Local News

WATUMISHI OFISI YA WAZIRI MKUU WATAKIWA KUHUDUMIA WANANCHI
Local News

WAZIRI MKUU wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Majaliwa Kassim Majaliwa amewataka wafanyakazi wa Ofisi ya Waziri Mkuu watambue jukumu walilonalo la kuwahudumia wananchi kutokana na majukumu ya ofisi hiyo.   Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo jana wakati akizungumza na wakuu wa Taasisi, wakurugenzi na watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu kwenye mkutano uliofanyika ofisini kwake, Magogoni, jijini Dar es Salaam.   Mbali na hayo amewataka watumishi hao kuwa tayari kutekeleza kaulimbiu ya ‘Hapa Kazi Tu’ambayo imekuwa ikisisitizwa na Rais...

Like
256
0
Tuesday, 24 November 2015
CHANGAMOTO YA UKOSEFU WA MITAJI YAWAKABILI WASINDIKAJI WADOGO WA MAFUTA YA MBEGU YA ALIZETI
Local News

KUTORATIBIWA kwa mbegu za Alizeti na ukosefu wa mitaji umeelezwa kuwa changamoto kubwa kwa wasindikaji wadogo wa mafuta ya mbegu ya alizeti katika uendeshaji wa viwanda.   Hayo yameelezwa na Wakala wa uendelezaji Kongano la Mafuta ya Alizeti wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo la Viwanda (UNIDO) Vedastus Timothy wakati akizungumza na waandishi wa habari walioambatana na Mratibu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania, Alvaro Rodriguez.   Timothy amesema kwamba pamoja na kuwepo kwa taarifa za...

Like
292
0
Monday, 23 November 2015
WANAFUNZI WENYE MAHITAJI MAALUM VYUO VIKUU WAMEASWA KUTUMIA ELIMU KUJILETEA MAENDELEO
Local News

WANAFUNZI wenye mahitaji maalum wanaosoma vyuo vikuu nchini wameaswa kutumia elimu wanayoipata ili kuendesha maisha yao na kujiletea maendeleo yao na taifa kwa ujumla.   Hayo yamesemwa na Mgeni rasmi wakati wa Mahafali ya nane ya Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaama (DUCE) Profesa  Martha Qorro yaliyofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita jijini Dar es salaaam.   Profesa Qorro amesema kuwa mwamko wa wanafunzi wenye mahitaji maalum kujiunga na elimu ya juu nchini ni mzuri licha ya changamoto zinazowakumba...

Like
380
0
Monday, 23 November 2015
RAIS WA IRELAND ATUMA SALAMU ZA PONGEZI KWA MAGUFULI
Local News

RAIS wa Ireland, Michael Higgins amemtumia Salamu za Pongezi  kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mheshimiwa dokta John Pombe Magufuli kwa kuchaguliwa kwake kuwa Rais wa Awamu ya Tano. Katika Salamu zake hizo, Rais Higgins amesema Ireland na Tanzania zimekuwa na uhusiano mzuri na wa kirafiki kwa miaka mingi, hivyo ana matarajio kwamba katika kipindi cha uongozi wa Rais Magufuli, uhusiano huo utaimarishwa zaidi. Katika hatua nyingine Rais wa  Jamhuri ya Zimbabwe, Mheshimiwa Robert Mugabe amemtumia Salamu za...

Like
221
0
Friday, 20 November 2015
RAIS MAGUFULI AHUTUBIA BUNGE KWA MARA YA KWANZA
Local News

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mheshimiwa dokta John Pombe Magufuli amelihutubia Bunge la Tanzania ikiwa ni mara ya kwanza kulihutubia na kulifungua rasmi Tangu aingie Madarakani. Katika hotuba yake Rais Magufuli ameeleza mikakati yake na vipaumbele vyake vitakavyowaletea maendeleo wananchi pamoja na Taifa kwa ujumla na mwelekeo wa kiuchumi. Kabla ya kulihutubia Bunge Rais Magufuli leo asubuhi amemwapisha rasmi Waziri Mkuu wa Serikali ya Awamu ya Tano mheshimiwa Majaliwa Kassim...

Like
399
0
Friday, 20 November 2015
UKOSEFU WA USHIRIKIANO NI KIKWAZO CHA ELIMU YA MSINGI TABORA
Local News

USHIRIKIANAO mdogo kati ya wazazi, walimu na wanafunzi mkoani TABORA umetajwa kuwa ni sehemu ya vikwazo vya kimaendeleo ya elimu ya msingi mkoani humo. Hayo yamebainishwa na wadau mbalimbali wa elimu mkoani TABORA walioshiriki mdahalo wa masuala ya elimu uliohoji anguko la elimu mkoani humo. Moja ya vitendo vilivyotajwa kufanywa na wazazi ni pamoja na kuwepo kwa hisia za vitendo vya kishirikina hali inayotajwa kukimbiza walimu wengi wanaopangwa kufundisha shule za msingi mkoani...

