Msichana mwenye umri wa miaka saba Leia Armitage amekuwa akiishi katika maisha ya ukimya kutokana na kutosikia katika kipindi cha miaka miwili ya mwanzo ya masha yake , lakini upasuaji wa hivi karibuni wa ubongo na tiba vimeweza kubadili maisha yake na sasa anaweza kusikia sauti zake na hatimae anaweza kusikia sauti za wazazi wake na kuwambia kuwa anawapenda. “Tuliamboiwa kuwa unaweza kuweka bomu nyuma yake na asingeliweza kabiza kusikia sauti ya mlipuko wake ,” amesema baba yake Leia ,...
Korea Kaskazini imesema kuwa imefanyia majaribio silaha yenye kombora kali , ikiwa ni mara ya kwanza tangu mazungumzo kati ya rais Donald Trump na Kim Jong un kugonga mwamba. Vyombo vya habari vya serikali vilitoa maelezo , lakini wachanganuzi wanansema kuwa jaribio hilo halionekani kuwa lile la kombora la masafa marefu ambalo ni tishio kwa Marekani. Jaribio jingine kama hilo mnamo mwezi Novemba lilionekana kama hatua ya kuishinikiza Marekani kurudi katika meza ya mazungumzo. Kumekuwa na hatua chache zilizopigwa tangu...
Moto mkubwa umezuka katika kanisa kongwe la Notre-Dame mjini Paris Ufaransa ambalo ni moja ya makanisa maarufu na linalotembelewa na idadi kubwa ya watalii kutoka pande mbali mbali duniani kila mwaka. Vikosi vya zima moto vinaendelea kuzima moto huo katika kanisa hilo lililodumu kwa takriban miaka 850. Sehemu kubwa ya paa la majengo ya kanisa hilo yameteketezwa na mto huo huku moto katika minara miwili ya kengele umefanikiwa kuzimwa. Chanzo cha moto huo hakijajulikana, lakini maafisa maafisa wanauhusisha mkasa huo...
Mwanafunzi wa kike wa mwaka wa tatu katika Chuo Kikuu cha Pwani kilichoko Kaunti ya Kilifi nchini Kenya, jana alichomwa visu mara kadhaa na mwanafunzi mwenzake anayedaiwa kuwa alikuwa mpenzi wake. Mwanafunzi huyo aliyetajwa kwa jina la Naomi Chepkemboi, alichomwa visu mara kadhaa kifuani na alikimbizwa katika hospitali ya Kaunti ya Kilifi anakoendelea kupatiwa matibabu. Kwa mujibu wa Jeshi la polisi, mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kenyatta aliyetambulika kwa jina la Henry Kipkoech, ambaye alikuwa mpenzi wake anashikiliwa na jeshi...
Baraza la mpito la kijeshi nchini Sudan limewakamata waliokuwa maafisa wa serikali na kuahidi kutowatawanya waandamanaji. Msemaji mmoja pia ameuomba upinzani kumchagua waziri mkuu mpya na kuahidi kumuidhinisha watakayemchagua. Maandamano ya miezi kadhaa nchni Sudan yamechangia kutimuliwa kwa kiongozi wa muda mrefu nchini Sudan Omar al-Bashir Alhamisi wiki iliyopita Waandamanaji wameapa kusalia mitaani mpaka itakapoundwa serikali ya kiraia Raia wanaendelea kuandamana na wamekita kambi nje ya makao makuu ya wizara ya ulinzi katika mji mkuu...
Polisi nchini sudan imewaamuru maafisa wake kutowashambulia maelfu ya waandamanaji waliopiga kambi nje ya makao makuu wa jeshi mjini Khartoum tangu Ijumaa. Waandamanaji hao wanamtaka rais Omar al-Bashir ajiuzulu. Awali milio ya risasi ilisikika nje ya makao ya jeshi na ripoti zinasema kuwa maaskari wanaotoa ulinzi kwa waandamanaji wamepigwa risasi na maajenti wa serikali. Katika taarifa yake msemaji wa polisi aliandika”Tunatoa amri kwa vikosi vyote” visiingilie “maandamano ya amani aukuwashambulia wananchi”....
Maelfu ya waandamanaji wamekita kambi nje ya makao makuu ya jeshi nchini Sudan, wakimtaka rais Omar al-Bashir ajiuzulu. Inavyoonekana wanatarajia mapinduzi ya ndani ya nchi, wakiliomba jeshi kumtimua Bashir na kufungua njia ya kupatikana serikali ya mpito. Ni maandamano makubwa dhidi ya Bashir tangu kuzuka ghasia mnamo Desemba mwaka jana. Bashir amekataa kuondoka, akieleza kwamba wapinzani wake wanastahili kutafuta uongozi kupitia uchaguzi. Jeshi halijaingilia kati. Maafisa wa usalama wamefyetua gesi ya kutoa machozi kuwatimua wandamanaji nje...
Ripoti ya uchunguzi kuhusu kuanguka kwa ndege ya Ethiopia Airlines mwezi uliopita inasema kuwa ndege hiyo ilitaka kuangukia pua yake mara kadhaa kabla ya ajali hiyo. Marubani walifuata maagizo yaliopendekezwa na Boeing kabla ya ajali hiyo kulingana na ripoti ya kwanza ya ajali hiyo. ”Licha ya juhudi zao , marubani walishindwa kuidhibiti ndege hiyo” , alisema waziri wa uchukuzi Dagmawit Moges. Ndege hiyo aina ya ET302 ilianguka baada ya kupaa kutoka mji wa Adis Ababa , na hivyobasi kuwaua watu...
Uhuru Kenyatta amekuwa gumzo kuu katika mitandao ya kijamii nchini Kenya wakati akitarajiwa kulihotubia taifa leo. Kiongozi huyo mkuu nchini Kenya anatarajiwa kuizungumzia hali ya mambo nchini katika hotuba anayotarajiwa kuitoa bungeni leo mchana. Na hili linatarajiwa kufanyika wakati ufisadi, deni kubwa la taifa na suala la ukosefu wa ajira na mishahara yakizungumziwa pakubwa na wakenya ambao wametumia fursa kumshinikiza kiongozi huyo kuyazungumzia leo. Swali kuu ni je, Rais Uhuru Kenyatta atasema nini leo kipya katika hotuba yake ya...
Rais wa Algeria, Abdelaziz Bouteflika amejiuzulu wadhifa wake baada ya miaka 20 kufuatia wiki kadhaa za maandamano nchini mwake. Bouteflika amekuwa madarakani kama rais kwa muda wa miaka 20 , tayari alikuwa amefutilia mbali mpango wa kugombea muhula mwingine kutawala kutokana na kukuwa kwa upinzani. Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na Shirika la Habari la nchi hiyo, kiongozi huyo tayari aliondoa mipango yake ya kusaka awamu ya tano madarakani, wakati upinzani dhidi ya serikali yake ukiongezeka. Jeshi la Algeria ambalo...
Majambazi wamenyofoa na kutokomea na mashine ya kielektroniki ya kutolea pesa nchini Ireland ya Kaskazini. Majambazi hao walitumia tingatinga ambalo pia waliliiba katika kunyofoa ATM hiyo kutoka kwenye ukuta wa duka moja katika Kaunti ya Antrim. Tukio hilo limetokea saa tisa ya usiku wa Jumatatu. Polisi wamethibitisha kuwa jengo hilo limeharibiwa vibaya. Majambazi wamenyofoa na kutokomea na mashine ya kielektroniki ya kutolea pesa nchini Ireland ya Kaskazini. Majambazi hao walitumia tingatinga ambalo pia waliliiba katika kunyofoa ATM hiyo...