Global News

MAREKANI YAUNGA MKONO UUNDWAJI WA JESHI LA PAMOJA KUPAMBANA NA BOKO HARAM
Global News

MAREKANI imeunga mkono uundwaji wa jeshi la pamoja lenye askari hadi 10,000 katika eneo la Afrika Magharibi kwa lengo la kukabiliana na kundi la wanamgambo wenye itikadi kali la Kiislamu Boko Haram. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Wizara ya Ulinzi ya Marekani Mataifa 54 ya Umoja wa Afrika yameidhinisha jeshi hilo na kuuomba Umoja wa Mataifa kuridhia utekelezeji wake kwa dharura baada ya mashambilizi ya kundi hilo katika maeneo ya kaskazini mwa Nigeria na mataifa jirani ya Chad, Niger,...

Like
231
0
Thursday, 12 March 2015
MAOFISA WA POLISI WASHAMBULIWA FERGUSON
Global News

MAAFISA Polisi wawili wameshambuliwa kwa risasi mjini Ferguson, mji ambao umekuwa katika hali ya wasiwasi mwingi tangu kijana mweusi alipouawa na askari wa kizungu mwezi Agosti. Afisa mmoja alipigwa usoni mwingine alijeruhiwa begani.Polisi wanasema wote wanapata matibabu hospitalini. Shambulio la risasi lilitokea nje ya jengo la idara ya Polisi, ambako waandamanaji kadhaa walikusanyika baada ya Mkuu wa Polisi mjini humo Thomas Jackson alipotangaza kujiuzulu....

Like
304
0
Thursday, 12 March 2015
KAMANDA WA POLISI FERGUSON AJIUZULU KUFUATIA RIPOTI YA KASHFA YA UBAGUZI WA RANGI
Global News

KAMANDA wa Polisi katika mji wa Ferguson nchini Marekani amejiuzulu baada ya ripoti ya shirikisho kulaumu kitengo chake kina ubaguzi. THOMAS JACKSON anakabiliwa na miito ya kumtaka ajiuzulu tangu yalipotokea maafa ya kuuawa kwa kupigwa risasi kwa MICHAEL BROWN, kijana Mweusi ambaye hakuwa na Silaha yoyote wakati tukio hilo likitokea. Kijana huyo ameuawa na Mmoja wa Maafisa wake Agusti mwaka jana....

Like
249
0
Thursday, 12 March 2015
BARAZA LA USALAMA LA UMOJA WA MATAIFA LASHUTUMIWA KUSHINDWA KUTETEA RAIA SYRIA
Global News

RIPOTI ya Mashirika zaidi ya Ishirini ya Misaada ya Kibinadamu na yale ya kutetea Haki za Binaadamu yamelishutumu Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa kushindwa kutetea raia walio katikati ya vita nchini Syria. Ripoti hiyo imezishutumu nchi zenye nguvu kubwa ya ushawishi duniani kwa kushindwa kutumia nguvu zao kuandaa maazimio ya kusaidia Uhuru wa huduma za Misaada ya Kibinadamu kwa Waathirika. Aidha Ripoti ya Masharika hayo ni ya kuadhimisha Miaka Minne ya Vita nchini Syria ambavyo vinaendelea hadi...

Like
228
0
Thursday, 12 March 2015
VENEZUELA YAMUONDOA BALOZI WAKE WASHINGTON KUFUATIA VIKWAZO DHIDI YA MAAFISA WAKE
Global News

Venezuela imesema imemuita balozi wake mjini Washington MAXIMILIEN SANCHEZ arejee nyumbani baada ya vikwazo vya Marekani dhidi ya maafisa wake. Rais wa Venezuela NICOLAS MADURO ameikosoa vikali Marekani kwa kuwawekea vikwazo maafisa wa Venezuela wanaoshutumiwa kwa ukiukaji wa haki za binaadamu, akisema ataliomba bunge limpe mamlaka zaidi kupambana na kitisho cha...

Like
249
0
Tuesday, 10 March 2015
ANGELA MERKEL AITAKA JAPAN KUTAFUTA UFUMBUZI WA TUHUMA ZA WANAJESHI KUJIHUSIHA NA UTUMWA WA NGONO
Global News

KANSELA wa Ujerumani ANGELA MERKEL ameitaka Japan kuutafutia ufumbuzi mzozo unaohusiana na mfumo wa nchi hiyo wa utumwa wa ngono wakati wa vita. Akikamilisha ziara yake nchini Japan ,MERKEL amekutana na KATSUYA OKADA, Mkuu wa Chama cha Upinzani cha Democratic na kusema, Japan inatakiwa kuendelea mbele na juhudi za maridhiano na Korea Kusini. Kwa mujibu wa takwimu rasmi wanahistoria wanasema hadi Wanawake 200,000 wengi kutoka Korea, China, Indonesia, Ufilipino na Taiwan, waliwatumikia wanajeshi wa Japan katika madanguro ya...

