MIAKA miwili tangu machafuko yalipoanza Sudan kusini, mashirika ya misaada yametahadharisha kuhusu upungufu mkubwa wa chakula unaotarajia kuikumba nchi hiyo na kutaka hatua za haraka zichukuliwe ili kumaliza vitendo vya uhalifu wa kivita ndani ya Taifa hilo. Ingawa makubaliano ya amani yalitiwa saini miezi kadhaa iliyopita, machafuko bado yanaendelea na karibu watu milioni moja na laki Tano wamelazimika kuyahama makazi yao. Tangu kuanza kwa mapigano nchi nzima miaka miwili iliyopita, Rais na makamu wa rais wa zamani wa nchi hiyo...
WAZIRI wa Mambo ya nje wa Marekani John Kerry yupo nchini Moscow kwa ajili ya mazungumzo na Rais Vladimir Putin kuhusu njia za kumaliza vita vinavyoendelea nchini Syria. Mazungumzo hayo yanalenga kupunguza mfarakano kati ya Urusi na Marekani, hasa kuhusu makundi ambayo yanafaa kujumuishwa kwenye mazungumzo ya mzozo huo. Urusi ambayo inamuunga mkono Rais wa Syria Bashar Al-Assad, imesema mkutano uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita wa makundi yanayopinga serikali ya Syria haukuwakilisha makundi yote yanayovutana katika mzozo...
KUNDI kuu la kiislamu nchini Nigeria linaloungwa mkono na waislamu wa Kishia wa Iran, linasema kuwa mke wa kiongozi mkuu Sheikh Ibrahim Zakzaky, ameuwawa katika makabiliano na jeshi kaskazini mwa mji wa Zaria. Vuguvugu la kiislamu nchini Nigeria (IMN) linadai kuwa Zeenat Ibraheem ameuwawa kwa pamoja na mwanaye Sayyid Ibraheem Zakzaky. Sheikh Zakzaky alikamatwa na wanajeshi waliozingira nyumba yao kufuatia madai kuwa wanachama wa kundi hilo walijaribu kumuua kamanda mkuu wa jeshi Jenerali Tukur Buratai huko Zaria siku...
MAAFISA wa upelelezi wa ajali za ndege kutoka Misri wamesema kuwa hawajapata ushahidi wowote kuwa ndege ya Urusi iliyoanguka katika rasi ya Sinai na kuua watu 224 ililipuliwa. Ndege hiyo iliyokuwa ikitokea Sharm el-Sheikh ikielekea Moscow ilianguka jangwani mwezi Oktoba. Kundi moja la wapiganaji wanaoliunga mkono kundi la Islamic State –IS, walidai kuwa wao ndio walioidungua ndege...
SERIKALI ya Marekani imeshauri Raia wake walio nchini Burundi kuondoka nchini humo haraka iwezekanavyo baada ya watu 87 kuuawa kwenye ghasia zilizotokea siku ya Ijumaa. Ghasia zilizojitokeza kwenye mitaa ya mji mkuu wa nchi hiyo, Bujumbura ni mbaya zaidi tangu kuanza kwa vurugu mwezi Aprili mwaka huu , baada ya Rais Pierre Nkurunziza kuamua kuwania tena urais kwa muhula wa tatu. Shirika la kutetea haki za kibinadamu la Human Rights Watch (HRW) limeitisha uchunguzi kuhusu mauaji hayo ya...
RAIS Xi Jinping wa China na Barack Obama wa Marekani walikuwa na mazungumzo ya simu leo na kuahidi kwamba nchi zao zitaendelea kushirikiana katika suala la mabadiliko ya tabia nchi. Televisheni ya taifa nchini China imeripoti kwamba marais hao wawili wamesema watashirikiana kwa karibu kuendeleza mafanikio yatakayotokana na mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu tabia nchi unaoendelea mjini Paris, Nchini Ufaransa....
TUME ya Taifa ya Uchaguzi nchini-NEC-imewataka Wananchi waliojiandikisha kupiga Kura katika Majimbo na Kata husika, kujitokeza kwenye vituo walikojiandikisha siku ya Jumapili ili kuweza kupiga Kura na kuwachagua viongozi wanaowataka. Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Mstaafu Damiani Lubuva amesisitiza kwamba taratibu zilizotumika katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25 mwaka huu ndizo zitakazotumika katika uchaguzi...
SHIRIKA la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limesema jana kuwa muungano unaoongozwa na Saudi Arabia umeshambulia kwa mabomu shule nchini Yemen, na kukiuka sheria za kimataifa za kiutu na kuzuwia maelfu ya watoto kupata elimu. Shirika hilo lenye makao yake makuu mjini London limeyataka mataifa yote ambayo yanaupatia silaha muungano wa kijeshi unaoongozwa na Saudi Arabia , ikiwa ni pamoja na Marekani na Uingereza, kusitisha upelekaji...
WAZIRI wa mambo ya nje wa Ufaransa, Laurent Fabius, amewasilisha rasimu ya mkataba mpya kwa wajumbe katika mkutano mkuu unaojadili kuhusiana na mabadiliko ya tabia nchi mjini Paris, kwa usiku wa pili wa majadiliano. Fabius amesema kwamba lengo lao kuu ni kuhitimisha mazungumzo kwa dhima, sheria, matarajio,na makubaliano ya haki na ya kudumu mpaka kufikia leo, nakuongeza kusema kwamba wajumbe wa mkutano huo wanakaribia kufikia makubaliano ya mwisho. Awali, mkurugenzi wa kitengo cha Umoja wa Mataifa kinachojishughulisha na mazingira, Achim...
MPIGANAJI wa mwisho kati ya wapiganaji 11 wa Taliban ambao waliuzingira uwanja wa ndege wa Kandahar, Afghanistan ameuawa, zaidi ya saa 24, baada ya shambulizi kuanzishwa. Wizara ya Ulinzi ya Afghanistan imesema leo kuwa watu 50 wakiwemo raia na maafisa wa usalama, wameuawa. Shambulizi hilo ambalo ni kubwa dhidi ya kambi ya jeshi la anga nchini humo, lilifanyika sambamba na mkutano wa kikanda nchini Pakistan, ambako Rais Ashraf Ghani wa Afghanistan aliitaka Pakistan kusaidia kuanzisha tena mazungumzo ya...
VIONGOZI kadha kutoka eneo la Mandera, kaskazini mashariki mwa Kenya, wamekamatwa na polisi kuhusiana na madai ya kuwepo kwa makaburi yaliyozikwa miili ya watu kadha. Seneta Billow Kerrow amekamatwa pamoja na wabunge wengine wanne baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Wilson, Nairobi na kupelekwa makao makuu ya uchunguzi upande wa akosa ya...