Global News

GUINEA: MGONJWA WA MWISHO WA EBOLA APONA NA KURUHUSIWA
Global News

MAAFISA wa Afya nchini Guinea wamesema mgonjwa wa mwisho aliyeripotiwa kupata maradhi ya Ebola amepona na ameruhusiwa kutoka kwenye kituo cha matibabu kilichopo mji mkuu wa nchi hiyo, Conakry. Ugonjwa huo ulioanza nchini Guinea, umeua zaidi ya watu 11,000 Afrika magharibi ingawa tayari Nchi jirani za Sierra Leone na Liberia zimefanikiwa kuutokomeza ugonjwa huo. Mgonjwa mmoja aliyekuwa amebaki ni mtoto wa siku 19 ambaye mama yake alifariki kutokana na ugonjwa huo huku msemaji wa kitengo kinachoratibu mapambano dhidi ya Ebola...

Like
244
0
Tuesday, 17 November 2015
BAN KI-MOON KUANZA ZIARA KOREA KASKAZINI
Global News

KATIBU Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon anatarajiwa kufanya ziara nchini Korea Kaskazini, na hivyo kuwa kiongozi wa kwanza wa umoja huo duniani kuizuru nchi hiyo kwa zaidi ya miaka 20 iliyopita.   Shirika la habari la Korea Kusini, Yonhap, limesema kuwa Ban atazuru Korea Kaskazini baadae wiki hii, ingawa tarehe kamili bado haijatangazwa.   Hata hivyo taarifa kutoka ngazi za juu za Umoja wa Mataifa zimeeleza kwamba Ban alikuwa tayari kukutana na kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-Un,...

Like
219
0
Monday, 16 November 2015
UGANDA NA KENYA ZAIMARISHA USALAMA
Global News

NCHI za Uganda na Kenya zimeimarisha usalama kufuatia mashambulio yaliyojitokeza mjini Paris mwishoni mwa wiki lengo ikiwa ni  kuzuia mashambulio kutoka kwa wapiganaji wa Kiislamu. Msemaji wa polisi nchini Uganda amesema polisi na wanajeshi wameimarisha doria kuzuia mashambulio, hasa kutoka kwa wapiganaji wa Kiislamu wa Al-Shabaab kutoka Somalia. Nchini Kenya, usalama pia umeimarishwa mipakani na katika miji mikuu, na kuwataka wananchi kutoa taarifa haraka mara wanapoona kitu au mtu yeyote wanayemtilia...

Like
193
0
Monday, 16 November 2015
UFARANSA YAFANYA MASHUMBULIZI DHIDI YA IS
Global News

UFARANSA imefanya mashambulizi ya kulipiza kisasi dhidi ya kundi la Dola la Kiislamu katika mji wa Raqqa, nchini Syria. Mashambulizi hayo ya anga ni ya kwanza kufanywa na Ufaransa tangu mji wake mkuu, Paris, kushambuliwa usiku wa Ijumaa na kundi hilo, ambapo watu 132 waliuawa. Maafisa wa Ufaransa wamesema mabomu 20 yaliangushwa na ndege zaidi ya kumi, zilizoruka kutoka Umoja wa Falme za Kiarabu na Jordan, kwa kushirikiana na kituo cha kijeshi cha...

Like
170
0
Monday, 16 November 2015
SHAMBULIO LEBANON: TISA WAKAMATWA
Global News

IDARA za Usalama nchini Lebanon zimefanikiwa kuwakamata watu Tisa wanaodhaniwa kuhusika katika shambulio lililotokea Alhamisi ya wiki iliyopita na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 40. Taarifa zinaeleza kwamba watu Saba kati ya tisa wanaoshikiliwa na Polisi ni raia wa Syria huku wengine wawili ni raia wa Lebanon huku tayari kundi la wapiganaji wa Kiislamu limedai kuhusika na shambulio hilo. Hata hivyo Wachunguzi wamebaini kuwa washambuliaji hao waliilenga hospitali inayoendeshwa na taasisi ya wapiganaji wa majeshi ya Kilebanon ya madhehebu...

