Global News

NEPAL YAPATA RAIS WA KWANZA MWANAMKE
Global News

BUNGE la nchini Nepal limemchagua mtetezi wa haki za wanawake Bidhya Devi Bhandari kuwa rais wa kwanza mwanamke, katika hatua ambayo imetajwa kuwa ya kihistoria. Mwanamke huyo wa miaka 54 kwa sasa ndiye Naibu mwenyekiti wa chama tawala cha kikomunisti ambaye awali alikuwa waziri wa ulinzi mwaka 2009 na 2011. Bhandari atachukua nafasi ya Ram Baran Yadav, aliyekuwa rais wa kwanza wa Taifa hilo kuchaguliwa na watu mwaka 2008 baada ya Nepal kufuta utawala wa...

Like
353
0
Thursday, 29 October 2015
MAREKANI KUIMARISHA MASHAMBULIZI YA ANGA DHIDI YA IS SYRIA NA IRAQ
Global News

WAZIRI wa Ulinzi wa Marekani Ashton Carter amesema Marekani inapanga kuimarisha mashambulizi yake ya anga dhidi ya kundi la kigaidi la Dola la Kiislamu nchini Iraq na Syria. Akizungumza mbele ya Kamati ya Seneti kuhusu masuala ya ulinzi, waziri Carter amewaambia maseneta kuwa majeshi ya Marekani yatailenga miundo mbinu ya mafuta inayomilikiwa na kundi hilo na pia kuimarisha mafunzo ya wanajeshi wa mataifa ya Kiarabu wanaopambana ardhini na wanamgambo wa IS. Marekani na Urusi zina malengo yanayokinzana katika eneo hilo,...

Like
221
0
Wednesday, 28 October 2015
UN YAUNGA MKONO AZIMIO LINALOTOA WITO KWA MAREKANI KUIONDOLEA VIKWAZO CUBA
Global News

MKUTANO mKuu wa Umoja wa Mataifa umeunga mkono kwa kauli moja azimio linalotoa wito kwa Marekani kuondoa vikwazo dhidi ya Cuba. Baraza kuu la Umoja wa Mataifa lilipata kura 191 dhidi ya 2 kulaani vikwazo vya kibiashara, kiuchumi na kifedha ambavyo Marekani imeliwekea taifa hilo la kikomunisti. Hata hivyo ingawa kura hizo zilipigwa bado Marekani ilipiga kura ya kupinga azimio hilo la Vikwazo vilivyowekwa tangu mwaka 1960, wakati wa kilele cha Vita Baridi, Marekani ilipovunja mahusiano yake na...

Like
200
0
Wednesday, 28 October 2015
DRC: WANAHARAKATI WAMEZIONYA SHULE KUTOSAJILI WATOTO JESHINI
Global News

WANAHARAKATI wa kutetea Haki za Binadamu wamezionya shule za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo-DRC, kutowaandikisha watoto wa shule hizo kujiunga jeshini. Kundi la wanaharakati hao lenye makao yake makuu nchini Marekani limesema kuwa makundi yenye silaha yamekuwa yakiwateka wanafunzi katika majimbo ya Kivu ya kaskazini na kusini na kuwalazimisha kujiunga na Jeshi. Katika ripoti yake, kundi hilo pia limeyalaumu makundi ya waasi na jeshi la serikali ya Congo, kwa kutumia shule kama kambi zake za kijeshi au kuhifadhia...

Like
264
0
Wednesday, 28 October 2015
OUTTARA ASHINDA UCHAGUZI IVORY COAST
Global News

TUME ya Taifa ya Uchaguzi nchini Ivory Coast imemtangaza Alassane Ouattara kuwa mshindi wa uchaguzi wa urais nchini humo kwa ushindi wa asilimia 83.66. Raia wa Ivory Coast wameonesha kufurahishwa na ushindi wa Rais Alassane Outtara kama walivyotarajiwa kwamba rais huyo ataongoza kwa muhula mwingine wa miaka mitano. Baada ya mwongo mmoja wa kutoimarika kwa uchumi na vita vya wenyewe kwa wenyewe, wengi watafurahia kwamba uchaguzi huo ulifanyika kwa...

Like
223
0
Wednesday, 28 October 2015
PEGIDA LAONGEZA WAFUASI UJERUMANI
Global News

KUNDI  linalopinga  uhamiaji PEGIDA  limehamasisha  idadi kubwa  ya  watu  wanaoliunga  mkono  katika  mji  wa mashariki  nchini  Ujerumani  wa  Dresden kujiunga na kundi hilo. Kwa  mujibu  wa  kundi huru la wanafunzi linalofanya utafiti la Durchgezält, mkutano  wa  PEGIDA ulihudhuriwa na  watu  kati  ya  Elfu kumi hadi Elfu kumi na mbili. Lutz Bachmann, mmoja  kati  ya  waasisi  wa  kundi  hilo, alihutubia  hadhara  hiyo  na  kukosoa msimamo  wa serikali  ya  kansela  Angela  Merkel, akidai imechukua...

