WAZIRI wa Mambo ya Nje wa Ujerumani, FRANK-WALTER STEINMEIER amesema pande zinazohusika katika mzozo wa Ukraine, lazima ziepukane na hatua zozote zinazoweza kupelekea mzozo mpya kusambaa zaidi nchini humo. Aidha, STEINMEIER ametoa wito wa kuendelea kwa mchakato wa mpango wa amani wa Minsk, ambao umesainiwa mwaka uliopita, katika juhudi za kusimamisha mapigano Mashariki mwa Ukraine. STEINMEIER na maafisa wengine waandamizi wanaohusika na mzozo wa Ukraine, wanatarajiwa kukutana mjini Paris, Ufaransa kujadiliana kuhusu hatua za kusitisha mapigano...
KANSELA wa Ujerumani, ANGELA MERKEL na Waziri Mkuu wa Ugiriki, ALEXIS TSIPRAS wamesisitiza nia yao ya kuondoa mvutano uliopo kati ya serikali zao. Hayo wameyaeleza katika mkutano wao na Waandishi wa Habari uliofanyika mjini Berlin. TSIPRAS amezuru rasmi Ujerumani kwa mara ya kwanza tangu aingie madarakani mwezi Januari mwaka...
KANSELA wa Ujerumani Angela Merkel anakutana leo na waziri mkuu wa Ugiriki Alexis Tsipras , ambaye amemlaumu kansela kwa kusisitiza kuhusu hatua ya kubana matumizi kwa nchi yake ambayo imesababisha mzozo wa kiutu wa umasikini pamoja na ukosefu mkubwa wa ajira. Viongozi hao wa Ugiriki na Ujerumani wanakutana mjini Berlin baada ya wiki kadhaa za hali ya wasi wasi kuhusiana na matatizo ya upatikanaji wa fedha kwa Ugiriki , hisia za baada ya ...
KIONGOZI mashuhuri wa Singapore, anayejulikama kama baba wa taifa hilo , Lee Kuan Yew amefariki dunia. Serikali ya nchi hiyo imetangaza hii leo kwamba Lee mwenye umri wa miaka 91 alilazwa hospitalini mapema Februari akiwa anaugua ugonjwa wa kichomi, na amekuwa akipumua kwa kutumia mashine katika kitengo cha wagonjwa mahututi tangu wakati huo. Rais wa Marekani Barack Obama ametuma salamu zake za rambi rambi na kumuelezea Lee kuwa mtu aliyeona ...
Wazazi huko india wameparamia ukuta kupitisha majibu ya mitihani kwa watoto wao Watoto katika shule ya Bihar wilaya ya Hajipur wamekuwa wakipata msaada wa kupitishiwa majibu na wazazi wanapokuwa kwenye vyumba vya mitihani. Kwenye mkanda wa video uliorekodiwa na chanzo kimoja cha habari za ndani nchini humo kinaonyesha umati wa wazazi wakiparamia kuta za ghorofa kuwapitishia wanafunzi majibu ya mtihani kwa kutumia madirisha ya jengo hilo Zaidi ya wanafunzi milioni 1.4 wapo katika mitihani ambayo inarajiwa kumalizika march 24 nchini...
MASHIRIKA ya utoaji misaada yanaonya hali bado ni tete, mwaka mmoja tangu ugonjwa wa maradhi ya Ebola kulipuka Magharibi mwa Afrika. Shirika la Madaktari wasiokuwa na Mipaka- MSF, limesema kuwa mlipuko huo ambao umewauwa zaidi ya watu Elfu Kumi. Shirika limesema namna Mashirika ya Matibabu na watoaji Misaada ya Dharura, yanavyoendesha shughuli za kuwaokoa watu kuwa ni taratibu mno....
VIONGOZI wa Taifa na Serikali wa nchi za Umoja wa Ulaya wamekubaliana kurefusha vikwazo vya Kiuchumi dhidi ya Urusi hadi Desemba mwaka huu. Katika mkutano wao wa kilele mjini Brussels viongozi hao wa Mataifa 28 wamefungamanisha vikwazo hivyo na kuheshimu makubaliano ya kuweka chini silaha na kurejesha amani Mashariki mwa Ukraine. Hata hivyo Viongozi hao wamezidi kumshinikiza Rais wa Urus VLADIMIR PUTIN, atumie ushawishi wake kuwatanabahisha Waasi wanaoelemea upande wa Urusi ili kumaliza mzozo wa Mashariki mwa...
MSEMAJI wa Serikali ya Marekani, JOSH EARNEST, amesema Waziri Mkuu wa Israel BENJAMIN NETANYAHU, amekiuka dhamira yake ya awali ya kuundwa kwa Mataifa mawili kama suluhu ya mgogoro wa Israel na Palestina mwanzoni mwa wiki hii. Matamshi ya waziri mkuu huyo wa Israel ya kutotaka kuwepo kwa taifa la Palestina yanaonekana na wengi kama ndio yaliyomsaidia kushinda katika uchaguzi uliofanyika siku March 17 mwaka huu. Taarifa zinasema kuwa NETANYAHU amekiambia Kituo cha Televisheni cha Marekani, MSNBC, kwamba bado anabaki na...
MARUBANI wa Shirika la ndege la Ujerumani Lufthansa wametangaza kwamba wataendelea na mgomo wao leo mgomo ambao tayari umewaathiri maelfu ya abiria na kushuhudia kufutwa kwa mamia ya safari kutokana na mzozo juu ya mpango wa malipo ya kustaafu. Msemaji wa Shirika la ndege la Lufthansa amesema nusu ya safari 1,400 za shirika hilo za ndani na zile za Ulaya kuingia na kuondoka Frankfurt na Munich zimefutwa hapo na kuathiri abiria 80,000. Mgomo huo wa siku moja awali ulikuwa umepangwa...
RAIS BARRACK OBAMA ametoa ujumbe katika kanda ya video kwa viongozi na raia wa Iran akisema kwamba hapajakuwa na wakati muafaka zaidi katika miongo kadha iliyopita kwa Marekani na Iran kutafuta uhusiano mpya. Katika ujumbe wa kusherehekea mwaka mpya wa Iran, OBAMA amesema Mataifa hayo mawili yana nafasi ya kihistoria ambayo haipaswi kupotea. Amesema mazungumzo kuhusu mpango wa nuklia wa Iran yamepiga hatua lakini ameonya kuwa kuna watu wanaopinga mazungumzo juu ya mpango huo kwa nchi zote mbili yaani Marekani...
CHINA na Japan wanafanya mkutano wa kwanza wa kiwango cha juu wa usalama katika muda wa miaka minne. Mkutano huo unaofanyika Tokyo unajumuisha maafisa kutoka wizara za mambo ya nje na ulinzi ambapo mazungumzo hayo yalisitishwa mnamo mwaka 2011 kutokana na hofu kuhusu visiwa vinavyozozaniwa Mashariki mwa bahari ya China. Pande zote zimesisistiza umuhimu wa mazungumzo ya kweli kudumisha amani....