E-fm na DTB Bank kwa kushirikiana na na Halmashauri ya Wilaya ya Kinondoni chini ya Mkuu wa Wilaya hiyo, Mh. Paul Makonda pamoja na waigizaji wa Bongo Movie na wananchi wa wilaya ya Kinondoni leo wametekeleza agizo la Rais Mh. John Pombe Mgufuli kwa kuitumia siku ya maadhimisho ya uhuru kufanya usafi kwenye maeneo mbalimbali ya nchi. Usafi huu ulianzia eneo la Kinondoni Moroco hadi magomeni ambapo Makamu wa Rais Mh. Samia Suluhu pia alijumuika kufanya usafi ikiwa ni pamoja na...
JUMUIYA ya Wafanyabiashara Tanzania inatarajia kufanya usafi wa Mazingira katika baadhi ya maeneo ya Manispaa ya Ilala ikiwa ni hatua ya kuunga mkono Agizo la Rais Dokta John Pombe Joseph Magufuli la kufanya usafi siku hiyo. Akizungumza na Wanahbari jijini Dar es salaam Kaimu Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Jeddah Hasabubaba amewataka Wafanyabiashara wote wa Jumuiya hiyo kujitokeza na kushiriki kufanya usafi wa mazingira. Aidha Hasabubaba ameongeza kuwa suala hilo halitokuwa suala la siku moja bali ni endelevu na kuwa wanaunga...
TUME ya Nguvu za Atomiki, Tanzania kwa kushirikiana na Shirika la Nguvu za Atomiki Duniani wanaendeshesha mafunzo ya namna ya kukabilina na matukio ya mionzi hatari yenye lengo la kutoa mwongozo jinsi ya kukabiliana na majanga yanayoweza kusababishwa na mionzi hatari ya nyuklia. Akifungua mafunzo hayo Jijini Arusha, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomiki nchini dokta Mwijarubi Nyaruba amesema kutokana na kukua kwa kasi kwa teknolojia duniani ni muhimu kwa nchi wanachama wa shirika la nguvu za...
TAASISI isiyo ya kiserikali ya- NEMA FOUNDATION imetoa msaada wa mashuka miamoja katika baadhi ya hospitali za Jijini Dar es salaam ikiwemo hospitali ya Mwananyamara ikiwa ni sehemu ya utaratibu wao ambao wanaufanya kila mwaka. Mwenyekiti wa Taasisi hiyo Bi Mariam Dedes amesema kuwa wameguswa kutoa misaada hiyo kwa kutambua changamoto mabalimbali zinazo ikabili sekta ya Afya. Kwa upande wake Mbunge wa kinondoni Muheshimiwa Mahulid Mtulya ameishukuru taasisi hiyo na kuziomba taasisi nyingine kujitokeza kutoa misaada kwenye ...
IMEELEZWA kuwa zaidi ya asilimia 15 ya wanawake nchini wamekuwa wakifanyiwa vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia . Hayo yamebainishwa jana Jijini Dar es alaamu na mkuu wa program wa mtandao wa jinsia TGNP Sikola Makwaiya wakati wa maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia ambapo amesema zaidi ya wanawake Elfu 15 nchini sawa na asilimia 15 hukumbwa na vitendo vya unyanyasaji wa kijimsia. Makwaiya ametaja baadhi ya mikoa inayoongoza kwa vitendo hivyo kuwa ni Shinyanga, Mara na...
WANANCHI wametakiwa kujitokeza kwa wingi katika kuunga mkono Juhudi za Serikali za kufanya usafi siku ya Maadhimisho ya Uhuru Disemba 9 mwaka huu ili kuweka mazingira safi na kusaidia kupunguza magonjwa ya mlipuko. Wito huo umetolewa leo Jijini Dar es salaam na Meneja Mawasiliano na Mahusiano wa Kituo cha Radio cha 93.7 Efm Denis Ssebo wakati akizungumza na waandishi wa Habari juu ya umuhimu wa zoezi hilo kwa kila mtu ambapo amesema Efm radio kwa kushirikiana na Benki ya DTB,...
KUTOKANA na utendaji mbovu wa Mamlaka ya Bandari kwa muda mrefu bila hatua zozote kuchukuliwa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta John Pombe Magufuli amevunja Bodi yote ya Bandari na kutengua uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi hiyo Profesa Joseph Msambichaka na Mkurugenzi Mkuu wa Bandari Awadhi Massawe. Aidha Mheshimiwa Rais ametengua uteuzi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Dokta Shaban Mwinjaka kuanzia leo hadi atakapopangiwa kazi nyingine. Hatua hiyo imekuja kufuatia ziara za kushitukiza zilizofanywa...
JUMUIYA ya Kimataifa imekumbushwa kuisaidia Tanzania katika kuhudumia wakimbizi kutoka nchi za Burundi na Kongo ambao wanaishi kwenye kambi ya Nyarugusu mkoani Kigoma. Kauli hiyo imetolewa na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukamilisha ziara yake mkoani Kigoma. Rodriguez amesema kwamba serikali ya Tanzania kwa miaka mingi imekuwa ikikubali kusaidia majirani zake kwa kuhifadhi wakimbizi na kuitaka Jumuiya ya...
KATIBU MKUU wa Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Omar Chambo amewaagiza madaktari wa Hospitali ya wilaya ya Kahama kuandaa utaratibu wa kuwawezesha wahanga wa Mgodi wa Nyangalata kwenda kufanyiwa uchunguzi wa Afya zao kwenye Hospitali za rufaa. Mhandisi Chambo ameyasema hayo baada ya kuwatembelea wahanga hao waliolazwa katika hospitali ya Wilaya ya Kahama kutokana na ajali ya kufunikwa na kifusi cha mgodi huo kwa muda wa siku 41. Katibu Mkuu ametoa agizo hilo kufuatia maombi yaliyotolewa na...
EFM Radio kwa kushirikiana na Benki ya DTB na Halmashauri ya Wilaya ya Kinondoni chini ya Mkuu wa Wilaya hiyo, Mh. Paul Makonda, tumeamua kuunga mkono na kutekeleza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta John Pombe Magufuli la kuadhimisha Siku ya Uhuru 09/12/ 2015 kwa kufanya Usafi: ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuondoa ama kumaliza kabisa tatizo la magonjwa ya mlipuko ikiwemo Kipindupindu. EFM na DTB Bank, tutashirikiana na wakazi wa Mji huu wa...
ZAIDI ya mitambo ya sola 30 imetolewa kwa jamii mbalimbali yenye uhitaji zikiwemo Zahanati, vituo vya afya, ofisi za watendaji kata na shule mbalimbali kwa ajili ya kuwasaidia kuboresha huduma zao wanazotoa kwa jamii. Hayo yamesemwa na Meneja masoko wa kampuni ya Sola ya Mobisol Seth- Joseph Zikhali wakati akizungumza na waandishi wa habari katika hafla ya kutangaza ofa mpya ya msimu wa sikukuu kwa wateja...