Local News

TEMEKE: SEKTA YA UHANDISI IMETAKIWA KUANDAA MIRADI INAYOTEKELEZEKA
Local News

MSTAHIKI MEYA wa Manispaa ya Temeke Abdallah Chaurembo ameitaka sekta ya uhandisi pamoja na Watendaji wa Manispaa hiyo kuandaa miradi michache inayotekelezeka na kuwasilisha katika kamati ya maendeleo ya manispaa hiyo badala ya kuwa na miradi mingi isiyotekelezeka. Chaurembo ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na Waandishi wa habari baada ya kufanya ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo na kubaini kuwa miradi mingi haijakamilika kutokana na sababu mbali mbali ikiwemo ufinyu wa bajeti. Aidha Chaurembo amewataka Wahandisi na Watendaji hao...

Like
226
0
Monday, 25 January 2016
WAUMINI NCHINI WAASWA KULINDA AMANI
Local News

WAUMINI wa dini zote nchini wameaswa kutojihusisha na vitendo vya kupeana majina mabaya yanayo hamasisha vurugu au uvunjifu wa amani. Wito huo umetolewa Jijini Dar es salaam na Mmoja wa Viongozi wa Kuu wa kiroho wa Waislamu Dhehebu la Shia Ithina Sheria Tanznia Sheikh Hemed Jalala alipokuwa akizungumza kwenye semina ya kujadili changamoto zinazo wakabili umma wa kiislamu nchini na duniani kwa ujumla. Sheikh JALALA amebainisha kuwa kuitana majina hayo ndio chanzo kikubwa cha kuibuka kwa vitendo vya kigaidi vinavyo...

Like
204
0
Monday, 25 January 2016
UCHIMBAJI WA KOKOTO MARUFUKU TEMEKE
Local News

MKUU wa Wilaya ya Temeke Sofia Mjema amepiga marufuku shughuli za uchimbaji Kokoto na Mchanga zinazofanyika kigamboni pamoja na maeneo mengine ya Manispaa ya Temeke kutokana na uharibifu mkubwa wa mazingira unaofanyika  kupitia shughuli hizo.   Mjema amechukua maamuzi hayo baada ya kutembelea maaneo hayo akiambatana na kamati ya Ulinzi na Usalama ya Manispaa ya Temeke ambapo amebaini uharibifu mkubwa wa mazingira unaofanyika kupitia shughuli hiyo huku akirejea Kauli ya Mkuu wa Mkoa Dar es salaam Said Meck Sadick kua...

Like
376
0
Friday, 22 January 2016
DK SHEIN AONGOZA MAZISHI YA BI ASHA BAKARI MAKAME
Local News

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dokta Ali Mohamed Shein  leo ameongoza mazishi ya marehemu Bi Asha Bakari Makame aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT). Mazishi ya Marehemu yamefanyika huko Kianga, Wilaya ya Magharibi ‘B’, Mkoa wa Mjini Magharibi kwa heshima zote za Chama Cha Mapinduzi, ambapo viongozi mbali mbali wa vyama na serikali wamehudhuria  akiwemo Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad na Makamu wa Pili wa Rais Balozi...

Like
534
0
Friday, 22 January 2016
DUKA LA DAWA LA MSD LAZINDULIWA MWANZA
Local News

WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto. Mheshimiwa Ummy Mwalimu amezindua rasmi duka la Dawa la MSD mkoani Mwanza ambalo lipo ndani ya Hospitali ya SekouToure, na kufanya maduka ya MSD yaliyofunguliwa baada ya agizo la Rais Dkt John Magufuli kufikia mawili baada ya lile la Muhimbili lililofunguliwa mwaka jana.   Katika hotuba yake ya uzinduzi wa duka hilo, Waziri Ummy ameipongeza MSD kwa hatua hiyo nzuri ya kufungua maduka ili kuwawezesha wananchi kupata dawa, na kuitaka...

Like
416
0
Friday, 22 January 2016
JK ATUNUKIWA SHAHADA YA HESHIMA YA UDAKTARI WA FALSAFA WA MAHUSIANO YA KIMATAIFA
Local News

RAIS mstaafu wa awamu ya nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete jana ametunukiwa Shahada ya heshima ya udaktari wa falsafa wa mahusiano ya kimataifa Jijini Dar es Salaam katika mahafaliya 30 ya Chuo Kikuu Huria Tanzania.   Mheshimiwa Dkt Jakaya Kikwete amesema amefarijika sana kutunukiwa shahada hiyo ya heshima itolewayo na Chuo kikuu Huria Tanzania kwa watu ambao wametoa mchango katika maendeleo ya jamii kupitia nafasi zao kiutendaji.   Maraisi wengine waliowahi kupata hiyo kutoka Chuo hicho ni Rais wa Awamu...