Like
178
0
Friday, 20 November 2015
RAIS MAGUFULI AMUAPISHA WAZIRI MKUU WA SERIKALI YA AWAMU YA TANO
Local News

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mheshimiwa dokta John Pombe Magufuli amemuapisha Waziri Mkuu Mteule wa Serikali ya awamu ya Tano Mheshimiwa Majaliwa Kassim Majaliwa Ikulu Ndogo iliyopo Chamwino Mkoani Dodoma ambapo baadaye pia atalihutubia Bunge la Tanzania. Viongozi mbalimbali wameshirki katika Zoezi la kumuapisha Waziri Mkuu Mteule akiwemo makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hata hivyo Watanzania wengi wanatarajia kusikia mikakati ya Mheshimiwa Rais dokta Magufuli atakayoitekeleza ikiwemo aliyowaahidi wakati wa Kampeni...

Like
153
0
Friday, 20 November 2015
SERIKALI IMETAKIWA KUTUNGA NA KUBORESHA SERA ZA KUPAMBANA NA UKATILI
Local News

SERIKALI imetakiwa kuhakikisha inatunga na kuboresha sera za kupambana na ukatili wa kijinsia hasa kwa wanawake katika masoko na maeneo mbalimbali nchini. Hayo yamesemwa leo Jijini  Dar es Salaam na Mratibu wa Kituo cha Usuluhisho cha Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania-TAMWA,  Gladness Munuo wakati kizungumza kwenye semina ya kuwajengea uwezo wafanyabiashara wa soko la Ilala juu ya namna ya kutoa habari za unyanyasaji wa kijinsia kwa waandishi wa habari. Aidha MUNUO ameeleza kuwa mifumo dume ya uongozi nchini imekuwa haitoi...

Like
146
0
Thursday, 19 November 2015
BUNGE LIMEPOKEA NA KUTHIBITISHA UTEUZI WA KASSIMU MAJALIWA KUWA WAZIRI MKUU
Local News

BUNGE la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limepokea na kuthibitisha Uteuzi wa jina la Waziri Mkuu wa serikali ya awamu ya Tano ambaye ni mheshimiwa Majaliwa Kassim Majaliwa Mbunge wa Jimbo la Ruangwa Mkoani Lindi kupitia chama cha mapinduzi-CCM. Akitangaza jina hilo Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai amewaeleza wabunge kuwa kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inampa Rais Mamlaka ya kuteua jina la Waziri Mkuu na kuliwasilisha bungeni kwa ajili ya kuthibitishwa na wabunge. Mheshimiwa...

Like
305
0
Thursday, 19 November 2015
TAASISI YA MISA YAZINDUA RIPOTI MAALUM KUANGALIA HALI YA VYOMBO VYA HABARI
Local News

TAASISI ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika-MISA-kwa kushirikiana na Taasisi binafsi ya Friedrich Ebert Stiftung jana imezindua rasmi ripoti maalum ya kuangalia hali ya Vyombo vya habari ilivyo nchini kwa kuangazia masuala muhumu ya kiutafiti kwa nia ya kupima mwenendo na hali ya vyombo vya habari.   Ripoti hiyo imelenga kutoa uchambuzi wa hali halisi ya namna Vyombo vya Habari nchini vinavyofanya kazi zake kwa uhuru na kwa kuzingatia sera, sheria na kanuni za uendeshaji wa vyombo hivyo.   Akizungumzia...

Like
309
0
Thursday, 19 November 2015
RAIS MAGUFULI AMTEUA KASSIM MAJALIWA KUWA WAZIRI MKUU
Local News

BUNGE la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limepokea jina la Waziri Mkuu wa serikali ya awamu ya Tano ambaye ni mheshimiwa KASSIM MAJALIWA Mbunge wa Jimbo la Ruangwa Mkoani Lindi kupitia chama cha mapinduzi-CCM. Akitangaza jina hilo Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai amewaeleza wabunge kuwa kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inampa Rais Mamlaka ya kuteua jina la Waziri Mkuu na kuliwasilisha bungeni kwa ajili ya kuthibitishwa na wabunge. Kabla ya kutajwa kwa jina lake...

Like
286
0
Thursday, 19 November 2015