Global News

UGIRIKI YAJITOA MHANGA KULIKABILI DENI LAKE
Global News

SERIKALI ya Ugiriki imeleezea imani yake kwamba mkataba kuhusu madeni yake, utafikiwa ndani ya saa arobaini na nane, licha ya kupinga muda wa mwisho uliowekwa na nchi za Ulaya zinazotumia sarafu ya euro. Mkutano wa mawaziri kutoka nchi za Ulaya zinazotumia sarafu ya euro waliokutana mjini Brussels, Ubalegiji ulivunjika mapema kuliko ulivyotarajiwa wakati serikali ya Ugiriki ilipo tupilia mbali fursa iliyotolewa kwa nchi hiyo hadi Ijumaa kuhusu mpango wa nchi hiyo kudhaminiwa, au kuona mipango ikiisha kufikia mwishoni mwa mwezi...

Like
211
0
Tuesday, 17 February 2015
HALI BADO TETE UKRAINE LICHA YA MAKUBALIANO YA KUSITISHA MAPAMBANO
Global News

WANADIPLOMASIA wamesema Wanachama 15 wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa watakuwa na mashauriano zaidi juu ya usitishaji mapigano Mashariki mwa Ukraine, lakini bado hawapo tayari kupitisha maazimio. Baraza hilo la Amani na Usalama Duniani linatarajiwa kupiga kura juu ya rasimu ya maazimio dhidi ya Urusi inayotaka pande zote kutekeleza mpango uliotoa nafasi ya kusitishwa kwa mapigano kulikoanza siku ya Jumapili. Licha ya makubaliano hayo, milio ya mizinga imekuwa ikisikika Mashariki mwa...

Like
279
0
Monday, 16 February 2015
MISRI YAFANYA MASHAMBULIZI YA ANGA DHIDI YA IS LIBYA
Global News

MISRI imefanya mashambulizi ya angani dhidi ya wanamgambo wa dola la Kiislamu nchini Libya, baada ya wanamgambo hao kutoa mkanda wa Video, ulioonyesha mauaji ya Wakristo wa madhehebu ya Koptik ambao ni raia wa Misri. Waumini hao wameuawa kwa kukatwa vichwa walikuwa wamechukuliwa mateka na kundi hilo kwa wiki kadhaa. Msemaji wa jeshi la Misri ametangaza mashambulizi hayo leo kupitia Radio ya Kitaifa nchini humo, tangazo lililoashiria Misri kukiri kwa mara ya kwanza hadharani kufanya operesheni ya Kijeshi katika nchi...

Like
279
0
Monday, 16 February 2015
WAKIMBIZI 2000 KUTOKA LIBYA WAOKOLEWA ITALIA
Global News

ITALIA imefanikiwa kuokoa Wakimbizi Elfu-2 waliokuwa wakisafiri kwa boti kutoka Libya kuelekea Ulaya. Wakimbizi hao walikuwa kwenye Meli ya Jeshi na boti za Shirika la Uokozi Baharini na pia kwenye boti za Polisi wa Mpakani. Hata hivyo Wizara ya Uchukuzi ya Italia imeeleza kuwa baadhi ya waokozi wametishiwa na wanaume waliokuwa wamebeba Silaha na ambao wanaaminika kuwa ndio waliowasafirisha Wakimbizi hao.  ...

Like
280
0
Monday, 16 February 2015
SHAMBULIO LA KUJITOA MHANGA LAUA 16 NIGERIA
Global News

POLISI mjini Damaturu, Nigeria, imesema Mshambuliaji wa Kike wa kujitoa Mhanga amejilipua katika Kituo kimoja cha Basi kilichokuwa kimejaa watu mjini humo na kusababisha vifo vya watu 16 huku wengine zaidi ya 30 wakijeruhiwa. Mji wa Damaturu ulioko Kaskazini Mashariki mwa Nigeria umekuwa ukishambuliwa mara kwa mara na wanamgambo wa Boko Haram. Mtu mmoja aliyeshuhudia tukio hilo amesema amesema amesikia mlipuko uliosababisha taharuki katika eneo...

Like
318
0
Monday, 16 February 2015
KILELE CHA MAZUNGUMZO JUU YA MGOGORO WA UKRAINE KUFIKIWA HIVI KARIBUNI
Global News

MSEMAJI wa Ikulu Nchini Urusi amesema leo hii kwamba viongozi wa Urusi,Ukraine na Ujerumani wanaendelea kuwasiliana juu ya suala la mzozo wa Ukraine na kwamba anatarajia mazumgumzo hayo kwa njia ya simu yatafikiwa siku chache zijazo. Dmitry Peskov amesema serikali ya Urusi inatarajia vipengele vyote vilivyomo katika makubaliano ya kusitisha mapigano yaliofikiwa Minsk vitatekelezwa. Usitishaji wa mapigano katika eneo zima la  mzozo unatakiwa uanze Jumapili ambapo pande zote mbili zinatakiwa zianze kuondowa silaha nzito kutoka kwenye medani ya...

