Global News

CHUO KIKUU MAKERERE KUCHUNGUZA KASHFA YA SHAHADA BANDIA
Global News

CHUO KIKUU cha Makerere nchini Uganda kimeanzisha uchunguzi kuhusu madai ya kashfa ya shahada bandia katika chuo hicho. Uchunguzi huo unataka kujua ni mazingira gani yaliyosababisha wanafunzi 600 kati ya wote waliofuzu zaidi ya elfu 11 kuwekwa katika orodha ya waliohitimu bila ya kufikisha viwango vya kuwafanya kufuzu. Chuo kikuu cha Makerere kinaorodheshwa kama taasisi ya elimu ya saba bora katika kanda za Afrika mashariki na kati na Afrika Magharibi....

Like
309
0
Thursday, 12 February 2015
DRC: MASHIRIKA YA KIRAIA YAMEIOMBA UN KUFIKIRIA UPYA MPANGO WA KUJIONDOA KWENYE MAPAMBANO DHIDI YA FDLR
Global News

MASHIRIKA mbali mbali ya kiraia nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo yameomba majeshi ya Umoja wa Mataifa ya kulinda amani nchini humo MUNUSCO kufikiria upya mpango wake kujiondoa kupambana na kundi la waasi la FDLR. Hapo jana majeshi ya kulinda amani ya Umoja wa Mataifa yaliyopo Jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo yalitangaza kujiondoa katika operesheni hiyo kwa kushirikiana na majeshi ya serikali ya DRC hadi hapo serikali ya Kongo itakapotengua uteuzi wa majenerali wawili walioteuliwa kuongoza opereshini hiyo. Kwa mujibu...

Like
251
0
Thursday, 12 February 2015
OBAMA KUSUBIRI MAAUMUZI YA NGAZI ZA JUU MGOGORO WA UKRAINE
Global News

RAIS Barack Obama  wa Marekani amesema atasubiri matokeo ya mazungumzo ya ngazi ya juu kuhusu Ukraine kabla ya kuamua kama Marekani itume silaha kwa serikali ya Ukraine. Wakati akisema anapendelea  diplomasia, Obama  aliweka wazi suala la kuipa silaha serikali mjini Kiev. Rais huyo wa Marekani ameyasema hayo katika mazungumzo yake na Kansela wa Ujerumani Angela Merkel jana mjini Washington....

Like
271
0
Tuesday, 10 February 2015
MALAYSIA: KIONGOZI WA UPINZANI APIGWA MIAKA 5 JELA KWA KOSA LAKULAWITI
Global News

MAHAKAMA ya juu nchini Malaysia leo imethibitisha hukumu ya awali dhidi ya kiongozi wa upinzani Anwar Ibrahim kwa kosa la kufanya  mapenzi na mwanamme mwenzake, kesi inayoangaliwa nje na ndani ya nchi hiyo kuwa ni njama ya kisiasa kumaliza  mwanasiasa huyo ambaye ni kitisho kwa serikali. Jaji wa mahakama ya Shirikisho Arifin Zakat amesema  madai ya  msaidizi wa Anwar kuwa alimtongoza  na kuwa na uhusiano naye yana uzito na kwamba hukumu ya kifungo cha miaka mitano jela iliyopitishwa na mahakama...

Like
342
0
Tuesday, 10 February 2015
MAREKANI KUWAKABILI WAASI UKRAINE
Global News

RAIS wa Marekani Barack Obama amesema kuwa Marekani inatafakari kupeleka silaha nchini Ukraine kusaidia kukabiliana na Waasi wanaoiunga mkono Urusi. Akizungumza katika Ikulu ya White House baada ya mazungumzo na Kansela wa Ujerumani Angela Markel, Obama amesema nia itakuwa kuisaidia Ukraine kuimarisha ulinzi kuliko kulishinda jeshi la Urusi. Kwa upande wake Kansela wa Ujerumani Angela Markel amesema haoni kama njia za kijeshi zinaweza kuumaliza mzozo huo....

Like
216
0
Tuesday, 10 February 2015
MAMA SALMA AWATAKA WAKAZI WA LINDI KUTOUZA MAENEO YA UFUKWE WA BAHARI
Global News

MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia wilaya ya Lindi mjini Mama Salma Kikwete amewataka wakazi wa wilaya hiyo kutokubali kuuza maeneo ya ufukwe wa Bahari  ya Hindi kwa kiasi kidogo cha fedha  kwani thamani ya maeneo hayo ni kubwa. Mama Kikwete ambaye ni Mke wa Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ametoa rai hiyo wakati akiongea  kwa nyakati tofauti  na viongozi wa Halmashauri kuu ya tawi ya Chama hicho  katika matawi ya Raha leo...

