Global News

Sergei Skripal: Wanadiplomasia wa Urusi wazidi kufurushwa katika nchi mbalimbali
Global News

Australia imekuwa nchi ya karibuni kufukuza wanadiplomasia wa Urusi kutoka nchini kwake kutokana na shambulio la jasusi wa zamani wa urusi nchini Uingereza Sergei Skripal na binti yake ambao wako katika hali mbaya kiafya. Novichok: Sumu iliyotumiwa kumshambulia jasusi wa Urusi Waziri mkuu Malcolm Turnbull amesema uamuzi huo unatokana na shambulio hatari la kutumia kemikali za neva zinazotengezwa na Urusi na zilitomiwa mara mwisho vita vya pili vya dunia.Idadi ya wanadiplomasia wa Urusi wanaofukuzwa inazidi kuongezeka, na hii ndio idadi...

Like
391
0
Tuesday, 27 March 2018
Rangi ya ngozi yako yaweza kukupa uraia nchini Liberia
Global News

Tony Hage ameishi Liberia kwa zaidi ya miaka hamsini. Na ndipo mahali alipo kutana na mke wake kisha kuanzisha biashara yake yenye mafanikio. Aliendelea kuishi Liberia katika kipindi ambacho raia wengi wa nchi hiyo wali kimbia ili kuepuka machafuko akilenga kuiona nchi anayoipenda ikipata mafanikio. Mpaka sasa bwana Hage si raia wa Liberia, amezuiwa kupata uraia wa kudumu wa nchi hiyo kwa sababu ya rangi ya ngozi yake na asili ya familia yake kutoka huko Lebanon. ‘Tutakuwa watumwa’ Nchi ya...

Like
583
0
Monday, 26 March 2018
Miguna atarajiwa kuwasili Nairobi Jumatatu
Global News

Wakili na mwanaharakati mzaliwa wa Kenya ambaye alilazimishwa kwenda uhamishoni nchini Canada mwezi Februari mwaka huu alitarajiwa kurejea mjini Nairobi siku ya Jumatatu Machi 26, 2018 huku kukiwa na wasiwasi kwamba huenda asiruhusiwe na serikali ya Kenya kuingia nchini. Katika taarifa aliyoituma kwa idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya Amerika siku ya Jumapili akiwa mjini London Uingereza, Miguna Miguna alisema kuwa ataingia Kenya hata bila pasipoti au viza kumruhusu kufanya hivyo. “Ndege yetu itatua Nairobi Jumatatu saa nane na dakika...

Like
339
0
Monday, 26 March 2018
Watu 37 wafariki katika mkasa wa moto jumba la Kemerovo, Urusi
Global News

Watu 37 wamethibitishwa kufariki baada ya moto kuzuka katika jumba moja kubwa la kibiashara katika mji maarufu kwa uchimbaji wa mkaa wa mawe wa Kemerovo, eneo la Siberia nchini urusi. Watu zaidi ya 64 hawajulikani walipo, wakiwemo watoto 41. Baadhi ya maeneo ya jumba hilo kubwa yanadaiwa kuwa kwenye hatari ya kuporomoka. Moto huo ulianza katika ghorofa ya juu katika jumba Winter Cherry. Inadaiwa wengi wa waliofariki walikuwa kwenye kumbi za sinema. Video zilizopakiwa mitandao ya kijamii zinawaonesha watu wakiruka...

Like
394
0
Monday, 26 March 2018
Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Jacob Zuma kuburuzwa mahakamani
Global News

  Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Jacob Zuma kuburuzwa mahakamani mwezi Aprili kwa makosa 16 yakiwemo ya kutumia vibaya ofisi wakati akiwa madarakani na ufisadi. Duru za habari nchini Afrika Kusini kusini likiwemo gazeti la News24 limeeleza kuwa Zuma atafikishwa kizimbani katika Mahakama Kuu mjini Durban tarehe 6 Aprili 2018 kwa makosa 16. Kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa na msemaji wa bodi ya kuzuia na kupambana na rushwa nchini humo, Brigedia Hangwani Mulaudzi amesema kuwa mwishoni mwa wiki hii...

