Global News

IRAN: MAZUNGUMZO YA MPANGO WA NYUKLIA YAENDELEA USWISI
Global News

MAZUNGUMZO kuhusu mpango tata wa Iran wa Nyuklia yameendelea nchini Uswisi, kwa kuwasili Mawaziri wa Mambo ya Nje kutoka Mataifa Sita yenye nguvu duniani. Kiongozi wa mazungumzo wa Iran ABBAS ARAQCHI amesema makubaliano yanawezekana lakini mazungumzo yako katika hatua ngumu na bado kuna mambo ya kutatua. Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza PHILIP HAMMOND pia amesema anaamini makubaliano yatafikiwa lakini yatatakiwa kuhakikisha Iran haipati uwezo wa kutengeneza bomu la nyuklia....

Like
226
0
Monday, 30 March 2015
BARAZA LA USALAMA LA UMOJA WA MATAIFA LIMEPITISHA AZIMIO KUVIONGEZEA MUDA VIKOSI VYA USALAMA DRC
Global News

BARAZA la Usalama la Umoja wa Mataifa limepitisha azimio la kuviongezea muda wa mwaka mmoja wa ziada vikosi vya kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, MONUSCO. Hata hivyo idadi ya vikosi vya Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo itapunguzwa kwa kiwango cha asilimia 10 sawa na wanajeshi 2,000. Zaidi ya makundi thelathi ya watu wenye silaha bado yanaendelea kuhatarisha usalama wa raia hususan mashariki mwa nchi hiyo pamoja na hali ya sintofahamu ambayo imekua ikiripotiwa...

Like
292
0
Friday, 27 March 2015
NIGERIA: UTATA WATAWALA UCHAGUZI MKUU UNAOTARAJIWA KUFANYIKA KESHO
Global News

WANANCHI wa Nigeria kesho wanatarajiwa kujitokeza katika uchaguzi mkuu wa nchi hiyo. Hata hivyo kumekuwa na vuta ni kuvute huku kukiwa na Taarifa ya Mtendaji Mkuu wa Kampuni inayosambaza mashine za kusoma vitambulisho vya elekroniki vya wapiga kura kukamatwa na maafisa usalama wa nchi hiyo. Chama kinachotawala nchini humo cha PDP kimesema kwamba mtendaji huyo Musa Sani anahusishwa na chama kikuu cha upinzani nchini humo cha APC ambaye anadhaniwa kutaka kuvuruga uchaguzi...

Like
266
0
Friday, 27 March 2015
UK YAPANGA KUTOA MAFUNZO YA KIJESHI KWA WAASI SYRIA
Global News

KATIBU wa ulinzi nchini Uingereza Michael Fallon, amesema Nchi hiyo  itatoa mafunzo ya kijeshi kwa waasi wa Syria wanaokabiliana na serikali ya rais Bashar Al Asaad. Karibia wakufunzi 75 pamoja na wafanyakazi wengine wa makao makuu watasaidia katika matumizi ya silaha ndogo ndogo,mbinu za kijeshi pamoja na zile za matibabu. Mafunzo hayo yatafanyika nchini Uturuki ikiwa ni miongoni mwa mipango ya serikali ya Marekani.  ...

Like
274
0
Thursday, 26 March 2015
IRAQ: NDEGE ZA KIJESHI ZA MAREKANI ZIMEANZA KUTEKELEZA MASHAMBULIZI TIKRIT
Global News

NDEGE za kijeshi za Marekani zimeanza kutekeleza mashambulizi makali, katika maeneo yenye wanamgambo wa Islamic State, katika mji wa Tikrit uliotekwa na waasi hao. Vifaru vya jeshi la Iraq pia vimerejesha mashambulizi makali ya ardhini katika mji huo. Kiongozi mmoja mkuu wa Marekani, anasema kwamba mashambulizi ya angani kwa maeneo yanayolengwa, yanafuatia ruhusa kutoka kwa serikali ya...

Like
343
0
Thursday, 26 March 2015
SAUD ARABIA YAANZA OPERESHENI ZA KIJESHI NCHINI YEMEN
Global News

SAUD ARABIA imeanza operesheni zake za kijeshi nchini Yemen, ikiwa ni kujibu ombi la Rais wa nchi hiyo ABD RABBUH MANSOUR HADI. Balozi wa Saudi Arabia Nchini Marekani amesema kuwa, taifa lake na washirika wao wa ghuba wanatumia mashambulizi ya angani katika harakati za kuunga mkono serikali halali ya Yemen, ili isichukuliwe na kundi wa waasi la Houthi. Awali duru zasema kuwa wapiganaji wa Houthi walikuwa wakikaribia kuutwa mji wa Aden, ulioko kusini mwa Nchi hiyo.  ...

