SHIRIKA la kibinadamu la Human Rights Watch limewalaumu wapiganaji wa kikurdi kutoka kaskazini mashariki Mashariki mwa Syria kwa kufanya kampeni ya makusudi kuwatimua katika makazi yao watu wenye asili ya Kiarabu kutoka maeneo ambayo wameyakomboa. Taarifa zinaeleza kuwa tatizo hilo linalingana na lililotokea awali katika eneo la Kaskazini mwa Iraq, ambapo Wakurdi wa Syria waliojitokeza kama wafuasi waaminifu zaidi kwa muungano wa wanajeshi wanaoongozwa na Marekani na kushambulia eneo hilo. Hata hivyo imebainika kuwa Wamarekani waliwasaidia...
WAZIRI mkuu wa Uturuki Ahmet Davotuglo amesema kuwa wachunguzi wa nchi hiyo wanakaribia kumtambua mmoja kati ya washambuliaji wa kujitoa muhanga wa mashambulizi ya mabomu dhidi ya maandamano ya amani katika kituo cha treni yaliyowaua watu wasiopungua 97 mjini Ankara. Davutoglu amesema kwamba kundi la dola la Kiislamu limepewa kipaumbele katika uchunguzi huo kwa kushukiwa kuhusika kwa kiasi kikubwa. Wakati hayo yakijiri katibu mkuu wa Jumuiya ya kujihami ya NATO Jens Stoltenberg ameihimiza Uturuki iwe makini katika njia inazozitumia...
WAZIRI wa Mazingira wa Zimbabwe Oppah Muchinguri amesema kuwa daktari wa meno ambaye alisababisha hali ya taharuki baada ya kumuua Simba mmoja mashuhuri nchini Zimbabwe hatashtakiwa kwa kuwa alikuwa na kibali cha kuwinda. Daktari huyo anayefahamika kwa jina la Walter Palmer alikubali kumuua Simba aitwaye Cecil lakini alikana kutekeleza shughuli za uwindaji kinyume cha sheria. Awali Waziri huyo alitaka Palmer afunguliwe mashtaka ya kumuua mnyama huyo lakini baadaye ilibainika kuwa hakuna sheria iliyovujwa katika mauaji ya Simba...
POLISI wa Israel wamesema wamempiga risasi na kumuua mwanamume mmoja wa Kiarabu mapema leo aliyejaribu kumchoma kisu afisa mwenzao huko Jerusalem Mashariki. Polisi wamemueleza mshambuliaji huyo wa Kipalestina kuwa ni gaidi lakini hawakutoa maelezo zaidi kuhusu utambulisho wake. Msemaji wa polisi amesema Mpalestina huyo ambaye ni wa 24 kuuawa tangu mwanzoni mwa mwezi huu, alimshambulia afisa wa Israel aliyejaribu...
MAWAZIRI wa Mambo ya nje wa nchi za Umoja wa Ulaya wanakutana leo Luxembourg kujadili njia za kuutafutia ufumbuzi mzozo nchini Syria. Mkutano huo unafanyika huku kukiwa na wasiwasi kuhusu hatua ya Urusi kujiingiza kijeshi katika mzozo huo na mustakabali wa rais wa Syria Bashar al Assad ukiwa haujulikani. Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, mzozo wa Syria umesababisha watu wapatao 250,000 kuuawa tangu mwaka...
MAELFU ya Watu wamekusanyika mjini Ankara nchini Uturuki kuomboleza vifo vya takriban watu 95 waliouawa kwa milipuko miwili ya mabomu. Watu wanaounga mkono Chama cha Kikurdi ambao walikuwepo kwenye mkutano katika eneo ambalo mabomu yalilipuka wanaamini kuwa idadi ya kweli ya waliopoteza maisha ni Watu 128. Vyanzo vya ulinzi vinasema kuwa vinalishuku kundi la wanamgambo wa IS kuhusika kwenye shambulio hilo huku Serikali ikikanusha vikali madai kuwa imehusika katika mashambulizi...
RAIS wa Urusi Vladimir Putin ametetea uamuzi wa nchi yake wa kuchukua hatua za kijeshi nchini Syria, kwa kusema kuwa lengo lake ni kusaidia utawala halali wa Rais wa Syria Bashar al-Assad. Awali rais Putin aliiambia runinga ya taifa ya Urusi kwamba Moscow pia inataka kuunda mazingira yatakayowezesha kuwepo kwa maafikiano ya kisiasa nchini humo. Hata hivyo amekanusha madai kwamba mashambulio ya ngani ya Urusi yanalenga makundi ya upinzani badala ya yale ya wapiganaji wa Islamic...
WIZARA ya ulinzi ya Urusi imekanusha madai yaliyotolewa na afisa mmoja wa Marekani kuwa makombora manne ya Urusi yaliyofyatuliwa katika Bahari ya Caspian kuelekea Syria yalianguka nchini Iran. Msemaji wa wizara hiyo Jenerali Igor Konashenkov amesema makombora yote yaliyofyatuliwa yalipiga katika maeneo yaliyolengwa. Afisa wa Marekani, ambaye jina lake halikujulikana, amesema makombora hayo yalianguka nchini Iran siku ya Jumatano lakini hakutoa maelezo yoyote kuhusu mahali yalikoanguka au ikiwa yalisababisha uharibifu wowote....
UFARANSA imeanzisha mashambulizi mapya ya anga usiku wa kuamkia leo nchini Syria dhidi ya kambi ya mafunzo ya kundi la Dola la Kiislamu-IS na mashambulizi zaidi yatafuata. Waziri wa Ulinzi wa Ufaransa, Jean-Yves Le Drian, amesema leo kuwa nchi hiyo imewashambulia wapiganaji hao, na haitakuwa mara ya mwisho. Wakati huo huo, taarifa zinaeleza kuwa mshauri wa kijeshi wa Iran, Jenerali Hussein Hamdani, ameuawa na wanamgambo wa IS nchini...
UTAFITI mpya umeonya kuwa sigara ina uwezo wa kuua kijana mmoja kati ya vijana watatu nchini China. Hali hiyo itatokea kama hapatakuwa na hatua yeyote itakayofanyika itakayowafanya waache tabia hiyo. Utafiti huo, uliochapishwa katika jarida la Lancet linalohusiana na masuala ya tiba, unasema kuwa China inakabiliwa na ongezeka kubwa la vifo vya mapema kwa kuwa theluthi mbili ya vijana nchini humo huanza kuvuta sigara wakiwa chini ya miaka...
WASIWASI umezuka katika mji wa Calabar, kusini mwa Nigeria kutokana na mtu mmoja kufariki baada ya kuonyesha dalili zinazofanana na zile za ugonjwa wa Ebola. Shirika la usimamizi wa mambo ya dharura nchini humo limesema kuwa watu kumi wamewekwa karantini baada ya kugusana na mtu aliyeonekana kuwa na dalili za ugonjwa huo. Shirika la afya duniani WHO lilitoa taarifa yake siku ya Jumatano kuwa nchi tatu zilizokuwa zimeathiriwa kwa kiasi kikubwa na ugonjwa huo ambazo ni Guinea, Sierra Leone na...