Like
331
0
Monday, 26 March 2018
Soko la Facebook latetereka kwa kupoteza uaminifu
Global News

Pamoja na mmiliki wa mtandao wa kijamii wa Facebook Mark Zuckerbag kuomba msamaha kutokana na kupoteza uaminifu kitu kilichowakera watu zaidi ya milioni 50 duniani, soko lake la hisa limeonyesha kutetereka. Kwa mujibu wa mtandao wa kibiashara MoneyWatch soko la hisa za mtandao huo zilianguka kwa asilimia saba. Thamani ya hisa ilishuka kutoka Dola 176.80 siku ya Jumatatu hadi Dola 159.30 siku ya Ijumaa jioni. Siku hiyo hisa za mtandao wa Facebook ziliuzwa kwa $38 kila moja na kuufanya mtandao...

Like
542
0
Sunday, 25 March 2018
Papa Francis awataka vijana duniani kuinua sauti zao
Global News

Kiongozi mkuu wa kanisa la Katoliki, Papa Francis, Jumapili aliwashauri vijana duniani kuendelea kutetea masuala wanayoyaamini, na kutokubali sauti zao kuzimwa. Akizungumza wakati wa ibada ya Jumapili ya matawi, Palm Sunday, iliyofanyika kwenye ukumbi wa St Peters Square mjini Vatican, Papa Francis aliwataka vijana kuendelea kupaza sauti zao hadi zitakaposikika. Kauli yake imejiri siku moja baada ya maandamano makubwa kufanyika ulimwenguni kote siku ya Jumamosi kuishinikiza Marekani kuunda sheria zinazodhibiti umiliki wa bunduki hatari. Hata...

Like
379
0
Sunday, 25 March 2018
Korea Kusini na Kaskazini kufanya mkutano wiki ijayo
Global News

Korea Kusini na Korea Kaskazini ambazo zimekuwa mahasimu kwa muda mrefu, zimekubaliana kufanya mkutano wa ngazi ya juu wiki ijayo ili kufanya maandalizi ya mkutano wa Aprili kati ya Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un na Rais wa Korea Kusini Moon Jae-in. Korea Kusini imesema mkutano huo unalenga kuimarisha uhusiano na kusuluhisha mkwamo kuhusu mpango wa nyuklia wa Korea Kaskazini. Waziri wa Muungano Cho Myoung-gyon ataongoza ujumbe wa Korea kusini katika mkutano huo ambao umepangwa kufanyika tarehe 29 Machi...

Like
480
0
Saturday, 24 March 2018
China yaionya Marekani wakati mzozo wa kibiashara ukifukuta
Global News

China imeionya Marekani kuwa iko tayari na ina uwezo wa kulinda maslahi yake, wakati ambapo mgogoro wa kibiashara ukifukuta kati ya nchi hizo mbili. Shirika la habari la China-Xinhua, limeripoti kuwa Naibu Waziri Mkuu wa China Liu He amempigia simu Waziri wa Fedha wa Marekani, Steven Mnuchin na kufikisha ujumbe huo. Liu pia amesema uchunguzi wa miezi saba uliofanywa na Marekani kuhusu shughuli za kibiashara za China, unakiuka sheria za kimataifa za biashara. Mazungumzo hayo ya simu kati ya Liu...

Like
362
0
Saturday, 24 March 2018
Trump amteua Bolton kuwa mshauri wake mpya wa usalama
Global News

Rais wa Marekani Donald Trump amemuomdoa Mshauri wake wa usalama wa taifa H.R McMaster na kumteua katika nafasi hiyo John Bolton mtu mwenye msimamo mkali na aliyewahi kuwa balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa. Trump kama kawaida alitumia ukurasa wake wa Twitter kutoa tangazo hilo la karibuni la mabadiliko ya watumishi, hatua ya mbayo inauweka katika mashaka makubwa mustakabali wa makubaliano ya kihistoria kuhusu mpango wa nyukilia wa Iran.Hii ni mara ya tatu kwa Trump kubadilisha mshauri wake wa...

Like
451
0
Friday, 23 March 2018
Rais Donald Trump aonyesha nia ya kutoa ushahidi mbele ya mwendesha mashitaka maalum
Global News

Rais wa Marekani Donald Trump ameonyesha nia ya kutoa ushahidi mbele ya mwendesha mashitaka maalum anayechunguza uingiliaji kati wa Russia katika uchaguzi mkuu wa Marekani wa mwaka 2016 na mambo mengine. Ningependa Trump alijibu alipohojuiwa na waandishi wa habari kutaka kujua kama ana nia ya kuhojiwa na wachunguzi. Rais alitoa jibu hilo wakati akiondoka katika chumba cha kidiplomasia cha White house mara tu baada ya kusaini nyaraka ya kuelekeza utawala wake kuchukua hatua za kibiashara dhidi ya China. Majibu ya...

Like
368
0
Friday, 23 March 2018