Like
231
0
Thursday, 26 March 2015
SINGAPORE: MAELFU WAJITOKEZA KUTOA HESHIMA ZA MWISHO KWA LEE KUAN YEW
Global News

MAELFU ya watu wamepanga foleni nje ya majengo ya bunge nchini Singapore, ili kutoa heshima zao za mwisho kwa aliyekuwa waziri mkuu wa kwanza wa nchi hiyo Lee Kuan Yew. Marehemu Lee Kuan Yew aliyefariki siku ya jumatatu akiwa na umri wa miaka 91 atazikwa siku ya jumapili. Mashirika na kampuni nyingi za kibiashara zimewapa wafanyakazi wao ruhusa ya kwenda kumuaga marehemu Lee kwa heshima na...

Like
360
0
Wednesday, 25 March 2015
KIFAA CHA KUNASA SAUTI KWENYE NDEGE UJERUMANI CHAHARIBIKA
Global News

WAZIRI wa maswala ya ndani nchini Ufaransa, Bernard Cazeneuve, amesema kuwa kifaa cha kunasa sauti kwenye ndege kilichopatikana hapo jana Jumanne baada ya kuanguka kwa  ndege ya Ujerumani katika milima ya Alps kimeharibika. Hata hivyo amesema kuwa kifaa hicho bado kitatoa taarifa kwa watalamu wanaojaribu kubaini kilicho sababisha kuanguka kwa ndege hiyo, ambayo iliwauwa abiria wote 150 na wahudumu waliokuwemo kwenye ndege hiyo. Shughuli za utafutaji wa ndege hiyo zimeendelea huku helikopta zinaonekana zikipaa katika maeneo hayo na maafisa wa...

Like
290
0
Wednesday, 25 March 2015
ANGELA MERKEL ATARAJIA KWENDA MAHALI ILIPOANGUKA NDEGE YA SHIRIKA LA UJERUMANI
Global News

KANSELA wa Ujerumani ANGELA MERKEL anatarajia kwenda mahali ilipoanguka Ndege ya Shirika la Ujerumani, GermanWings katika Milima ya Alps nchini Ufaransa. GermanWings ambayo ni tawi la bei nafuu la Shirika la Ndege la Ujerumani, Lufthansa imesema, ndege yake iliyopata ajali ilikuwa ikitoka katika mji wa Barcelona nchini Uhispania, ikielekea Duesseldorf Ujerumani, ikiwa na watu Zaidi ya 100. Rais wa Ufaransa FRANCOIS HOLLANDE amesema anaamini hakuna mtu aliyenusurika katika ajali...

Like
269
0
Wednesday, 25 March 2015
YEMEN YAOMBA MSAADA WA KIJESHI KUPAMBANA NA WAPIGANAJI WA KIHOUTHI
Global News

WAZIRI wa Mambo ya nchi za Nje wa Yemen RIYADH YASEEN amezitolea wito nchi ya Ghuba ya Uarabu kuingilia Kijeshi katika nchi yake, kuwazuia wapiganaji wa Kihouthi ambao wanaipinga Serikali ya Rais ABDU RABBU MANSOUR HADI, ili wasiendeleei kuyateka maeneo zaidi ya nchi. Katika mahojiano na Gazeti la Kiarabu la Al-Sharq al-awsat, Waziri YASEEN amesema wapiganaji hao wameteka Miji na Viwanja vya ndege, na kumtia kizuizini yoyote wanayemtaka. Amesema wameelezea hofu yao kwa Baraza la Ushirikiano wa nchi za Ghuba,...

Like
304
0
Tuesday, 24 March 2015
NDEGE YA UJERUMANI YAANGUKA NCHINI UFARANSA
Global News

NDEGE ya abiria inayomilikiwa na shirika la ndege la Germanwing Airbus A320 Imeanguka katika Milima ya Alps nchini Ufaransa. Ndege hiyo ilikuwa imebeba abiria 142 na Wahudumu 6 ikitoka Barcelona Uhispania kuelekea Duesseldorf. Ndege hiyo inayomilikiwa na shirika la ndege la Ujerumani Lufthansa chini ya nembo Germanwings imeripotiwa kuanguka karibu na mji wa...

Like
309
0
Tuesday, 24 March 2015