 2015