WAKATI Burundi ikiendelea kukabiliwa na ghasia kutoka wa upinzani baada ya kuchaguliwa kwa Rais Pierre Nkurunziza kuongoza kwa mhula wa tatu katika mazingira yenye utata, rais huyo ametoa ilani ya mwisho kwa wale aliowataja kuwa watenda mabaya kujisalimisha. Katika hotuba yake kwa Taifa, Nkurunziza amesema kuwa wale ambao hawatajisalimisha katika kipindi cha siku tano zijazo watashtakiwa kama maadui wa Taifa. Hayo yamejiri wakati mauaji yakiendelea kuripotiwa katika mji mkuu wa Bujumbura ambapo watu kadhaa wameuwawa kutokana na...
UTATA umeendelea kujitokeza katika ajali ya ndege iliyoanguka katika rasi ya Sinai huko nchini Misri na kuua abiria 224 waliokuwemo kwenye ndege hiyo. Wakati mkuu wa Mamlaka ya Anga ya nchini Urusi Aleksandar Neradko akisema kuwa ni mapema kutabiri chanzo cha ajali hiyo, lakini wamiliki wa ndege hiyo wamesema ajali imesababishwa na nguvu ya mvutano kutoka kutoka nje. Kwa upande wake Balozi wa Urusi nchini Misri Serge Kirpichenko amesema itachukua muda mrefu kabla ya kupata taarifa sahihi kutoka kwenye...
TAARIFA kutoka nchini Syria zinaeleza kwamba ,waasi nchini humo wanatumia askari mateka wanajeshi na wengine wenye uhusiano na serikali kama ngao yao ili kujikinga na mashambulizi ya askari wa serikali ya rais Bashar al-Assad. Mkanda wa video uliooneshwa katika mitandao ya kijamii inaonesha wanawake na wanaume waliofungwa katika vikinga vya chuma vilivyowekwa nyuma ya malori na magari hayo kuendeshwa taratibu katika mitaa ya mji mkuu wa nchi hiyo Damascus. Inasemekana video hiyo imetoka katika eneo linalokaliwa na waasi katika vitongoji...
CHAMA cha AK cha Uturuki kimepata viti vingi vya bunge vitakavyoweza kudhibiti bunge la nchi hiyo baada ya kupoteza miezi mitano iliyopita. Matokeo rasmi yanatarajiwa kutangazwa kwa siku kadhaa zijazo lakini karibu kura zote zimeshahesabiwa ambapo chama hicho cha AK kimejikusanyia zaidi ya asimilia hamsini kutawala bunge. Matokeo hayo yatampa nguvu rais Recep Tayyip Erdogan ambaye aliita kura hiyo kama kura ya amani na ujumbe kwa wanamgambo wa kikurdi na kudai kuwa vurugu haziwezi kuishinda...
KATIBU Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ametoa wito kwa mataifa kuweka kando misimamo mikali wakati wa mashauriano mjini Vienna kuhusu mapigano yanayoendelea nchini Syria. Aidha amewataka washiriki watano wakuu ambao ni Marekani, Urusi, Iran, Saudi Arabia na Uturuki, kuacha mtazamo wa utaifa na kukumbatia mtazamo wa kutoa uongozi kwa ulimwengu. Hata hivyo Marekani na washirika wake wamesisitiza kwamba Rais Assad hawezi kuwa sehemu ya suluhu juu ya mzozo unaoendelea katika Taifa...
Rais wa mpito wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Catherine Samba-Panza, ameonya kuwa maadui wa Amani wanaojaribu kuzuia uchaguzi mkuu nchini humo usifanyike mwezi Disemba. Uchaguzi huo ulikuwa umepangwa kufanyika mwezi Septemba lakini ukaahirishwa baada ya kuzuka tena kwa makabiliano kati ya Wakristo na Waislamu na kusababisha watu 40 kuawa. Hata hivyo Rais Samba amesema suluhu pekee ya kumaliza matatizo hayo ni kuwa na serikali halali iliyochaguliwa na...
HALI katika mji mkuu wa Haiti ni tete baada ya wafuasi wa mgombea mmoja wa kiti cha urais kuleta vurugu kwa kuwasha moto magurudumu ya magari na kuweka vizuzi barabarani. Vurugu hizo zimejiri baada ya mgombea wanaomuunga mkono Moise Jean-Charles, kudai kuwa kura zake zimeteketezwa moto na zingine kufichwa. Hatha hivyo wanaishtumu tume ya uchaguzi nchini humo kwa kukiuka kanuni na utendaji wa uchaguzi huru na wa...
MWANASIASA wa chama cha Republican nchini Marekani Paul Ryan ameteuliwa kuwa Spika wa Bunge la Wawakilishi nchini Marekani. Ryan, anayetoka jimbo la Wisconsin, hakutaka kuwania mwanzoni lakini mwisho alijitosa kwenye kinyang’anyiro na kuungwa mkono na wengi wa wabunge wa Republican katika Bunge la Congress kumrithi John Boehner aliyetoka Ohio. Mwanasiasa huyo mwenye umri wa miaka 45 alikuwa mgombea mwenza wa mgombea urais kwa tiketi ya chama cha Republican Mitt Romney mwaka...
WANADIPLOMASIA wa ngazi za juu duniani wanakutana mjini Vienna leo kujaribu kusaka ufumbuzi wa pamoja wa namna ya kuvimaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Syria. Wanadiplomasia hao kutoka Urusi, Marekani, Saud Arabia na Uturuki wanakutana kwa duru ya pili ya mazungumzo kuhusu Syria, baada ya ile ya wiki iliyopita kabla ya kuitishwa mkutano utakaowajumuisha wanadiplomasia wa eneo hilo. Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Iran Javad Zarif atajiunga na wenzake kutoka Uingereza, Misri, Ufaransa, Ujerumani na Umoja...
WANAOWANIA nafasi ya kuwania urais wa Marekani kwa tiketi ya chama cha Republican jana wamejibizana vikali kwenye mdahalo wa tatu ulioandaliwa katika jimbo la Colorado. Donald Trump na Ben Carson, ambao hawana uzoefu mkubwa kisiasa lakini ndio wanaoongoza kinyang’anyiro hicho, wameshambuliwa kwenye mdahalo huku Gavana wa Ohio John Kasich akiukashifu mpango wake “wa ndoto kuhusu ushuru”. Hata hivyo Pendekezo lake kuhusu ushuru, lilishutumiwa vikali na Kasich, ambaye pia alishutumu vikali mpango wa Trump wa kuwaondoa wahamiaji milioni 11...
MUUNGANO wa Afrika umelilaumu Jeshi la serikali ya Sudan Kusini na vikosi vya waasi kwa ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu na uhalifu wa kivita. Uchunguzi wa AU umebaini kuwa mapigano yaliyotokea mwezi Disemba mwaka 2013 yalitokana na mzozo kati ya makabila ya Dinka na Nuer ndani ya kikosi cha kumlinda Rais. Aidha uchunguzi huo umebaini kuwa vikosi hivyo hasimu viliwachinja watu na kuwalazimisha watu waliodhaniwa kuwa mahasimu wao kula nyama ya binadamu na kunywa damu...