Global News

Chama cha Trump, Republicans chabanwa mbavu katika uchaguzi
Global News

Chama cha Rais Donald Trump, Republicans kinaelekea kupoteza wingi katika bunge la Congress hali ambayo iatafanya urais wa Trump kupitia katika wakati mgumu zaidi. Hata hivyo, chama cha Republicans kinatarajiwa kuendelea kuwa na wingi katika Magavana na viti vya bunge la Seneti. Kwenye uchaguzi wa bunge la Congress, mpaka sasa majimbo 383 yametangaza matokeo. Democrats wanaongoza kwa viti 200 huku Republicans wakifuatia na viti 183. Bado kuna majimbo ya uchaguzi 52 hayajatangaza matokeo na Democrats wanatarajia kushinda zaidi. Katika uchaguzi...

Like
506
0
Wednesday, 07 November 2018
Nchi nane kulegezewa masharti ya vikwazo dhidi ya Iran
Global News

Marekani imesema italegeza masharti ya vikwazo dhidi ya Iran kwa nchi nane huku waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu akiisifu hatua ya Marekani na kulitaja tukio hilo kuwa la kihistoria. Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo ameziorodhesha China, India, Italia, Ugiriki, Japan, Korea Kusini, Taiwan na Uturuki kuwa nchi ambazo zitapewa ahueni ya muda ya kuagiza mafuta ya Iran na kuepuka kuadhibiwa kwa kukiuka vikwazo vilivyowekewa nchi hiyo. Pompeo amesema Marekani haitachoka kuishinikiza Iran. Maafisa wa Iran...

Like
499
0
Tuesday, 06 November 2018
Kiongozi wa upinzani nchini Bahrain ahukumiwa kifungo cha maisha jela
Global News

Kiongozi wa upinzani nchini Bahrain Sheikh Ali Salman amehukumiwa kifungo cha maisha jela baada ya mahakama ya rufaa kumpata na hatia ya kupeleleza kwa niaba ya Qatar. Hukumu hiyo inakuja miezi michache baada ya mahakama ya juu nchini Bahrain kumuondolea mashtaka Salman kwa kushirikiana na taifa hasimu. Bahrain ilikata uhusiano wake na Qatar mwaka 2017. Shirika la haki za binadamu la Amnesty limetaja uamuzi huo kama ukiukaji wa haki wakati huu Bahrain inaendelea kuwazima wakosoaji. Ali Salman ambaye aliongoza vuguvugu...

Like
535
0
Monday, 05 November 2018
Kitendawili cha dada wawili wa Saudia waliopatikana wamefariki New York
Global News

Polisi mjini New York inachunguza vifo vya dada wawili kutoka Saudi Arabia ambao walipatikana wamefariki wakiwa wamefungwa pamoja katika mto Hudson wiki iliyopita. Tala Farea, 16, na Rotana Farea, 22, walipatikana wakiwa wameelekeana uso kwa uso huku wakiwa wamevalia nguo zao na hapakua na ishara zozote za kuonyesha kuwa walipata usumbufu. Wachunguzi wanasema ni mapema kubaini ikiwa uhalifu wowote ulifanyika au vifo vyao vilitokana na tukio la kujitoa uhai. Polisi wanasema wasichana hao walikua wametoa maombi ya kutaka kupewa hifadhi...

Like
874
0
Thursday, 01 November 2018
Mshukiwa wa vifurushi vya mabomu akamatwa
Global News

  Mtu anayeshukiwa kutuma kwa njia ya posta, vifurushi vya mabomu kwa wakosoaji wakubwa wa Rais Donald Trump wa Marekani amekamatwa jimboni Florida Ijumaa. Trump amesema ingawa mtu huyo ni mfuasi wake, hawezi kuwajibishwa. Mtu huyo, Cesar Sayoc mwenye umri wa miaka 56, ana rekodi ya vitendo vya kihalifu, vikiwemo kutishia kuripua mabomu. Alikamatwa na maafisa wa usalama wa serikali kuu ya Marekani, nje ya kiwanda cha vipuri vya magari karibu na mji wa Miami. Helikopta zilikuwa zikizunguka juu ya...

Like
685
0
Saturday, 27 October 2018
Mchumba wa mwandishi Khashoggi akataa mwaliko wa Donald Trump
Global News

Mchumba wa mwanahabari wa Saudia aliyeuawa Jamal Khashoggi anasema amesusia mwaliko wa rais wa Marekani Donald Trump katika Ikulu ya White House kwa madai kiongozi huyo wa haijaonesha nia ya kutaka kujua ukweli kuhusu mauaji hayo ya kikatili. Hatice Cengiz amekiambia kituo kimoja cha Televisheni nchini Uturuki kwamba mwaliko huo unalenga kubadili maoni ya Wamarekani Khashoggi aliuawa ndani ya ubalozi mdogo wa Saudi Arabia mjini Istanbul wiki tatu zilizopita. Riyadh imekanusha madai ya kuhusishwa kwa familia ya kifalme katika mauaji...

