Global News

MEXCO YARUHUSU MATUMIZI YA CHANJO YA DENGE
Global News

MEXICO imekuwa nchi ya kwanza duniani kuruhusu matumizi ya chanjo ya kukinga maradhi ya homa ya denge yanayowasibu karibu watu Milioni mia moja kila mwaka   duniani, na hasa katika nchi za joto. Idara kuu ya tiba nchini Mexico imesema chanjo hiyo ilifanyiwa majaribio kwa  wagonjwa zaidi yaelfu  40,000 katika  sehemu mbalimbali za dunia. Virusi vya homa ya denge husababisha mvujo wa damu wa ndani kwa ndani na kushindwa kwa viungo kufanya  kazi. Virusi hivyo vinaenezwa na mbu....

Like
291
0
Thursday, 10 December 2015
SHAMBULIO LA NDEGE YA MAREKANI LAUA KIONGOZI WA AL SHABAAB
Global News

KONGOZI mmoja wa kundi la Al Shabaab ameuawa katika shambulizi la ndege ya Marekani. Msemaji wa makao makuu ya ulinzi ya Marekani Peter Cook amesema kifo cha Abdirahman Sandhere ni pigo kubwa kwa usimamizi na uwezo wa mashambulizi ya kundi hilo linalounga mkono wanamgambo wa Al Qaeda. Al Shabaab inaendesha kampeini ya kuing’oa madarakani serikali inayoungwa mkono na jamii ya kimataifa inayoundwa na zaidi ya majeshi Elfu 22 wa umoja wa Afrika....

Like
272
0
Tuesday, 08 December 2015
ETHIOPIA YAONYWA KUKUMBWA NA BALAA LA NJAA
Global News

SERIKALI ya Ethiopia imeonya kuwa watu milioni 10 wanakabiliwa na janga la njaa kufuatia ukame mkubwa uliokumba maeneo mengi nchini humo. Ukame huo umekadiriwa kwamba utaathiri takriban watoto milioni 6 ambao watahitaji msaada wa chakula kuanzia mwezi ujao. Hata hivyo tayari Serikali imeanza kugawa chakula cha msaada kwa ushirikiano na mpango wa chakula duniani WFP kufuatia ukame ulioathiri mazao katika kipindi cha msimu...

Like
275
0
Tuesday, 08 December 2015
RUSHWA: MAHAKIMU 20 WAFUKUZWA KAZI GHANA
Global News

MAMLAKA ya mahakama nchini Ghana imewafuta kazi mahakimu 20 huku wengine wakiendelea kuchunguzwa kutokana na kuhusishwa na kashifa ya kupokea rushwa. Ufisadi wa mahakimu hao umebainika baada ya mwandishi wa habari za uchunguzi, Aremeyaw Anas, kukusanya kwa muda wa miaka miwili kanda za video zenye muda wa saa 500 kama ushahidi dhidi ya mahakimu 30. Kutokana na sakata hilo, baadhi ya mahakimu nchini Ghana wametaka kuwepo kwa mabadiliko katika mahakama nchini humo ili kukomesha vitendo...

Like
208
0
Tuesday, 08 December 2015
BURUNDI KUJADILIWA BRUSSELS LEO
Global News

MKUTANO wa ngazi za juu wa kujadili hali nchini Burundi utaanza leo mjini Brussels, Ubelgiji huku mada kuu ikiwa ni msukosuko wa kisiasa nchini humo na uhusiano wake na Umoja wa Ulaya. Mkutano huo, ambao utashirikisha viongozi wa ngazi za juu kutoka mataifa ya Afrika Mashariki, unafanyika kutokana na Umoja wa Ulaya kukusudia kuiwekea vikwazo vya kibiashara nchi ya Burundi. Umoja wa mataifa umesema kwamba kufuatia Burundi kushindwa kuheshimu vipengele muhimu katika mkataba wa ushirikiano umoja huo unatarajia kuanzisha utaratibu...

