MASHIRIKA ya misaada yamesema kuwa hali ya hewa ya El Nino ambayo imekuwa ndiyo kali zaidi katika historia itazidisha hatari ya njaa na maradhi kwa mamilioni ya watu duniani 2016. Hali hii ya hewa inatarajiwa kusababisha ukame baadhi ya maeneo na mafuriko kwingine, ambapo baadhi ya maeneo yanayotarajiwa kuathirika sana yako Afrika, huku uhaba wa chakula ukitarajiwa kufikia kilele mwezi Februari. Hali ya hewa ya El Nino, hutokana na kuongezeka kwa joto na huathiri hali ya hewa maeneo...
UMOJA wa Afrika leo umetishia kuyawekea vikwazo makundi hasimu nchini Burundi iwapo yatashindwa kuhudhuria mazungumzo ya amani mwezi ujao, wakati ukiibana serikali kukubali jeshi la kulinda amani. Serikali ya Burundi na upinzani, pande zilizokutana nchini Uganda siku ya Jumatatu, zinatarajiwa kukutana tena Januari Mjini Arusha kwa mazungumzo yenye lengo la kumaliza miezi kadhaa ya ...
WANANCHI wa Jamuhuri ya Afrika ya kati hii leo wanashiriki katika zoezi la uchaguzi wa Rais na wabunge nchini humo. Uchaguzi huo uliokuwa ufanyike tarehe 27 mwezi huu ulisogezwa mbele na tume ya uchaguzi nchini humo hadi tarehe ya leo Desemba 30 kutokana na kasoro zilizojitokeza wakati wa kipindi cha maandalizi ya uchaguzi huo. Msemaji wa Tume ya uchaguzi nchini humo Julius Rufin Ngoadebaba ameahidi kuwa uchaguzi huo utakwenda vizuri katika maeneo yote nchini humo ambako Zaidi ya...
MASHAMBULIZI ya angani yanayoongozwa na Marekani yamefanikisha kuwaua viongozi kumi wa kundi la itikadi kali la Dola la Kiisilamu katika kipindi cha mwezi uliopita wakiwemo wanaodaiwa kuhusika na shambulizi la mjini Paris au mashambulizi mengine ambayo yalipangwa kufanyika barani ulaya . Afisa mmoja wa jeshi la Marekani nchini Iraq Kanali Steve Warren amesema wanamgambo hao waliuawa wakati wa mashambulizi ya anga yaliyofanywa nchini Iraq na Syria. Kwa mujibu wa Warren mmoja wa walioua katika mashambulizi hayo ni...
MELI iliyobeba kilo 11,000 za madini ya Urani ambayo yamerutubishwa kwa kiwango kidogo imeng’oa nanga nchini Iran ikielekea Urusi, katika hatua ya Iran kutekeleza makubaliano kuhusu mpango wake wa nyuklia ambayo yalifikiwa tarehe 14 Julai baina yake na mataifa yenye nguvu duniani. Hayo yamethibitishwa na Marekani. Huku kipengele muhimu cha makubaliano hayo kinaitaka Iran kupunguza akiba yake ya madini ya Urani yaliyorutubishwa kiasi hadi chini ya kilo 300. Yakirutubishwa zaidi, madini hayo yanaweza kutumiwa kuunda silaha za nyuklia, azma...
WAZIRI MKUU wa zamani wa Israel Ehud Olmert ametakiwa kutumikia kifungo cha miezi 18 jela kwa makosa ya rushwa. Olmert alikuwa amehukumiwa kifungo cha miaka sita jela na mahakama mwaka 2014, lakini adhabu hiyo sasa imepunguzwa na Mahakama ya Juu. Mwanasiasa huyo wa umri wa miaka 70 alipatikana na hatia kuhusu mkataba wa ujenzi wa nyumba ambao ulifanyika alipokuwa meya wa Jerusalem, kabla yake kuwa waziri mkuu...
MAREKANI imelipongeza jeshi la Iraq kwa kuweza kuurejesha mji wa Ramadi uliokuwa ukishikiliwa na wapiganaji wa Islamic State. Waziri wa Ulinzi wa Marekani Ash Carter amesifu hatua hiyo kwa kusema ni muhimu katika kulishinda kundi hilo, aliloliita kuwa ni la kipuuzi. Amesema ni muhimu pia kwa mamlaka za Iraq kwa kupata nasafi ya kudhibiti amani katika mji huo wa Ramadi na kudhibiti kurudi tena kwa kundi hilo la IS....
SHIRIKA la Afya Duniani leo linatarajiwa kuitangaza Guinea kuwa nchi isiyo na maambukizo ya ugonjwa wa Ebola. Mlipuko wa virusi vya ugonjwa wa Ebola ulianza nchini humo miaka miwili iliyopita. Ugonjwa wa Ebola umesababisha vifo vya maelfu ya watu katika nchi za Afrika magharibi, hususan katika nchi za Guinea, Liberia na Sierra Leone. Waguinea wanajiandaa kusherehekea kumalizika kwa janga hilo nchini mwao kwa kufanya maonesho na kurusha...
WATU 43 wameuawa katika kipindi cha siku tano zilizopita kutokana na kimbunga maeneo ya kusini na magharibi mwa Marekani. Mafuriko, upepo mkali na barafu vimeharibu mamia ya nyumba na biashara na hivyo kuyumbisha shughuli za uchukuzi. Idara ya taifa ya utabiri wa hali ya hewa nchini humo imetoa tahadhari ya kutokea kwa vimbunga katika majimbo ya Texas, Arkansas, Louisiana, Oklahoma and...
WATU wawili wamefariki na wengine watatu kujeruhiwa baada ya wanajeshi kufyatulia risasi gari moja mjini Mandera katika hali ya kutatanisha. Wanajeshi wamekuwa wakifanya operesheni kali mjini humo baada ya kuripotiwa kwa visa kadha vya mashambulio ya kigaidi siku za hivi karibuni. Maafisa wanne wa polisi wameuawa kwenye mashambulio kadha katika mji huo ulioko kaskazini mashariki mwa Kenya katika kipindi cha wiki...
Taarifa kutoka Yemen zinasema aliyekuwa mlinzi wa Osama Bin Laden, amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu. Vyanzo vya habari vya kitabibu vinaeleza kwamba Nasser al Bahri ambaye pia alikuwa akijulikana kama Abu Jandal alifariki siku ya Jumamosi, katika Hospitali iliyoko kwenye mji wa Mukalla kusini mwa Yemen. Alirudi nchini humo mwishoni mwa mwaka 2008, baada ya kuachiliwa kutoka katika kizuizi alichowekewa na Marekani huko...