Like
248
0
Friday, 13 February 2015
BOKO HARAM YAISHAMBULIA CHAD KWA MARA YA KWANZA
Global News

KUNDI la jihad lililoko Nigeria, Boko Haram, kwa mara ya kwanza limeishambulia Chad. Wakuu nchini humo wanasema kuwa, wapiganaji wa Boko Haram walivuka ziwa Chad kwa maboti usiku na kushambulia kijiji cha Ngouboua, kilichoko kandokando ya ziwa hilo. Majeshi ya Chad yanasemekana kuwarudisha nyuma wapiganaji hao ambao wanadhibiti eneo kubwa la ziwa hilo upande wa Nigeria....

Like
303
0
Friday, 13 February 2015
DRC: TUME YA UCHAGUZI YAFURAHISHA WAPINZANI
Global News

UPINZANI nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo umepokea kwa furaha hatua ya tume ya uchaguzi ya nchi hiyo kutangaza tarehe ya uchaguzi. Hapo jana Tume ya Uchaguzi nchini humo ilitangaza uchaguzi mkuu wa rais na wabunge utafanyika Novemba 27 mwaka 2016 na kutanguliwa na uchaguzi wa serikali za mitaa baadae mwaka huu. Kutangazwa kwa tarehe hiyo ya uchaguzi mkuu kunakuja wiki chache baada ya ghasia zilizotokea katika miji kadhaa nchini humo kupinga sheria ya uchaguzi mbayo ingesogeza mbele tarehe uchaguzi....

Like
258
0
Friday, 13 February 2015
BUNGE LA AFRIKA KUSINI LAGEUKA UWANJA WA MAPAMBANO
Global News

BUNGE la Afrika kusini liligeuka kuwa uwanja wa vita ambapo wabunge wa upinzani ilifikia hatua ya kuvutana mashati na maafisa wa usalama na kufanya wabunge wa upinzani wa chama cha Economic Freedom Fighters (EFF) wakiongozwa na Julias Malema kutolewa nje ya ukumbi wa bunge kwa nguvu na baadae wabunge wengine wa upinzani nao wakatoka nje ya ukumbi. Sakata hilo lilizuka wakati Rais wa nchi hiyo Jacob Zuma alipokuwa akilihutubia taifa na kuulizwa maswali na wabunge wa chama cha EFF kinachoongozwa...

Like
238
0
Friday, 13 February 2015
MAREKANI KUCHUNGUZA MAUAJI YA WANAFUNZI WATATU WA KIISLAMU
Global News

POLISI nchini Marekani inachunguza iwapo mauaji ya wanafunzi watatu wa Kiislamu siku ya Jumanne yalichochewa na chuki dhidi za kidini, wakati ambapo miito inazidi kutolewa kwa mauaji hayo kuchukuliwa kama kosa la chuki. Mtu aliefanya mauaji hayo Craig Stephen Hicks mwenye umri wa miaka 46, ameshtakiwa kwa makosa matatu ya mauaji ya daraja la kwanza, baada ya mauaji hayo katika mji wa Chapel Hill, kusababisha ghadhabu miongoni mwa Waislamu duniani kote. Polisi imesisitiza kuwa uchunguzi wa awali ulionyesha mgogoro kati...

Like
239
0
Thursday, 12 February 2015
RAIS WA UKRAINE ASISITIZA USITISHAJI WA MAPIGANO BILA MASHARTI
Global News

MAZUNGUMZO tete ya amani mjini Minsk kati ya viongozi wa Ukraine, Urusi, Ujerumani na Ufaransa yemendelea hadi leo, wakijadili mpango wa kukomesha mapigano ya miezi 10 nchini Ukraine. Mwanzoni mwa mazungumzo hayo marefu, rais wa Ukraine Petro Poroshenko amesisitiza juu ya usitishaji mapigano usio na masharti yoyote. Chanzo kilicho karibu na mazungumzo hayo kilisema viongozi hao walipanga kusaini taarifa ya pamoja inayotoa mwito wa kutekelezwa kwa mpango wa amani wa awali uliyosainiwa kati ya serikali ya Kiev na waasi mwezi...

Like
208
0
Thursday, 12 February 2015