Like
199
0
Tuesday, 08 December 2015
UPINZANI WASHINDA UCHAGUZI VENEZUELA
Global News

CHAMA cha upinzani nchini Venezuela kimeshinda wingi wa viti bungeni kwa mara ya kwanza tangu chama cha kisoshiolisti kiingie madarakani 1999 chini ya uongozi wa rais wa zamani Hugo Chavez . Rais wa baraza kuu la chaguzi Tibisay Lucena, amesema kuwa upinzani umeshinda takriban viti 99 kati ya viti...

Like
224
0
Monday, 07 December 2015
DIENDERE ASHTAKIWA KWA KUHUSIKA NA MAUAJI YA SANKARA
Global News

KIONGOZI wa mapinduzi yaliyodumu kwa muda mfupi nchini Burkina Faso Jenerali Gilbert Diendere ameshtakiwa kwa kuhusika katika mauaji ya rais wa zamani wa nchi hiyo Thomas Sankara alieuawa mwaka 1987. Jenerali Gilbert Diendere ni afisa wa ngazi ya juu zaidi kushatakiwa kwa mauaji hayo. Rais Sankara aliuawa na kundi la askari, lakini mazingira halisi ya kifo chake yamekuwa...

Like
212
0
Monday, 07 December 2015
UFARANSA: NATIONAL FRONT PARTY YAONGOZA MATOKEO YA AWALI
Global News

KURA zilizohesabiwa katika awamu ya kwanza ya uchaguzi wa kikanda nchini Ufaransa, zinaonyesha chama cha National Front Party kinaongoza katika matokeo kwa asilimia 30 ya kura zote zilizopigwa. Uchaguzi huo ni wa kwanza kufanyika tangu kundi la kigaidi la wanamgambo wa dola ya Kiislamu la Islamic State kuua watu 130 mjini Paris mwezi uliopita. Chama Tawala cha kisoshalisti kimeshika nafasi ya tatu katika kura ingawa kimelazimika kujiondoa katika uchaguzi wa awamu ya pili katika mikoa miwili ikiwa ni jitihada za...

Like
246
0
Monday, 07 December 2015
OBAMA ATAJA SHAMBULIO LA CALIFORNIA KUWA NI LA KIGAIDI
Global News

RAIS wa Marekani Barack Obama amelihutubia Taifa lake kufuatia shambulio la risasi la wiki iliyopita katika jimbo la California ambalo lilisababisha vifo vya watu 14. Rais Obama amesema wazi kuwa hakuna ushahidi kwamba mhusika alikuwa anatekeleza mauaji hayo kwa maelekezo ya kundi lolote kutoka nje ya Marekani. Katika hotuba yake amesema kwamba shambulio hilo lilikuwa la kigaidi hivyo ni muhimu kupambana nalo bila kuchukua sura ya vita baina ya Marekani na waislamu bali ni kwa waislamu wenye itikadi kali za...

Like
190
0
Monday, 07 December 2015
THAILAND YAANZA KUCHUNGUZA MAGAIDI
Global News

POLISI nchini Thailand wanachunguza ripoti zinazoeleza kuwa wanamgambo kumi kutoka kundi la wapiganaji wa Islamic state wameingia nchini humo na wanapanga kushambulia sehemu zinazomilikiwa na Urusi. Taarifa hizo zimeeleza kwamba Sita kati yao wameripotiwa kuelekea maeneo ya kifahari ya Pattaya na Phuket huku wengine wakiwa hawajulikani waliko. Hata hivyo Polisi nchini humo wamesema kuwa hawajafanikiwa kuthibitisha uwepo wa raia hao wa Syria nchini...

Like
228
0
Friday, 04 December 2015
BOMU LAUA 16 MISRI
Global News

WATU 16 wameuawa katika mji mkuu wa Mirsi, Cairo, baada ya bomu kulipuliwa kwenye mgahawa mmoja lililopo eneo la Agouza, katikati ya jiji hilo. GAZETI la The Cairo Post linasema watu watatu waliokuwa wamejifunika nyuso zao walirusha bomu mgahawani na kisha kutoroka. Shirika la habari la Reuters limemnukuu afisa mmoja wa usalama, ambaye hakutajwa jina lake, akisema mmoja wa washukiwa ni mfanyakazi wa zamani wa mgahawa...

Like
238
0
Friday, 04 December 2015