Global News

MUDA WAONGEZWA KUYAFIKIA MAKUBALIANO YA MPANGO WA NYUKLIA IRAN
Global News

IRAN na nchi zenye nguvu zaidi duniani zimeongeza muda wa kufikia makubaliano kamili kuhusu mpango wa kinyuklia wa Iran hadi tarehe saba mwezi huu baada ya kushindwa kufikia makubaliano hayo hapo jana. Waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergei Lavrov amesema baada ya miaka miwili ya mazungumzo kati ya nchi zinazohusika, anaamini makubaliano yako karibu yatafikiwa. Rais wa Marekani Barack Obama hata hivyo amesisitiza nchi yake haitasita kujiondoa kutoka mazungumzo hayo ya kinyuklia iwapo masharti yanayotakiwa kutimizwa hayatakuwa ya...

Like
208
0
Wednesday, 01 July 2015
BAN KI MOON: MZOZO WA SYRIA ULIMWENGU UNAPASWA KUONA AIBU
Global News

KATIBU MKUU wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon amesema ulimwengu unapaswa kuona aibu kuwa miaka mitatu baada ya nchi zenye nguvu zaidi duniani kuidhinisha azimio mjini Geneva la kuleta amani Syria, lakini bado watu wa nchi hiyo wanataabika kwa kiwango kikubwa na mzozo huo  na huenda Taifa hilo likasambaratika. Ki Moon  amesema zaidi ya watu 220,000 wameuawa Syria katika vita ambavyo vimedumu kwa miaka mitano na zaidi ya nusu ya idadi ya raia wa nchi hiyo wamelazimika kuyatoroka makaazi...

Like
236
0
Wednesday, 01 July 2015
IDADI YA WALIOFARIKI GHANA YAFIKIA 175
Global News

TAKRIBAN watu 175 wamefariki kufiakia sasa kufuatia moto uliotokea katika kituo kimoja cha mafuta mji mkuu wa Ghana –Accra. Moto huo uliozuka siku ya jumatano usiku ulianza wakati wakazi wa mji huo walipokuwa wakikabiliana na siku mbili za mvua kubwa ambayo imewaacha raia wengi bila makazi. Taarifa zinasema kuwa mafuriko huenda yalisababisha moto ambao ulitokea jana wakati mamia ya watu walipokuwa wamejihifadhi katika kituo hicho cha mafuta kutokana na mvua kubwa...

Like
226
0
Friday, 05 June 2015
CHINA YAIKOSOA MAREKANI JUU YA TUHUMA ZA KUHUSIKA NA UDUKUZI
Global News

CHINA imeitaja Marekani kuwa imekosa kuwajibika kwa kudai kuwa wadukuzi wa china ndio waliosababisha udukuzi wa taarifa za ofisi ya serikali ya Marekani. Wizara ya mambo ya nje ya china imesema ni vigumu kujua chanzo cha udukuzi huo na kwamba dhana isiyo na ushahidi wowote wa kisayansi haitasaidia. Shirika la ujasusi la –FBI- nchini Marekani linachunguza namna wadukuzi wa komputa walivyoweza kuingilia taarifa hizo binafsi za wafanyakazi wa serikali wapatao milioni nne...

Like
278
0
Friday, 05 June 2015
MAREKANI: TAARIFA ZA WAFANYAKAZI ZADUKULIWA
Global News

SERIKALI ya marekani imekumbwa na udukuzi mtandao wa komputa ambapo taarifa binafsi za mamilioini ya wafanyakazi wa serikali zimeingiliwa. Ofisi ya Utumishi ya nchini hiyo inasema karibu ya watu milioni nne ambao wanafanya kazi au waliwahi kufanya kazi wameathirika na udakuzi huo. Taarifa zote za udakuzi huo na idadi ya watu waliohusika bado haijafahamika lakini Afisa mmoja anasema kila idara ya serikali itakuwa imeathirika kwa kiasi kikubwa....

Like
307
0
Friday, 05 June 2015
GHANA YATANGAZA SIKU TATU ZA MAOMBOLEZO KUFUATIA VIFO VYA WATU 150
Global News

GHANA imetangaza siku tatu za maombolezo ya kitaifa kufuatia vifo vya watu mia na hamsini vilivyotokana na mafuriko na mlipuko kwenye kituo kimoja cha mafuta.   Mlipuko huo ulitokea hapo jana wakati mamia ya watu walipokuwa wamejihifadhi katika kituo hicho cha mafuta kutokana na mvua kubwa zinazonyesha.   Rais wa Ghana,John Mahama amesema janga kama hilo halitajirudia tena. Rais Mahama amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika mji mkuu ,Accra alipotembelea eneo la tukio. baadhi ya picha za...

