RAIS wa Tunisia, Beji Caib Essebsi, amesema nchi yake imo vitani na ugaidi baada ya wanaume waliojihami kwa bunduki kuwaua watalii wa kigeni wapatao 17 na raia wawili katika shambulio lililotokea kwenye makazi mjini Tunis. Kiongozi huyo amesema nchi yake itakabiliana vikali na alichokitaja kama makundi madogo ya kishetani. Washambuliaji hao waliwapiga risasi wageni kutoka Japan, Colombia, Australia, Italia na Uhispania kabla ya kuuawa na maafisa wa...
WAJUMBE wa Mashirika ya Kiraia wa vijiji vya Tama na Itala Kusini mwa tarafa ya Lubero Jimboni Kivu Kaskazini, wametishwa na kundi la Waasi wa Kihutu kutoka Rwanda-FDLR wanaoongozwa na Kanali KIZITO. Vitisho hivyo vimekuja kutokana na uchapishaji wa Ripoti ya Mashirika ya Kiraia katika Sekta hiyo. Baadhi ya Wanachama wa Vyama vya Kiraia katika Vijiji vya Tama na Itala wamesema, raia katika maeneo hayo wanaishi katika hali ya maficho kwa siku tano sasa kulingana na unyanyasaji kutoka waasi wanaoishi...
PAKISTAN imewanyonga wafungwa wengine tisa wauaji na kuifikisha idadi ya walionyongwa katika kipindi cha siku mbili zilizopita kufikia 21 nakufikisha idadi ya watu 48 walio nyongwa katika mkoa wa Punjab tangu Pakistan iliporejesha adhabu ya kifo mwezi Desemba mwaka jana. Hatua hiyo imelaaniwa na Umoja wa Ulaya ambao unapinga adhabu ya kifo na katika taarifa yake umetoa wito wa kufutwa adhabu hiyo kote duniani. Katika taarifa yake Human Rights Watch imesema walionyongwa leo ni pamoja na Mohammad Afzal ambaye wakati...
CHAMA cha Likud cha Waziri Mkuu BENJAMIN NETANYAHU kimepata ushindi wa kushangaza katika uchaguzi mkuu wa Israel. Matokeo ya awali yameonyesha kuwa Chama cha Mrengo wa kushoto cha Zionist Union kupata Mshtuko. Kura nyingi zikiwa zimehesabiwa, Likud kinaonekana kupata Viti 29 katika Bunge lenye viti 120, huku chama cha Zionist Union kikiwa na Viti 24. ...
KIONGOZI Mkuu wa familia ya kifalme nchini Saudia ameonya kwamba makubaliano ya mpango wa nyuklia wa Iran huenda yakasababisha nchi zingine katika eneo hilo la ghuba kuanza kurutubisha madini ya atomiki. Mwanamfalme Turki al-Faisal amesema kwamba Saudi Arabia pia itatafuta haki sawa kama yatakavyofanya mataifa mengine. Mataifa sita yenye nguvu duniani yanayojadiliana na Iran yanadai kwamba inatosha kudhibiti shughuli za nyuklia za Iran ili isiweze kuunda silaha za...
WANAWAKE na watoto wachanga zaidi ya 45 wameuawa katika shambulizi lililotekelezwa katika kijiji kimoja huko Egba katika jimbo la Benue Nigeria. Maafisa wa usalama katika jimbo hilo la kati wanasema kuwa wavamizi walishambulia kijiji hicho alfajiri kuamkia leo . Hata hivyo,mwanasiasa mmoja kutoka eneo hilo Audu Sule ameiambia BBC kuwa zaidi ya watu 81wamauawa na watu waliokuwa wamejihami kwa bunduki aina ya...
ZAIDI ya Watu Milioni moja kutoka nchini Brazil wameandamana dhidi ya rais wa nchi hiyo DILMA ROUSSEFF, huku wengi wao wakitaka Rais huyo afunguliwe Mashtaka ya Ufisadi uliofanyika katika Shirika la Mafuta La serikali, Petrobras. Maandamano kama hayo yamefanyika katika miji mingi ya Brazil ikiwemo Mji Mkuu wa nchi hiyo Brasilia. Maandamano makubwa kabisa yamefanyika katika mji wa Sao Paulo ambalo ni eneo la upinzani waliokuwa wakipita mitaani. ...
TATIZO la Uhaba wa damu nchini limeendelea kuwa tishio kwa wagonjwa wanaohitaji damu kwenye vituo vya huduma nchini na kubababisha maisha yao kuwa hatarini. Takwimu zinaonyesha mahitaji ya Damu kwa mwaka ni Chupa 450,000 lakini makusanyo kwa mwaka ni Chupa 150,000,hali inayosababisha baadhi ya wagonjwa wanaohitaji damu kukosa huduma hiyo. Kutokana nma Hali hiyo,Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya-NHIF kwa kushirikiana na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,Kupitia Mpango wa Damu Salama,Inaendesha Kampeni ya Uchangiaji damu Katika mikoa...
IDADI ya watu waliofariki kutokana na maradhi ya Ebola katika nchi tatu za Afrika magharibi zilizoathirika zaidi na maradhi yao, Guinea, Sierra Leone na Liberia imezidi watu 10,000. Hayo ni kwa mujibu wa ripoti ya shirika la afya la Umoja wa mataifa WHO iliyochapishwa mjini Geneva. Hata hivyo shirika hilo limesema maradhi hayo yamepungua hivi sasa na kuna matukio machache mapya ya Ebola yaliyosajiliwa....
WIZARA ya ulinzi nchini Korea Kusini inasema kuwa Korea Kaskazini imefyatua makombora mawili ya masafa marefu kwenda baharini eneo la pwani ya mashariki. Tukio hilo limeripotiwa wakati kukiwa na msukosuko katika rasi hiyo huku korea kusini na marekani wakiendelea na mazoezi ya kijeshi ya kila mwaka. Korea na marekani wanasema kuwa mazoezi hayo ni ya kujilinda lakini korea kaskazini inayaona kuwa ya kutaka...
KATIKA mapigano makubwa na makali yanaondelea dhidi ya wanamgombo wa Islamic State, majeshi ya Iraq na yale Shia yamezidi kupata ushindi na kuurudisha tena mji wa Tikrit. Majeshi ya nchi hiyo yamesema imewachukua usiku mzima kupambana katika eneo la kaskazini, mashariki na magharibi kando ya mji, kuingian katikati mwa mji. Kwa mujibu wa ripoti moja, kwa sasa wapiganaji mia moja na hamsini wa kundi la Islamic State wameendelea kuwepo katika mji huo wa Tikrit, ambao ni makao makuu ya jimbo...