Global News

JARIBIO LA KOMBORA LA KOREA KUSINI LAFELI
Global News

KOREA Kaskazini imefanya jaribio lingine la makombora yake ya masafa marefu katika eneo la mashariki ya pwani yake lakini linaonekana kufeli. Wakizungumzia makombora hayo wanajeshi wa Korea Kaskazini wamesema kuwa haijulikani ni kombora gani limefeli na kwamba hiyo imejirudia baada ya makombora mengine yaliyojulikana kwa jina la ”Musudan” kufeli mnamo mwezi Aprili. Hata hivyo imeelezwa kutanda kwa wasiwasi katika eneo hilo baada ya Pyongyang kujaribu kombora la nne la Kinyukia mnamo mwezi Januari pamoja na makombora...

Like
394
0
Tuesday, 31 May 2016
HABRE AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MAISHA JELA
Global News

ALIYEKUWA rais wa Chad Hissene Habre amehukumiwa kifungo cha maisha jela baada ya kupatikana na hatia ya kuhusika kwenye uhalifu dhidi ya ubinadamu , ubakaji na utumwa wa ngono. Habre alihusika moja kwa moja katika uhalifu huo ambao ulifanyika wakati akiwa rais wa Chad. Waathiriwa waliokuwa ndani ya mahakama wakati wa kusomwa kwa hukumu hiyo mji Dakar nchini Senegal, wameshangilia wakati jaji alipomaliza kusoma...

Like
340
0
Monday, 30 May 2016
MUGABE ASISITIZA KUTOACHIA MADARAKA
Global News

RAIS wa Zimbabwe Robert Mugabe amesema kuwa yeye sio Mmarekani wala Muingereza wakati akiwahutubia karibu watu elfu 50,000, wafuasi wake kwenye mkutano uliofanyika kwenye mji mkuu Harare kwa heshima yake.   Mugabe mwenye umri wa miaka 92 amekana uwezekano wowote wa kuondoka madarakani na kuwashambulia viongozi hasimu ndani ya chama tawala cha ZANU-PAFU kwa kupanga kumrithi.   Amesema kuwa yeye anawahudumia watu wa Zimbabwe na kuwa ataondoka tu ikiwa watu wangetaka afanye...

Like
324
0
Thursday, 26 May 2016
HUKUMU YA KESI YA SHAMBULIO LA AL-SHABAB UGANDA
Global News

MAHAKAMA mjini Kampala leo inatarajiwa kutoa hukumu katika kesi ambapo wanaume 13 wameshtakiwa kuhusiana na mashambulio ya mabomu yaliyotekelezwa na al-Shabaab mwaka 2010. Watu zaidi ya 70 walifariki kwenye mashambulio hayo yaliyotekelezwa wakati watu wakitazama fainali ya Kombe la Dunia la mwaka 2010. Kesi hiyo imechukua miaka...

Like
296
0
Thursday, 26 May 2016
BRAZIL: MKANDA WA VIDEO WAMUUMBUA WAZIRI
Global News

WAZIRI wa mipango wa serikali mpya ya Brazil amewekwa pembeni baada ya kukutwa katika mkanda wa video akifanya njama ya kukwamisha uchunguzi mkubwa wa nchi hiyo unaohusu ufisadi. Katika rekodi ya kanda hizo, ambazo zimetolewa na gazeti moja nchini humo, waziri Romero Juca, ameonekana akisema kuwa kuondolewa madarakani kwa Rais Dilma Rousseff, kutazuia kuchunguzwa kwa kampuni ya serikali ambayo ni kubwa katika uzalishaji wa mafuta, Petrobras. Hata hivyo, waziri huyo amesema kauli yake hiyo imeeleweka vibaya na kwamba anaunga mkono uchunguzi...

Like
275
0
Tuesday, 24 May 2016
IRAQ YATANGAZA VITA KUKOMBOA FALLUJAH
Global News

WAZIRI Mkuu wa Iraq Haider al-Abadi ametangaza operesheni kubwa ya kijeshi ya kuukomboa mji wa Fallujah kutoka kwa wapiganaji wa Islamic State. Kundi hilo liliuteka mji huo miaka miwili iliyopita. Akiwa ameandamana na maafisa wakuu wa jeshi, Bwana al-Abadi ametoa tangazo hilo moja kwa moja kupitia televisheni na kusema bendera ya Iraq karibuni itapepea katika mji huo ambao upo takjriban kilomita 50 magharibi mwa mji wa...