Like
1860
0
Saturday, 27 October 2018
Utafiti ; Wanaume warefu kuwa na Saratani
Global News

Utafiti mpya wa kiafya umebaini kuwa watu warefu zaidi wapo katika hatari ya kuwa na ugonjwa wa Saratani. Mwandishi wa ripoti ya utafiti huu Dr Leonard Nunney anasema watu walio katika mazingira ya kupata ugonjwa wa saratani iwapo tu atakuwa na ongezeko la urefu wa kawaida kwa kuanzia sentimita kumi,basi hapo ni jambo la kujiuliza mara mbili. “Iwapo wastani wa wanawake 50 kati ya 500 watapata saratani, wastani huo unabadilika ifikapo kwa wanawake 60 kwa 500 warefu kufikia kimo cha...

Like
1417
0
Thursday, 25 October 2018
rais wa kwanza mwanamke Ethiopia
Global News

Wabunge nchini Ethiopia wamemchagua Sahle-Work Zewde kuwa rais wa kwanza mwanamke Ethiopia. Bi Sahle-Work ni mwanadiplomasia mwenye uzoefu ambaye sasa amekuwa kiongozi wa kipekee mkuu mwanamke barani Afrika. Kuchaguliwa kwake katika wadhifa huo kunajiri wiki moja baada waziri mkuu Abiy Ahmed kuliteua baraza la mawaziri ambapo nyadhifa nusu katika baraza hilo zimewaangukia wanawake. Katika hotuba yake ya kukubali wadhifa huo, rais Sahle-Work amezungumza kuhusu umuhimu wa kudumisha amani, vyombo vya habari nchini vinaeleza. Amechaguliwa baada ya...

Like
957
0
Thursday, 25 October 2018
Mizizi na asili ya nguli wa muziki duniani na visiwa vya Zanzibar
Global News

Filamu mpya imeingia sokoni kuhusu bendi ya mziki ya Queen kutoka Uingereza, na macho yameelekezwa tena juu ya maisha ya muimbaji kinara wa bendi hiyo Freddie Mercury. Ushawishi wake jukwaani, mavazi, mizizi yake na kifo chake kutoana na maradhi yanayohusiana na ugonjwa wa ukimwi akiwa na umri wa miaka 45 mwaka 1991 ni kumbukumbu tosha za mwanamuziki huyo wa miondoko ya rock kuanzia miaka ya sabini na themanini. Kile ambacho wengi hawakifahamu na hakizungumziwi sana katika filamu ni kuwa alizaliwa...

Like
1118
0
Wednesday, 24 October 2018
Watoto wafanyiwa upasuaji wa uti wa mgongo wakiwa tumboni mwa mama zao Uingereza
Global News

Watoto wawili ambao bado hawajazaliwa wamefanyiwa upasuaji wa uti wa mgongo wiki chake kabla ya kuzaliwa kwao. Upasuaji huo ambao ni wa kwanza wa aina hiyo nchini Uingereza ulifanywa na kundi la madaktari 30 kati chuo kimoja jijini London. Watoto hao walikuwa na tatizo lilalojulikana kama spinal bifida, ambapo uti wa mgongo hukosa kukua vile inavyotakikana. Mara nyingi hali hiyo hutibiwa baada ya mtoto kuzaliwa lakini ikiwa itatibiwa mapema hali ya afya ya mtoto huwa bora zaidi. Wakati wa upasuaji...

Like
978
0
Wednesday, 24 October 2018
Trump asema harakati za Saudia kuminya ukweli kuwa mbaya katika historia
Global News

Rais wa Marekani Donald Trump ameziita harakati za Suadi Arabia kuminya ukweli juu ya mauaji ya mwandishi Jamal Khashoggi kuwa harakati mbaya zaidi kwenye historia. Trump pia amesema yeyote aliyesuka mpango huo anatakiwa kuwa katika “matatizo makubwa.” Marekani wamekuwa katika shinikizo la kuwabana washirika wao Saudia juu ya mkasa huo uliotokea kwenye ofisi za ubalozi mdogo wa Saudia jijini,Instanbul Uturuki. Akiongea na wanahabari katika Ikulu ya White House, Trump amesema: “Walikuwa na wazo duni sana, na wakalitekeleza...

Like
635
0
Wednesday, 24 October 2018