Like
178
0
Monday, 16 November 2015
MAREKANI YAMSHAMBULIA JIHAD JOHN
Global News

WANAJESHI wa Marekani wametekeleza shambulio la Anga lililomlenga mwanamgambo wa Islamic State kutoka Uingereza ajulikanaye  kwa jina la Jihadi John.   John alilengwa kwenye shambulio hilo lililotekelezwa karibu na mji wa Raqqa, nchini Syria kufuatia msimamo wake mkali pamoja na kuonekana kwenye video akiwakata shingo mateka wa kutoka mataifa ya Magharibi. Afisa wa habari wa Pentagon-Peter Cook amesema kuwa wanaamini matokeo ya operesheni ya leo usiku italeta manufaa makubwa kulingana na malengo yao.  ...

Like
180
0
Friday, 13 November 2015
WAPIGANAJI WA KIKURDI WAUTWAA MJI WA SINJAR
Global News

WAPIGANAJI wa Kikurdi wamefanikiwa kuingia mji wa Sinjar kaskazini mwa Iraq, siku moja baada yao kuanza kwa operesheni ya kuutwaa kutoka kwa wapiganaji wa Islamic State. Wakati hayo yakijiri, jeshi la Iraq limesema limeanzisha operesheni ya kuukomboa mji wa Ramadi magharibi mwa nchi hiyo ambao ulikuwa umetekwa na wapiganaji wa IS. Hata hivyo hatua ya Kuukomboa mji wa Sinjar kutaziba mawasiliano kati ya ngome mbili za IS Raqqa na Mosul....

Like
195
0
Friday, 13 November 2015
POLISI ULAYA WASHIKILIA WATU 17
Global News

POLISI katika nchi sita za Ulaya wamewakamata watu 17, kwa tuhuma za kupanga mashambulizi. Watu hao wengi wao wakiwa ni Wakurd wa Iraq, wanachama wa kundi la Wapiganaji wa Kiislamu wanadaiwa kupanga mashambulizi nchini Norway na Mashariki ya Kati. Hata hivyo Polisi wamesema kundi hilo lilikuwa likijiandaa kufanya mashambulizi ili kumuokoa kiongozi wake, mwenye msimamo mkali, Mullah Krekar anayeshikiliwa nchini Norway....

Like
185
0
Friday, 13 November 2015
MAREKANI YAIONDOLEA LIBERIA VIKWAZO VYA KIUCHUMI
Global News

MAREKANI imeiondolea Liberia vikwazo vya kiuchumi huku Rais Barack Obama akiipongeza nchi hiyo kwa kujitolea kufanikisha demokrasia tangu kumalizika kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe mwaka 2003. Vikwazo hivyo viliwekwa miaka 11 iliyopita dhidi ya kiongozi wa wakati huo Charles Talyor ambaye kwa sasa yupo gerezani kwa makosa ya uhalifu wa kivita. Kwa mujibu wa Ikulu ya Marekani, Rais Obama amesema kwa kuwa utawala wa Taylor ulimalizika na tayari kwa sasa yupo gerezani ina maana kwamba vikwazo hivyo havihitajiki...

Like
177
0
Friday, 13 November 2015
AFRIKA NA ULAYA ZAKUBALIANA KUPUNGUZA IDADI YA WAHAMIAJI
Global News

VIONGOZI wa Muungano wa Ulaya na Afrika wametia saini makubaliano yanayotarajia kupunguza idadi ya wahamiaji wanaofunga safari hatari ya kutaka kufika Ulaya. Wakizungumza kwenye mkutano huo viongozi hao wameidhinisha kuundwa kwa hazina ya dola bilioni 1.9 bilioni za kusaidia mataifa ya Afrika katika suala la kukabiliana na wakimbizi. Miongoni mwa mataifa yatakayonufaika kutokana na hazina hiyo ni Kenya, Tanzania, Uganda, Djibouti, Somalia, Sudan Kusini, Eritrea na Ethiopia....

Like
289
0
Thursday, 12 November 2015
UN YATAFAKARI KUTUMA VIKOSI BURUNDI
Global News

UMOJA wa Mataifa unatafakari wazo la kutuma walinda Amani nchini Burundi iwapo machafuko nchini humo yatazidi kuendelea. Watu zaidi ya 200 tayari wameuawa huku maelfu ya wengine wakihama makazi yao tangu Aprili, mara baada ya Rais Pierre Nkurunziza kutangaza kuwania urais kwa muhula wa tatu. Muungano wa Afrika tayari umekitaka kikosi cha polisi wa akiba cha kanda ya Afrika Mashariki kuwa tayari kutumwa Burundi iwapo hali ya Amani itakuwa mbaya...

Like
182
0
Thursday, 12 November 2015