Like
295
0
Monday, 23 May 2016
MUUNGANO WA VYAMA UPINZANI KENYA WATANGAZA KUENDELEA NA MAANDAMANO
Global News

MUUNGANO wa vyama vya upinzani nchini Kenya-CORD, umetangaza kuendelea na maandamano ya upinzani leo Jumatatu, kama ilivyopangwa ikiwa ni sehemu ya kampeni ya kutaka kutupiliwa mbali kwa tume ya uchaguzi nchini humo, IEBC, kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka ujao. Maandamano kama hayo yaliyofanyika Juma liliopita, yaliambatana na ghasia ambapo polisi walishutumiwa kwa vitendo vya...

Like
246
0
Monday, 23 May 2016
WAJUMBE 5000 KUKUTANA COPENHAGEN KUHUDHURIA MKUTANO WA MASUALA YA WANAWAKE
Global News

ZAIDI  ya wajumbe 5,000 kutoka nchi 150 wamewasili mjini Copenhagen, Denmark kuhudhuria mkutano wa wiki nzima kuhusu masuala ya wanawake. Mkutano huo unoatajwa kuwa mkubwa zaidi kuwahi kuandaliwa katika kipindi cha muongo mmoja kujadili masuala ya wanawake kama afya, haki na maslahi ya wanawake na wasichana umeandaliwa na shirika la kimataifa la kutetea maslahi ya wanawake la Wellbeing. Mkutano huo unaanza leo hadi Alhamisi wiki hii na  Miongoni mwa ajenda za mkutano huo ni kuhusu jinsi ya kupunguza vifo vya...

Like
319
0
Monday, 16 May 2016
NCHI ZENYE NGUVU KUKUTANA VIENNA KUIJADILI IS
Global News

NCHI zenye nguvu duniani zinakutana mjini Vienna, Austria leo kujadili kupanuka kwa shughhuli za kundi la wanamgambo wenye itikadi kali la Dola la Kiislamu IS nchini Libya.   Mkutano huo unaongozwa na waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry na mwenzake wa Italia Paoli Gentiloni.   Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani John Kiry amesema mkutano huo wa Vienna utajadili uungwaji mkono wa serikali ya Umoja wa kitaifa ya Libya na jumuiya ya kimataifa kwa...

Like
270
0
Monday, 16 May 2016
JOHN KERRY AFANYA MAZUNGUZUMZO NA MFALME WA SAUDI ARABIA
Global News

WAZIRI wa Mambo ya nje wa Marekani John Kerry amefanya mazungumzo na Mfalme Salman wa Saudi Arabia kuhusu mizozo ya Syria, Libya na Yemen, kabla ya mikutano ya kimataifa inayopangwa kuandaliwa wiki ijayo barani Ulaya kuhusu mizozo hiyo. Ziara ya Kerry, ambaye pia amefanya mazungumzo na mwanamrithi wa ufalme na naibu mwanamrithi wa ufalme na waziri wa mambo ya nje, inakuja katika wakati muhimu wa kuimarisha juhudi za kudhibiti mapigano na kuhimiza mazungumzo ya kisiasa katika nchi zote tatu ambazo...

Like
311
0
Monday, 16 May 2016
31 WAUAWA KWA BOMU YEMEN
Global News

Watu 31 wameuawa kwa bomu la kujitoa muhanga nchini Yemen,shambulizi linalodaiwa kutekelezwa na wanamgambo wa Islamic state. Polisi wamethibitisha kutoka kwa shambulizi hilo katika ngome iliyoko kusini mwa nchi hiyo ya Mukalla. Vyanzo kutoka idara ya afya vinasema kuwa zaidi ya watu sita wamejeruhiwa katika shambulizi hilo. Maafisa wanasema kiongozi mmoja wa ulinzi na usalama alilengwa katika shambulizi la pili,ambapo aliponea chupuchupu, lakini walinzi wake wapatao sita waliuawa. Mashambulizi haya yanakuja pakiwa panafanyika mzungumzo ya...

Like
279
0
Monday, 16 May 2016