Like
198
0
Tuesday, 27 October 2015
PIS YASHINDA UCHAGUZI POLAND
Global News

CHAMA cha kihafidhina nchini Poland cha sheria na haki PiS kimeshinda uchaguzi  mkuu  uliofanyika Jumapili iliyopita kwa  mujibu  wa  matokeo  rasmi  yaliyotangazwa jana  jumatatu. Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Tume ya Uchaguzi zinasema kuwa Chama  cha  PiS  kilipata  asilimia  37.6  ya kura, huku  chama  cha  Civic Platform PO kimeshika  nafasi ya  pili kwa kupata  asilimia  24.1. Mgawanyiko  rasmi  wa  viti  bungeni ulikuwa bado haujapatikana, lakini  wadadisi  wanasema  matokeo huenda  yakatoa kwa ...

Like
194
0
Tuesday, 27 October 2015
PAKISTAN: 260 WAPOTEZA MAISHA KWA TETEMEKO LA ARDHI
Global News

Makundi ya uokoaji yanaendelea na juhudi za kuyafikia maeneo ya Kaskazini mwa Pakistan na nchi jirani ya Afghanistan, ili kuwaokoa watu wanodhaniwa kuwa wameathirika na tetemeko kubwa la ardhi lililokumba eneo hilo jana. Hadi sasa imeelezwa kuwa zaidi ya watu 260 wamefariki, kutokana na tetemeko hilo ambalo halijawahi kutokea tangu kipindi cha muongo mmoja uliopita. Hata hivyo baadhi ya maeneo yaliyoathirika zaidi nchini Afghanistan, yanadhibitiwa na wanamgambo wa Taliban, na kusababisha hali kuwa ngumu ya...

Like
174
0
Tuesday, 27 October 2015
MAWAZIRI WA ULINZI UJERUMANI NA IRAQ KUKUTANA
Global News

WAZIRI wa ulinzi wa Ujerumani Ursula von der Leyen anatarajiwa kukutana na waziri mwenzake wa Iraq kutafuta njia za kurekebisha hali inayosababisha watu kuikimbia nchi hiyo. Akiwa mjini Baghad waziri huyo anatarajiwa kukutana na Waziri Mkuu Haider al Abadi na waziri wa ulinzi Khaled al Obeidi kwaajili ya mazungumzo hayo. Akizungumza jana usiku kabla ya kuanza ziara yake hiyo von der Leyen amehimiza kuwepo kwa umoja ndani ya serikali ya Iraq na kuongeza kwamba maslahi ya Ujerumani katika eneo hilo...

Like
182
0
Tuesday, 27 October 2015
WANAMGAMBO WA IS WASHAMBULIWA DIYABAKIR
Global News

WANAMGAMBO wanne wanaotuhumiwa kuwa wa kundi la Dola la Kiislamu wameuwawa leo pamoja na polisi wawili wa Uturuki katika mashambuliano ya risasi yaliyotokea katika mji wa Diyabakir kusini mashariki mwa Uturuki. Taarifa kutoka usalama zimesema kuwa polisi ilikuwa imefanya upekuzi kwenye nyumba kadhaa katika kitongoji cha mji huo ambapo inadhaniwa kwamba wapiganaji wa jihadi wamekuwa wakijificha na ndipo wanamgambo hao walipowafyatulia risasi polisi. Hata hivyo mapigano makali bado yalikuwa yakiendelea na kwamba polisi ina hofu kuwa wanamgambo...

Like
212
0
Monday, 26 October 2015
TETEMEKO KUBWA LA ARDHI LAIKUMBA AFGHANISTAN
Global News

TETEMEKO kubwa la Ardhi limeyakumba maeneo mengi ya kaskazini mwa Afghanistan, na kutikisa ardhi maeneo ya Pakistan na India. Idara ya Utafiti imesema kuwa Kitovu cha tetemeko hilo lenye nguvu limetikisa katika maeneo mengi yenye milima mingi ya Hindu Kush, kilomita 45 kusini magharibi mwa Jarm. Hata hivyo Maafisa wamesema tetemeko hilo lilitokea kutoka kilomita 212 ndani ya ardhi huku Nguvu za tetemeko hilo awali zimedaiwa kuwa 7.7 lakini baadaye kipimo...

Like
207
0
Monday, 26 October 2015