Like
514
0
Tuesday, 10 March 2015
MAREKANI YATANGAZA KUTUMIA WANAJESHI 3000 KUSHIRIKI MAZOEZI YA KIJESHI YA NATO
Global News

MAREKANI imetangaza kutuma wanajeshi 3,000 kwenye mataifa ya Baltic kushiriki mazoezi ya Kijeshi na Washirika wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO. Tangazo lililotolewa na Wizara ya Ulinzi ya Marekani,limesema mazoezi hayo yatazijumuisha Estonia, Latvia na Lithuania, na yatakuwa ya miezi...

Like
293
0
Tuesday, 10 March 2015
UKRAINE: WAASI WAONYESHA DHAMIRA YA KUSITISHA MAPIGANO
Global News

RAIS PETRO POROSHENKO wa Ukraine amesema kwamba waasi wanaotaka kujitenga Mashariki mwa nchi yake wameondoa kiwango kikubwa cha silaha nzito kutoka mstari wa mbele wa mapambano, hali inayoashiria kuheshimiwa kwa makubaliano ya kusitisha mapigano. Akizungumza na Televisheni ya Taifa ya Ukraine Bwana POROSHENKO Amesema kuwa kila upande, kati ya Wanajeshi wa Serikali na Waasi, umeondoa silaha kwenye uwanja wa...

Like
209
0
Tuesday, 10 March 2015
BURUNDI: ALIEKUWA MWENYEKITI WA CNDD-FDD AMTUHUMU RAIS KUPANGA NJAMA ZA KUMFUNGA JELA
Global News

ALIYEKUWA mwenyekiti wa chama tawala nchini Burundi CNDD-FDD Hussein Rajabu aliyekuwa ameripotiwa kutoroka jela amemlaumu rais Pierre Nkurunziza kwa kumpangia njama ya kumfunga jela ili kutokomeza demokrasia nchini humo. Akizungumza na Shirika la Utangazaji la BBC, Bwana Rajabu amesema kuwa yeye yuko salama na wala hakutoroka jela kama ilivyodhaniwa bali alitoka jela rasmi baada ya kushirikiana na wafuasi wa chama chake. Rajabu amesema kuwa wazalendo wenzake wa CNDD-FDD ndio walifanikisha kuondoka kwake gerezani kwa ”heshima....

Like
250
0
Monday, 09 March 2015
JARIBIO LA KWANZA LA NDEGE INAYOTUMIA UMEME WA JUA LIMEFANYIKA LEO
Global News

Ndege hiyo iliruka majira ya saa 12 saa za Afrika Mashiriki ikianzia Abu Dhabi. Ndege hiyo yenye kiti kimoja ina mabawa yenye ukubwa wa jumbo jet huku ndege yenyewe ikiwa na uzito sawa na gari, mabawa yake yamefunikwa na vifaa vya vya kunasia mionzi ya jua yaani solar panels. Betri zake zina uwezo wa kuhifadhi nguvu ya umeme jua kutoka kwenye jua na hivyo kuiweza kusafiri hata nyakati za usiku. Marubani wawili wanaorusha ndege hiyo Bertrand Piccard na Andre Borschberg...

Like
236
0
Monday, 09 March 2015
JUHUDI ZA KUTATUA MZOZO SUDANI KUSINI ZAGONGA MWAMBA
Global News

MAZUNGUMZO ya kutatua mzozo unaokumba Sudan Kusini yamegonga mwamba, saa kadhaa kabla ya Umoja wa Mataifa kuwawekea vikwazo wanaohusika. Rais wa nchi hiyo, Salva Kiir na mpinzani wake ambaye aliwahi kuwa makamu wake, Riek Machar, wamekuwa wakijadili mipango ya kugawanya mamlaka ili kukomesha vita vya wenyewe kwa wenyewe ambavyo vimesababisha maelfu ya watu kuuawa na zaidi ya watu milioni moja na nusu kupoteza makazi. Umoja wa mataifa umetishia kuwawekea vikwazo watu binafasi wanaojaribu kuzuia makubaliano hayo iwapo makundi hayo mawili...

Like
256
0
Thursday, 05 March 2015