Mamilioni ya watoto wanaweza kupoteza maisha kutokana na maradhi yanayoweza kuzulika kwa sababu ya kukatizwa kwa programu za chanjo kutokana na virusi vya corona ambapo wataalam wametahadharisha. Shirika la Afya duniani limeshauri nchi nyingi kusitisha chanjo ili kusaidia kudhibiti kuenea kwa virusi vya corona ambapo takribani nchi 68 zimeathirika na baadhi zikisitisha kabisa kampeni za chanjo. Lakini sasa makundi kadhaa ya wataalamu wanaona kuwa kutakuwa na madhara ya muda mrefu kutokana na hali hii Mfuko wa Umoja wa Mataifa unaoshughulikia...
Kimataifa Maandamano juu ya kifo cha raia mweusi wa Marekani George Floyd bado yanaendelea kwa usiku wa nane mfululizo. Kifo cha Floyd kilichotokea Mei 25, mikononi mwa polisi huko Minneapolis kimesababisha maandamano makubwa katika maeneo mbalimbali nchini huko. Waandamanaji wameamua kukiuka hatua ya kusalia ndani iliyowekwa katika miji mbalimbali. Katika eneo la Fort Worth, Texas, inasemekana kundi dogo la watu lilisalia nje hata baada ya kuanza kwa muda wa kutoka nje saa mbili usiku. Waandamanaji katika mji wa New York...
Waafrika wenye rangi nyeusi huwa na wakati mgumu pale wanapohitaji tiba ya dawa kwa sababu wanawakilisha asilimia mbili tu ya sampuli ya vina saba iliyotumika na utafiti wa kutengeneza dawa, lakini kampuni mpya ya Nigeria inataka kubadili mumo huo. Uhaba wa tafiti kuhusu watu wa aina fulani unahatarisha kuenea kwa magonjwa duniani kote. Kwa mujibu wa muasisi na mkurugenzi wa kampuni inayoangazia biolojia ya vina saba ‘ 54gene’ , Dkt. Ene-Obong, watu wenye rangi nyeusi wako na utofauti wa kimaumbile...
Kifaa kilicho na muhuri maalum wa kuwatambua wanyanyasaji wa kingono katika magari ya usafiri wa umma kimezinduliwa nchini Japan. Kifaa hicho kinamfahamisha muathiriwa kuwa kuna mtu anampapasa na kuwawekea alama ya wino ambayo hauonekani. Watu wanaweza kuwatambua wanyanayasaji wa kingono waliowekwa alama hiyo kwa kutumia taa nyeusi kuwabaini. Shirika la kiteknolojia lililobuni kifaa hicho linasema kiitasaidia kukabiliana na uhalifu wa kingono. Hata hivyo shirika moja lisilokuwa na kiserikali linanahofia kifaa hicho kinaweza kutumika vibaya na...
Shambulio la angani la serikali ya Syria uliolenga msafara wa kijeshi wa Uturuki uliokuwa ukielekea katika eneo linalotawaliwa na waasi kaskazini mwa Syria limesababisha vifo vya raia watatu, Uturuki imedai. Watu wengine 12 walijeruhiwa katika shambulio hilo katika mkoa wa Idlib siku ya Jumatatu kulingana na wizara ya ulinzi ya Uturuki. Idlib ambayo ni mojawapo ya maeneo machache yasiodhibitiwa na serikali, ilitarajiwa kulindwa na kuwa eneo huru linalotenganisha majeshi pinzani lililoafikiwa na Uturuki inayowaunga mkono waasi mwaka uliopita....
Korea kaskazini imepinga mazungmzo ya ziada ya Korea kusini, na kusema uamuzi huo ni “makosa ya hatua za Korea kusini”. Imetoa taarifa kufuatia hotuba ya rais wa Korea kusini Moon Jae-in hapo jana Alhamisi. Wakati huo huo, mapema leo Ijumaa Korea kaskazini imefyetua makombora mawili baharini kutoka pwani ya mashariki, jeshi la Korea kusini limearifu. Likiwa ni jaribio la sita la aina hiyo, na linafanyika chini ya mwezi mmoja. Makombora hayo mawili “ambayo hayakutambuliwa ” yalifyetuliwa mwendo wa saa mbili...
Madaktari wa magonjwa ya wanawake wameonya kuhusu hatari inayotokana na kutumia mvuke wa moto kwenye sehemu za siri, baada ya kutokea kuwa mwanamke mmoja alijiunguza sehemu zake za siri baada ya kutumia mvuke wa maji kufusha sehemu za siri. Mwanamke huyo alikuwa na tatizo la kubadilika muundo wa maumbile ya sehemu zake za siri (prolapsed vagina) kitaalamu, na kuamini kuwa tiba hiyo itamfanya akwepe kufanyiwa upasuaji. Kufusha kwa mvuke sehemu za siri, kitendo ambacho uhusisha kukaa kwenye chombo chenye maji...
Korea kaskazini imefyatua kombora la masafa mafupi ambalo halijabainika mara mbili , kwa mujibu wa maafisa wa Korea Kusini , katika jaribio la tatu la silaha hizo katika kipindi cha wiki moja pekee. Ufyatuaji wa makombora hayo ulifanyika katika eneo la mwambao wa mashariki mwa taifa hilo mapema Ijumaa. hatua hiyo inaonekana kama hatua ya taifa hilo inayolenga kujibu mazoezi ya kijeshi ya baina ya Korea Kusini na Marekani yanayotarajiwa kuanza mwezi huu. Wakati huo huo Uingereza, Ufaransa na Ujerumani...
Mwana wa kiume wa muasisi wa al-Qaeda Osama Bin Laden, Hamza,amefariki , kwa mujibu wa maafisa wa ujasusi wa Marekani. Taarifa kuhusu mahala au tarehe ya kifo cha Hamza Bin Laden bado haijawa wazi katika ripoti ya chanzo hicho cha habari. Mwezi Februari, Serikali ya Marekani iliahidi kutoa dola milioni 1 kwa ajili ya yeyote atakayetoa taarifa zitakazosaidia kutambua ni wapi alipo. Hamza Bin Laden, anayedhaniwa kuwa na umri wa miaka 30, alikuwa ametoa ujumbe mbalimbali wa sauti na video...
Zaidi ya watu milioni 820 au 10.8% duniani bado wanakabiliwa na njaa, inasema ripoti ya Umoja wa Mataifa wakati dunia ikiadhimisha siku ya njaa siku ya njaa. Kiwango cha njaa kimepanda karibu katika maeneo yote ya Afrika, na kulifanya bara la Afrika kuwa kanda yenye idadi kubwa ya watu wenye utapiamlo, kwa takriban asilimia 20, ikifuatiwa na Asia ambako zaidi ya asilimia 12 ya wakazi wa bara hilo wana tatizo hilo. Asilimia 7 ya watu wa Amerika Kusini na Caribbean...
Matamshi ya mbunge wa Starehe nchini Kenya Charles ‘Jaguar’ Kanyi kuhusu kuwatishia raia wa kigeni wanaofanya kazi nchini Kenya yaliwasilishwa mbele ya kikao cha bunge ili kujadiliwa. Hatua hiyo inajiri huku Mbunge huyo akizuiliwa katika kituo cha polisi usiku kucha ambapo anasubiri kuwasilishwa mahakamani siku ya Alhamisi. Kulingana na mtandao wa runinga ya Citizen nchini Kenya, licha ya wabunge wengi kushutumu jinsi ambavyo bwana Jaguar alitoa hoja yake , baadhi yao walikubaliana kwamba kuna swala tata kuhusiana na raia wa...