Like
293
0
Tuesday, 10 February 2015
UN: MAZUNGUMZO JUU YA MGOGORO WA YEMEN KUANZA LEO
Global News

UMOJA WA MATAIFA umesema mazungumzo yanayolenga kuutatua mzozo wa kisiasa nchini Yemen yanatarajiwa kurejea leo na yatasimamiwa na mjumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Yemen Jamal Benomar. Taarifa kutoka umoja huo imesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon amepokea vyema tangazo kuwa mshauri wake maalum kuhusu Yemen Benomar atayasimamia mazungumzo hayo na kuzitaka pande zinazopigana nchini humo kurejea katika meza ya mazungumzo kwa nia njema na kuwa na nia ya kuafikiana. Yemen imekumbwa na mzozo tangu Rais...

Like
284
0
Monday, 09 February 2015
UKRAINE: MATAIFA YAOMBA KUFANYIKA MKUTANO WA KILELE
Global News

VIONGOZI wa Ukraine, Ujerumani na Ufaransa wanashinikiza kuwepo kwa mkutano wa kilele na Rais wa Urusi Vladimir Putin siku ya Jumatano wiki hii katika juhudi za hivi karibuni  za kuutafutia ufumbuzi mzozo wa mashariki mwa Ukraine. Hata hivyo Rais Putin ameonya kuwa mkutano huo unaotarajiwa kufanyika mjini Minsk, utafanyika tu iwapo viongozi hao watasikilizana kuhusu masuala kadhaa kabla ya Jumatano. Hii leo maafisa wa wizara ya mambo ya nje wa nchi hizo nne watafanya mazungumzo kwa ajili ya maandalizi ya...

Like
258
0
Monday, 09 February 2015
APC WAKOSOA KUAKHIRISHWA UCHAGUZI NIGERIA
Global News

UPINZANI  nchini Nigeria umekosoa hatua ya kuahirishwa kwa uchaguzi hadi mwishoni mwa Mwezi March. Chama kikuu cha upinzani cha APC kimesema hatua hiyo ni kikwazo kikubwa kwa Demokrasia nchini humo. Na kwamba Jeshi la Nigeria limelazimisha kuahirishwa kwa Uchaguzi ili liweze kumsaidia Rais wa nchi hiyo, Goodluck Jonathan kwenye Kampeni zake. Uchaguzi mkuu nchini humo ulipangwa kufanyika jumamosi ijayo lakini Tume ya Uchaguzi imesema Mashambulizi ya Boko Haram kwa kiasi kikubwa yanahatarisha uwepo wa zoezi la uchaguzi ,Usalama wa Wapigakura,...

Like
246
0
Monday, 09 February 2015
20 WAFARIKI, LIGI KUU YASIMAMISHWA MISRI
Global News

MISRI  imesimamisha kwa muda usiojulikana ligi kuu ya nchi hiyo baada ya watu zaidi ya  20 kufariki dunia. Kati ya waliofariki wengi wao ni Mashabiki wa timu ya Zamalek ambao walifariki kutokana na msongamano wakati Polisi walipowafyatulia mabomu ya machozi baadhi ya mashabiki waliokuwa wakijaribu kuingia kwa nguvu ndani ya uwanja wakati timu hiyo ilipokuwa ikipambana na timu ya ENPPI. (INI-P) Taarifa ya Wizara ya mambo ya ndani ya Misri inasema kuwa Mashabiki wa Zamalek walikuwa wanataka kuingia uwanjani kwa...

Like
567
0
Monday, 09 February 2015
LEO NI SIKU YA KIMATAIFA YA KUPINGA UKEKETAJI
Global News

LEO ni siku ya kimataifa ya kupinga ukeketaji. Umoja wa Mataifa ulianzisha siku hiyo kuhimiza jamii zinazowakeketa wanawake na wasichana kuacha mila hiyo ambayo inaleta athari kubwa za kiafya na kisaikolojia. Takwimu za Umoja wa Mataifa zinaonyesha kwamba duniani kote wapo wasichana na wanawake milioni 140 waliokeketwa. Umoja wa Mataifa unaonya kuwa idadi ya wataalamu wa afya wanaowakeketa wasichana inaongezeka, suala linalorudisha nyuma juhudi za kuitokomeza mila hiyo.  ...

Like
334
0
Friday, 06 February 2015