Like
449
0
Friday, 22 January 2016
EFM RADIO, YAKABIDHIWA ENEO LA UJENZI WA MADARASA YA SEKONDARI-KATA YA KIMARA- KINONDONI.
Local News

WILAYA ya Kinondoni kupitia Mkuu wa Wilaya hiyo inatarajia kuongeza shule za Sekondari ili kukidhi mahitaji ya wanafunzi katika Wilaya hiyo. Efm Radio 93.7 katika kuunga mkono juhudi hizo za Serikali imeahidi kujenga madarasa mawili . Mkuu wa Vipindi vya 93.7 efm Dickison Ponela akipokea mchoro wa madarasa, kutoka kwa Afisa Elimu wa Wilaya ya Kinondoni Bwana, Rogers J. Shemwelekwa Katikati ni Mhariri Mkuu wa Radio hiyo, Scholastica Mazula na Pembeni kushoto ni Injinia wa Wilaya hiyo Bwana Brighton. Mhariri...

Like
497
0
Thursday, 21 January 2016
WAFANYABIASHARA TEGETA KWA NDEFU WAIOMBA SERIKALI KUWATENGEA ENEO MAALUM LA SOKO
Local News

WAFANYABIASHARA  wa soko lisilo rasmi lililopo tegeta kwa ndevu  Jijini  Dar es salaam wameiomba serikali kuwatengea eneo maalum la kufanyia biashara zao kutokana soko la nyuki  lililotengwa  kuwa finyu  hali inayosababisha wao kuendelea kuwepo sokoni hapo.   Wakizungumza na efm Jijini  Dar es salaam Wafanya Biashara hao wamesema kuwa  kipinndi cha nyuma eneo hilo lilikuwa lipo chini ya serikali  ya mtaa ambapo kwa sasa linamilikiwa na mtu binafsi ambae ndie amewapangisha.   Kwa upande wake, Mwenyekiti  wa Soko hilo...

Like
324
0
Wednesday, 13 January 2016
MAKAA YA MAWE KUZALISHA UMEME TANZANIA
Local News

  SERIKALI imesema  itahakikisha  inafanya Makaa ya Mawe yanakuwa chanzo kingine kikubwa cha uzalishaji umeme Nchini.   Hayo yameelezwa na Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo alipotembelea  Mgodi wa Makaa ya Mawe wa Ngaka unaomilikiwa kwa ubia Kati ya Kampuni ya  TANCOAL na Serikali kupitia shirika la NDC.   Mgodi huo  upo katika Wilaya ya  Mbinga mkoani...

Like
255
0
Wednesday, 13 January 2016
GARISSA: WANAFUNZI WAREJEA CHUONI
Local News

WANAFUNZI wamerejea tena katika Chuo Kikuu cha Garissa na kuanza masomo miezi tisa baada ya chuo hicho kufungwa kutokana na shambulio la al-Shabab, Nchini Kenya. Serikali imesema imeweka usalama wa kutosha kuhakikisha kundi hilo kutoka Somalia haliwezi likashambulia tena, lakini licha ya hakikisho kutoka kwa maafisa wa usalama, ni wanafunzi wachache pekee waliorejea chuoni. Takriban wanafunzi 800 wa kufadhiliwa na serikali, waliokuwa wakisomea katika chuo hicho kabla ya shambulio kutokea, walihamishiwa chuo kikuu cha Moi mjini...

Like
176
0
Monday, 11 January 2016
CUF YAGOMA KURUDIA UCHAGUZI ZANZIBAR
Local News

WAKATI kesho ni maadhimisho ya miaka 52 ya Mapinduzi, Chama cha Wananchi –CUF, kimesema hakitakubali marudio ya uchaguzi wa urais visiwani Zanzibar. Taarifa ya chama hicho ambayo imesomwa leo na aliyekuwa mgombea wa urais wa CUF katika uchaguzi wa 25 Oktoba mwaka jana,  Maalim Seif  imeeleza kuwa hakuna hoja wala msingi wa kikatiba na kisheria wa uchaguzi  huo kurudiwa. Taarifa hiyo imeonyesha kutoa mapendekezo ya kuondolewa kwa mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Jecha Salim...

Like
210
0
Monday, 11 January 2016