Like
386
0
Friday, 05 June 2015
WANAJESHI WATANO WAUAWA KUTOKANA NA MAPIGANO UKRAINE
Global News

WANAJESHI watano wa Ukraine wameuawa katika mapigano karibu na  mji unaoshikiliwa na serikali wa Maryinka, ambako waasi wanaoipendelea Urusi wakijaribu kusonga mbele. Msemaji wa Ikulu mjini Kiev Yuri Biryukov, amesema kuwa katika ukurasa wake wa Faceboock, kwamba  raia 39 wa Ukraine wamejeruhiwa katika mapigano hayo. wizara ya ulinzi ya Ukraine imesema kwamba  waasi wanaotaka kujitenga, wakitumia vifaru  na mizinga walijaribu kuviteka vituo vya serikali karibu na Maryinka, mashariki mwa mji unaoshikiliwa na waasi wa Donetsk, ikiwa ni...

Like
235
0
Thursday, 04 June 2015
VIONGOZI WALIOTANGAZA NIA YA KUWANIA URAIS WATAJWA KUSHINDWA KUBAINISHA MIKAKATI YA UTU NA NGUVU YA MWANAMKE
Global News

LICHA ya baadhi ya Viongozi wa siasa nchini kutangaza nia za kutaka kugombea nafasi ya urais kupitia vyama vyao, Viongozi hao hawajaweza kubainisha  mikakati ya kuwezesha utu  na nguvu ya mwanamke wa Tanzania kama sehemu muhimu ya mipango yao. Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa mtandao wa wanawake na katiba MARRY RUSIMBI wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya namna watangaza nia wanavyopaswa kupambanua kiundani na changamoto mbali mbali zinazowakabili wanawake wakitanzania. Naye Mwenyekiti...

Like
422
0
Thursday, 04 June 2015
MAREKANI YAKIRI KUTUMA KIMETA ZAIDI
Global News

MAOFISA wa ulinzi nchini marekani wamekiri kuwa maabara kadhaa nchini humo zilipokea kimakosa sampuli hai za vidudu hatari vya kimeta zaidi ya mara mbili ya matarajio ya awali. Pentagon imesema vifaa hamsini na moja katika majimbo kumi na saba nchini Marekani, pamoja na maabara zilizopo nchini Canada, Australia na Korea kusini walitumiwa sampuli hizo kutoka maabara ya jeshi la marekani. Hata hivyo imeelezwa kuwa usafirishaji wa vidudu hivyo ulianza miongo kadhaa iliiyopita na kuendelea mpaka wiki iliyopita lakini hadi sasa...

Like
226
0
Thursday, 04 June 2015
ARGENTINA WAANDAMANA KUTETEA WANAWAKE
Global News

MAELFU ya watu wameandamana katika mji mkuu wa Argentine – Buenos Aires katika harakati za kupinga mateso dhidi ya mwanamke . Maandamano hayo yamekuja kufuatia matukio ya mara kwa mara ya visa vya mauaji kwa wanawake yaliyoshtua Taifa hilo yakiwemo ya mwalimu wa chekechea kwa kukatwa koo na mumewe mbele ya darasa lake. Vyama vya wafanyakazi kwa kushirikiana na vyama vya kisiasa na kanisa katoliki wameunga mkono maandamano hayo ambapo kwa sasa tayari Argentina imepitisha sheria dhidi ya unyanyasaji wa...

Like
197
0
Thursday, 04 June 2015
BOKO HARAM YATOA MKANDA MPYA WA VIDEO
Global News

WANAMGAMBO wa kiislamu nchini Nigeria wametoa picha mpya za video lakini Kiongozi wa Boko Haram ambaye huwa anaonekana kwenye video zao, ABUBAKAR SHEKAU hakuonekana kwenye picha hizo. Imeelezwa kuwa kutoonekana kwa Shekau kwenye Video hiyo kumeleta hali ya wasiwasi kuhusu kuwepo kwa mgawanyiko ndani ya kundi hilo. Hata hivyo katika picha ya video ya dakika 10imeonesha msemaji huyo anakanusha taarifa zilizotolewa na Jeshi la Serikali kuwa linadhibiti miji yote kutoka mikononi mwa...

Like
216
0
Wednesday, 03 June 2015