JESHI la Kenya limetuhumiwa kujihusisha na shughuli mbalimbali kinyume na malengo ikiwemo kufanya biashara badala ya kufanya kazi zinazowahusu nchini Somalia. Taasisi ya Waandishi wa habari Wanaopigania haki imelituhumu Jeshi hilo kujiingiza katika masuala mbalimbali ya kibiashara yanayowaletea faida na kuacha kazi ya iliyowapeleka ya kulinda Amani. Hata hivyo Taasisi hiyo imewalaumu baadhi ya maofisa wa jeshi hilo kushirikiana katika biashara haramu na wapiganaji wa Al Shabaab jambo ambalo ni kinyume cha...
KIONGOZI wa upinzani nchini Myanmar Aung Suu Kyi, leo ametoa wito wa kuwepo kwa mazungumzo ya kitaifa ya upatanishi kati ya rais wa Myanmar na mkuu wa jeshi la nchi hiyo lenye nguvu kubwa kisiasa baada ya chama chake kuonekana kupata ushindi wa kishindo katika Uchaguzi mkuu. Chama cha National League for Demcracy-NLD-kimeonekana kupata madaraka baada ya kupata asilimia 90 ya viti vilivyotangazwa hadi sasa sawa na viti 163 kati ya viti 182 vilivyotangazwa hadi sasa....
MAAFISA wanane wa polisi waliopatikana na hatia ya kumfanyia ukatili dereva wa teksi kutoka Msumbiji mwaka 2013 wamehukumiwa kifungo cha miaka 15 kila mmoja. Maafisa hao walinaswa kwenye kanda ya video wakimburuza dereva wa gari ndogo (teksi) kutoka Msumbuji aliyetambuliwa kwa jina la Macia mwenye umri wa miaka 27 mtaa wa Macia mashariki mwa Johannesburg. Awali kabla ya kutokea kwa tukio hilo Macia alikuwa amesimamishwa na maafisa tisa wa polisi kwa kosa la kuvunja sheria za usalama...
WATAALAMU wa Afya wamesema kuwa mpango wa chanjo kwa umma dhidi ya homa ya uti wa mgongo barani Afrika umepata mafanikio makubwa. Zaidi ya watu milioni mbili walipata kinga dhidi ya maradhi hayo katika nchi 16 barani Afrika, ikiwemo Gambia na Ethiopia. Shirika la Afya Duniani limesema katika kipindi cha mwaka 2013 kulikuwa na wagonjwa wanne wa Uti wa mgongo barani Afrika ingawa awali iliweka rekodi ya kuwa na maelfu ya vifo vinavyotokana na ugonjwa huo kila...
DONALD TRUMP, mmoja wa wanaowania nafasi ya Urais kupitia chama cha Republican katika Uchaguzi mkuu nchini Marekani, ameshutumiwa vikali kutokana na mpango wake wa kuwafukuza wahamiaji milioni 11 kutoka nchini humo. Kwenye mdahalo wa moja kwa moja kupitia runinga, wagombea wengine wawili wanaoshindana naye, John Kasich na Jeb Bush, waliukosoa vikali mpango huo wakisema hauwezi kutekelezeka na ni kitendo cha ubaguzi. Hali hiyo imesababisha watu waliohudhuria mdahalo huo kumzomea Trump, wakati alipojaribu kujitetea kuhusu huo mpango...
RAIS wa Marekani Barack Obama na waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu wamekubaliana kuweka kando mvutano uliosababishwa na kutiwa saini makubaliano ya mradi wa nyuklia wa Iran na kuweka nguvu za pamoja kutetea maslahi ya nchi zao mbili katika eneo la mashariki ya kati. Wakifanya mkutano wa pamoja kwa mara ya kwanza baada ya kupita miezi 13 katika Ikulu ya Marekani rais Obama amesema wazi kuwa usalama wa Israel ndio suala muhimu. Rais Obama na waziri mkuu wa...
KIONGOZI wa upinzani nchini Myanmar Bi. Suu Kyi amesema kwamba uchaguzi mkuu uliofanyika Jumapili iliyopita nchini humo haukuwa huru lakini ulikuwa wa haki. Kwenye mahojiano ya kipekee, Bi Suu Kyi aliwapongeza wananchi wa Myanmar kwa kumpigia kura ingawa Chini ya katiba ya nchi hiyo hawezi akawa rais, lakini amesema kwamba kama kiongozi wa chama atamteua rais. Uchaguz huo umechukuliwa na wengi kuwa ndio wa kidemokrasia zaidi katika kipindi cha miaka 25, baada ya miongo kadhaa ya uongozi wa...
CHAD imetangaza hali ya hatari eneo la Ziwa Chad baada ya kuongezeka kwa mashambulio kutoka kwa wapiganaji wa Boko Haram kutoka Nigeria. Uamuzi huo umechukuliwa baada ya watu wawili kuuawa katika shambulio la kujitoa mhanga linalodaiwa kutekelezwa na kundi la wanamgambo hao. Boko Haram wanashukiwa kuhusika katika mauaji ya watu wawili katika kijiji kimoja nchini Chad Jumapili iliyopita na wakimbizi watatu kutoka Nigeria kaskazini mwa Cameroon...
UFARANSA imependekeza hatua kali zichukuliwe kwaajili ya kusitisha mauaji ambayo yamekuwa yakiendelea nchini Burundi. Taifa hilo liliwasilisha muswada wa mapendekezo kwa Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa Jumatatu iliyopita likieleza wasiwasi wake juu ya hali ya usalama nchini Burundi. Ghasia zilianza mwezi Aprili baada ya maandamano ya kupinga hatua ya Rais Pierre Nkurunziza kutangaza kuwania urais kwa muhula wa tatu huku ikiaminika kuwa Machafuko hayo ndiyo mabaya zaidi nchini humo katika kipindi cha miaka kumi...
MKURUGENZI Mkuu wa kampuni ya simu ya MTN amejiuzulu kufuatia kampuni hiyo kutozwa faini kubwa ya dola bilioni 5.2 na Nigeria Mkuu huyo wa kampuni hiyo kubwa zaidi barani Afrika Sifiso Dabengwa, aliwasilisha barua ya kujiuzulu mara moja kwa maslahi ya wenye hisa na uendelevu wa kampuni hiyo. Faini hiyo ilitozwa na Tume ya mawasiliano ya Nigeria kufuatia uamuzi wa MTN kukataa kuzima namba za simu ambazo hazijasajiliwa kwa mujibu wa kanuni mpya za Taifa hilo....
IMEELEZWA kuwa nchi ya Iran imenunua silaha kali ya ulinzi dhidi ya ndege za kivita na makombora kutoka Urusi ikiwemo Mtambo wa S-300 wenye uwezo wa kudungua ndege na makombora yakiwa umbali wa kilomita 300. Hii si mara ya kwanza kwa Urusi kufanya makubaliano kama hayo na Iran ambapo Mwaka wa 2007 mataifa hayo yalikubaliana kuhusiana na mitambo hiyo ya ulinzi wa anga lakini walisitisha utekelezaji wake kufuatia marufuku iliyowekewa Iran kutokana na mipango yake ya kumiliki silaha za nyuklia....