Mahakama Kuu nchini Kenya imesimamisha kwa muda matumizi ya baadhi ya vipengee vya Sheria ya usalama yenye utata iliopitishwa na Bunge na kuidhinishwa na Rais UHURU KENYATTA. Wanasiasa wa upinzani wamewasilisha kesi Mahakamani kupinga uhalali wa Sheria hiyo Kikatiba, huku wakisema inahujumu haki ya raia wa...
Askari wanaolinda Pwani ya Italia wamejaribu kuwasaidia watu waliokwama ndani ya Meli ya Kibiashara, iliyotelekezwa katika Pwani ya Kusini Mashariki mwa nchi hiyo. Meli hiyo ina zaidi ya wahamiaji haramu wapatao mia nne. Taarifa zinasema hakuna mhudumu wala nahodha kwenye meli hiyo. ...
Utafiti mpya umeeleza kuwa aina nyingi za Ugonjwa wa Saratani ni matokeo ya bahati mbaya, kuliko malezo ya Vinasaba, Mazingira na Mtindo wa maisha. Watafiti nchini Marekani wamechunguza aina 31 za Saratani na kugundua kwamba Theluthi Mbili zimesababishwa na mgawanyiko holela wa Seli. Taarifa zaidi zimefafanua kuwa kwa mgawanyiko wa kila seli kuna hatari ya mabadiliko yanayoweza kusababisha...
MWAKA MPYA wa 2015 umepokewa kwa kishindo katika maeneo mbali mbali duniani na barani Afrika. Nchini Nigeria kumekuwa shamra shamra ambapo kwa mara ya kwanza mafataki yalirushwa katika eneo la kaskazini mwa nchi hiyo lenye waislamu wengi. Shamra shamra hizo zimefanyika katika kituo cha michezo katika mji wa Kano ambapo waliohudhuria ni wale waliopata mwaliko pekee....
SHEREHE ZA KUUPOKEA mwaka mpya 2015 zimegeuka kuwa majonzi baada ya watu35 kufa kwenye taharuki ya kukanyagana kwenye msongamano wakati wakiiupokea mwaka mpya. Maafa hayo yametokea katika mji Shanghai ambapo maelfu ya watu walikuwa wamekusanyika ili kuupokea mwaka mpya. Chanzo cha taharuki hiyo bado haijafamika lakini vyombo vya habari vya nchi hiyo vimenukuliwa vikisema imetokana na maelfu ya watu kuzuiwa kugombea fedha bandia zilizotupwa eneo hilo kutoka katika jengo...
SHIRIKA LA AFYA Duniani -WHO limesema idadi ya vifo vilivyotokana na mripuko wa ugonjwa wa maradhi ya Ebola Afrika magharibi imeongezeka na kufikia 7,842 kati ya kesi 20,081 zilizorekodiwa. Idadi ya mwisho ya vifo ilikuwa ni 7,693 na kesi 19,695 taarifa za Ebola zilizotolewa Desember mwaka huu. Takriban vifo na kesi zote za ugonjwa wa wa maradhi ya Ebola zimerekodiwa katika nchi tatu za Afrika Magharibi ambazo zimeathiriwa zaidi na mripuko huo yaani Sierra Leone, Liberia na Guinea....
WAPIGANAJI wanaodhaniwa kuwa ni Boko Haram wamevamia kijiji Kaskazini Mashariki mwa Nigeria na kuua watu takriban 15. Shambulizi hilo limetokea kijiji cha Kautikari katika jimbo la Borno, pale washukiwa wa Boko Haram walipowasili kijijini humo kwa magari yenye silaha, wakilenga Askari wa Ulinzi wa Jadi wa mji huo. Kijiji hicho kipo karibu na Chibok mahali ambapo kundi la Boko Haram, limewatekanyara Wasichana wa shule zaidi ya 200 mwezi Aprili mwaka...
Ndege ya Kivita ya Marekani imekihujumu kituo cha Wanamgambo wa Itikadi kali wa Al Shabab nchini Somalia. Kwa mujibu wa Wizara ya Ulinzi ya Marekani mjini Washington, hujuma hizo zimelengwa dhidi ya kiongozi mmoja wa vuguvugu hilo la itikadi kali kusini mwa...
WAJUMBE kutoka nchini za za Kiarabu katika Umoja wa Mataifa wameunga mkono pendekezo la Palastina kuhimiza makubaliano ya Amani pamoja na Israel mnamo muda wa mwaka mmoja unaokuja na kumaliza kukaliwa ardhi za Wapalastina na Israel hadi ifikapo mwaka 2017, licha ya upinzani wa Israel na Marekani. Taarifa zaidi zimeeleza kuwa bado haijafahamika ni lini haswa mswaada wa azimio hilo utapigiwa kura katika Baraza la...
OPERESHENI ya kuwaokoa watu waliopo ndani ya Feri iliyowaka moto kwenye Bahari ya Adriatiki zinaendelea. Watu 10 wamekufa katika ajali hiyo na wengine kadhaa wanahofiwa kupotea. Feri hiyo ilikuwa na abiria 478 pamoja na wafanyakazi huku Watu 41 hawajulikani walipo na maafisa wa Italia na Ugiriki wanajaribu kuthibitisha jumla ya watu waliokuwemo...
MABALOZI wa Mataifa ya Kiarabu wameidhinisha pendekezo la Palestina kuhusu marekebisho ya azimio la Umoja wa Mataifa la kutaka Israel kuacha kuikalia kwa mabavu Palestina katika kipindi cha miaka mitatu. Pendekezo hilo limepingwa na Israel pamoja na Marekani. Marekani imesisitiza kwamba lazima pawe na suluhisho la mazungumzo katika mzozo wa Israel na...