UMOJA wa Ulaya na Uturuki wamekubaliana, kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya Habari juu ya namna ya kuwachagua wakimbizi wa Syria watakaohamishiwa katika nchi za Umoja huo. Gazeti la “Bild” limenukuu waraka wa siri unaoonyesha kwamba wasyria tu ndio watakaoruhusiwa kwanza kuingia katika nchi za Umoja wa ulaya ikiwa wameomba kinga kabla ya novemba 29 nchini Uturuki. Aidha taarifa zimeeleza kwamba Makubaliano ya awali yanawataka wakimbizi kutojichagulia wenyewe nchi wanayotaka wapelekwe na badala yake kukubali kupangiwa nchi za...
RAIS wa zamani wa Burundi Kanali Jean-Baptiste Bagaza amefariki dunia wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya Sainte Elisabeth mjini Brussels nchini Ubelgiji. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mshauri wa rais wa Burundi Willy Nyamitwe kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter imeeleza kuwa Kanali Bagaza aliingia madarakani Novemba 1976 kupitia mapinduzi ya kijeshi. Hata hivyo baadaye aliondolewa madarakani kupitia mapinduzi mengine yaliyoongozwa na binamu yake Meja Pierre Buyoya mwezi Septemba...
IDADI ya watu waliofariki baada ya jumba la ghorofa sita kuporomoka siku ya Ijumaa imeongezeka baada ya miili zaidi kupatikana kwenye vifusi. Maafisa wa uokoaji wamepata miili mitatu zaidi na kufikisha miili 26, ambayo ni idadi ya watu waliofariki kutokana na mkasa huo uliotokea baada ya mvua kubwa kunyesha. Hata hivyo Shirika la msalaba mwekundu nchini humo limeeleza kuwa Watu 93 bado hawajulikani...
MAAFISA wanne wa polisi nchini China wamesema kuwa watashirikiana na wenzao wa Itali kupiga doria mjini Rome na Milan katika jaribio la wiki mbili zijazo. Waziri wa mambo ya nje wa Italia Angelino Alfano amesema Maafisa hao wanaozungumza Kiitaliano wanatumwa nchini Italia kwa lengo la kuwafanya watalii wa China kujisikia huru na salama wakati huu wa msimu wa juu wa utalii. Takribani watalii milioni 3 kutoka nchini China hutembelea nchi ya Italia kila mwaka....
MJUMBE wa Umoja wa Mataifa Staffan De Mistura anatarajiwa kukutana na waziri wa masuala ya kigeni nchini Urusi kujadiliana kuhusu juhudi za kunusuru kuvunjika kwa mkataba wa amani nchin Syria. De Mistura anataka Urusi na Marekani ambazo zinaunga mkono makundi pinzani nchini humo kushirikiana ili kurejesha makubaliano waliopatana mwezi Februari. Hata hivyo Washington imeilaumu Moscow kwa kushindwa kuwazuia wanajeshi wa Syria waliopo mjini...
TIMU ya kimataifa ya wanasayansi imekamilisha utafiti mkubwa zaidi kuwahi kutokea wa maumbile ya saratani ya matiti, ambayo wamesema inawapa karibu picha kamili ya nini husababisha ugonjwa huo. Wanasayansi hao wanajaribu kutizama mfuatano wa jinomu kamili wa kesi zaidi ya mia tano za saratani ya matiti. Utafiti huo unaoongozwa na taasisi ya Cambridge umeweza kugundua aina tano mpya za visababishi vya ugonjwa huo ambavyo vikibadilika husababisha uvimbe katika sehemu husika ya mwili wa...
MTOTO mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu amepatikana akiwa hai kwenye vifusi vya jengo lililoporomoka siku ya Ijumaa jijini Nairobi nchini Kenya. Jengo hilo la ghorofa sita liliporomoka katika mtaa wa Huruma baada ya mvua kubwa kunyesha. Akizungumzia hali ya afya ya mtoto huyo, Kamanda wa kitengo cha taifa cha kudhibiti majanga Pius Maasai amesema kuwa hali ya mtoto huyo inaendelea kuimalika tangu alipofikishwa hospitalini...
Maelfu ya waombolezaji walijitokeza kuadhimisha misa ya wafu kwa heshima ya mwanamuziki nyota wa muziki wa Soukus na Rhumba raia wa Jamhuri ya Congo Papa Wemba. Waomboloezaji walipiga foleni ilikupata fursa ya kutoa heshima zao za mwisho kwa msanii huyo nguli aliyeaga dunia juma lililopita alipokuwa akiwatumbuiza mashabiki wake huko Abidjan Ivory Coast. Mwili wake umewekwa katika majengo ya bunge mjini Kinshasa. Serikali imetangaza siku tatu za maombolezi kuanzia leo hadi jumatano atakapozikwa. Tayari amepewa tuzo kwa mchango wake. Msanii...
IMEELEZWA kuwa Wanajeshi wa Uingereza wamewasili nchini Somalia kusaidia katika juhudi za kukabiliana na wapiganaji wa Kiislamu wa Al-Shabaab. Wanajeshi 10 waliowasili nchini Somalia ni sehemu ya kikosi cha umoja wa mataifa na watasaidia kikosi cha wanajeshi wa Umoja wa Afrika (Amisom) kukabiliana na Al-Shabaab. Idadi ya wanajeshi wa Uingereza nchini Somalia inatarajiwa kupanda hadi 70 ambao watahusika na shughuli za matibabu, mipango na...
WAZIRI wa mambo ya nchi za nje wa Marekani John Kerry amefungua siku ya pili ya mazungumzo mjini Geneva yenye lengo la kutafuta njia ya kupata suluhu ya mapigano nchini Syria. Kerry amekutana na Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Saudi Arabia Adel Al-Jubeir na anapanga pia kuwa na mazungumzo baadae na mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na Syria Staffan De Mistura. Waziri Kerry amesema hatua za maelewano kuhusu njia ya kupunguza mashambulizi mjini Aleppo zinaendelea kuimarika,...
Kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa kwenye tovuti ya Standard Digital nchini Kenya zinasema kuwa mashirika mawili ya serikali nchini humo yamewatangazia watumiaji wa njia za Lang’ata, Muhoho, Popo, Lusaka, Gichuru, Ushirika, Jakaya Kikwete, Lenana, Jogoo kuwa makini na barabara hizo kutokana na mafuriko, hivyo watumiaji wametakiwa kuepuka njia hizo katika kipindi cha mvua kubwa zinazopelekea kuharibika kwa miundombinu ya...