KATIKA kuhakikisha wananchi wanapata huduma za Afya kwa bei nafuu Mfuko wa Hifadhi ya Jamii-PSPF-pamoja na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya-NHIF-wamesaini mkataba wa kutoa huduma hizo kwa wanachama waliojiunga na mpango wa uchangiaji wa hiari wa PSP. Akizungumza na Wadau mbalimbali wa Afya Jijini Dar es Salaam leo Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Michael Mhando amesema kuwa wanachama hao watachangia kiasi cha shilingi Elfu 76 na 800 kwa mwaka ambapo wataweza kupata huduma bora za afya katika...
MABADILIKO ya Tabia Nchi, uharibifu wa vyanzo vya maji katika mito mbalimbali na uchepushaji wa maji kwa ajili ya shughuli za kilimo na ufugaji ni chanzo cha kukauka kwa mabwawa ya maji yanayotumika katika kuzalisha umeme. Hayo yamesemwa jijini Dar es salaam na msemaji wa Wizara ya Nishati na Madini Bi. Badra Masoud alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ukaguzi wa wezi wa umeme nchini. Akizungumzia hali ya umeme nchini, Badra amesema kuwa kwa sasa hakuna mgawo...
WANAWAKE wajawazito nchini wameshauriwa kufuata kanuni bora za Afya ikiwemo kuhudhuria Hospitalini mara kwa mara ili waweze kuepuka kujifungua watoto njiti. Akizungumza Jijini Dar es Salaam wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya watoto waliozaliwa kabla ya miezi 9, Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadick amesema kuwa endapo wanawake watatimiza lengo la kuhudhuria Hospitalini na kufuata ushauri wanaoupata kutoka kwa madaktari kuna uwekano wa tatizo hilo kupungua. Aidha, Sadick amewataka wanaume kutoa ushirikiano wa kutosha...
BUNGE la kumi na moja la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limeendelea leo kwa kikao cha pili kinachoenda sambamba na zoezi la Kiapo cha Uaminifu kwa wabunge wote. Hiyo imekuja baada ya jana Bunge hilo kufanikiwa kumpata Spika Mheshimiwa Jobu Ndugai atakayeliongoza kwa kipindi cha miaka mitano. Mheshimiwa Ndugai alishinda nafasi hiyo baada ya kupata jumla ya Kura 254 kati ya 365 zilizopigwa na wabunge wote ambayo ni sawa na asilimia...
MANISPAA ya Kinondoni kwa kushirikiana na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, kama msimamizi na mtekelezaji wa sera ya Taifa ya Ardhi, inakusudia kuendesha zoezi la kubomoa nyumba zilizojengwa bila kufuata taratibu za ujenzi. Sera ya Taifa ya Ardhi imebainisha sababu inayosababisha Wizara kushirikiana na Manispaa ya Kinondoni kuendesha zoezi hilo la ubomoaji kwa kuhusisha nyumba zote zilizojengwa Bila kibali cha ujenzi na Bila kufuata michoro ya mipango miji Maeneo ambayo ujenzi wake umekiuka matumizi yaliyokusudiwa na...
ALIYEKUWA Mgombea wa nafasi ya Uspika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jobu Ndugai amefanikiwa kushinda nafasi hiyo baada ya kushinda katika Uchaguzi uliofanyika leo Bungeni mjini Dodoma. Mwenyekiti wa Muda wa kikao cha kumpata Spika, mheshimiwa Andrew Chenge amesema Mheshimiwa Ndugai ameshinda nafasi hiyo baada ya kupata kura 254 sawa na Asilimia 70 kati ya kura 365 zilizopigwa na wabunge wote wa Bunge hilo. Kwa upande wake Spika wa bunge hilo Mheshimiwa Jobu Ndugai amewashukuru...
UTAFITI uliofanywa na Chama cha Afya ya jamii (TPHA) unaonesha kwamba kati ya watoto 200 Asilimia sita ya watoto hao wanajihusisha na uvutaji wa Tumbaku. Akazingumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam Mratibu kutoka chama cha Afya ya jamii (TPHA), BERTHA MAEGA amesema kuwa utafiti huo umehusisha watoto wa shule ya msingi kuanzia darasa la nne hadi la sita huku wengi wao wakikiri kushawishiwa na wazazi na marafiki. BERTHA amesema kuwa ili kuweza kudhibiti tatizo hilo kuna umuhimu...
BUNGE la kumi na moja la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limeanza kikao chake cha kwanza kwa mchakato wa kumpata Spika wa Bunge hilo atakayeongoza kwa muda wa miaka mitano. Miongoni mwa wagombea wanaowania Nafasi ya Uspika ni pamoja na Jobu Ndugai kutoka-CCM, Goodluck Ole Medeye wa CHADEMA, Peter Sarungi wa AFP, Hassan Almas kutoka NRA na Godfrey Malissa wa chama cha CCK. Hata hivyo Baada ya kukamilika kwa Uchaguzi wa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania...
KAMATI ya Wabunge wote wa chama cha Mapinduzi-CCM-imempitisha Ndugu Job Ndugai kuwa mgombea wa Uspika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kufuatia wagombea wenzake wa chama hicho kujitoa katika kinyang’anyiro hicho. Akizungumza mara baada ya kupitishwa kwa mgombea huyo, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa-CCM-Nape Nnauye amesema wana imani na Ndugai kuwa atashinda katika nafasi hiyo kutokana na uwezo wake wa kuongoza. Kabla ya Ndugai kutangazwa kuwa ndiye atakayewania Uspika, wengine waliokuwepo katika kinyang’anyiro hicho ni...
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa dokta John Pombe Magufuli amepokea salamu za pongezi kutoka kwa Malkia Elizabeth II wa Uingereza kufuatia kuchaguliwa kwake kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Katika salamu hizo Malkia Elizabeth amemueleza Rais dokta Magufuli kuwa anatumaini mahusiano baina ya nchi hizi mbili ambazo ni wanachama wa Jumuiya ya Madola yataendelea kuwa mazuri wakati wa utawala wake. Katika hatua nyingine Mfalme Akihito wa Japan amemueleza Mheshimiwa Magufuli nchi yake ipo...
JAMII ya wafugaji imetakiwa kutumia juhudi katika kubadili mitazamo ya watu juu ya matumizi ya mila na desturi ili kusaidia kutokomeza vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia na kuleta maendeleo kwa Taifa. Wito huo umetolewa na Mtaalamu wa masuala ya vyombo vya habari vya kijamii Bi. Rose Haji Mwalimu wakati akiwasilisha mada kwenye kongamano la viongozi wa mila wa kabila la wamasai na wanawake Mashuhuri lenye lengo la kushawishi uondoaji wa mila potofu zinazorudisha nyuma maendeleo. Bi. Rose amewataka...