RAIS wa Marekani BARACK OBAMA ameihimiza Iran isitishe mpango wake wa nyuklia angalau Muongo Mmoja, kama sehemu ya Mkataba unaotarajiwa kufikiwa kulegeza vikwazo. Kauli ya Rais OBAMA imekuja kabla hotuba ya Waziri Mkuu wa Israel BANJAMIN NETANYAHU katika bunge la Marekani leo kupinga mkataba huo. Bwana OBAMA amesema Iran itahitaji kukubali mkataba utakaositisha uwezo wake wa kurutubisha Madini ya Urani na kuweka chini ya kiwango kinachohitajika kutengeneza Silaha za...
UMOJA wa mataifa umesema kuwa takriban watu 6000 wameuawa mashariki mwa Ukraine, Kwenye ripoti yake ya hivi punde kuhusu mzozo unaoendelea mashariki mwa Ukraine. Ofisi ya haki za binadamu ya umoja wa mataifa inasema kuwa mapigano ya hivi majuzi yamesababisa vifo vya mamia ya watu. Ripoti hiyo inatoa picha kuhusu hali ilivyo mashariki mwa Ukraine ambapo mamia ya watu wameuawa kwa muda wa miezi miwili iliyopita na kufikisha idadi ya wau ambao wameuawa eneo hilo kuwa takriban watu 6,000. ...
SERIKALI ya Iraq imesema kuwa wanajeshi wake wameanza kampeni ya kuwaondoa wapiganaji wa Islamic State kutoka mji wa Tikrit . Mji huo mkuu wa jimbo la kaskazini la Salahuddin ulidhibitiwa na wanamgambo wa Islamic state Juni mwaka uliopita. Serikai inasema kuwa wanajeshi 30,000 wakiwemo wapiganaji 200 wakujitolea wa kisuni pamoja na wakurdi wanaelekea mji wa Tikrit wakisadiwa na ndege za kivita . Mji wa Tikrit uko kilomita 150, Kaskazini mwa mji wa mkuu wa...
WAZIRI Mkuu wa Israeli BENJAMIN NETANYAHU amewasili nchini Marekani kupinga dhidi uwezekano wa kufikia makubalino na Iran juu ya mpango wake wa Nyuklia. Bwana NETANYAHU amesema mkataba huo hautoshi kuizuia Iran kumiliki Silaha za Nyuklia. Pia anatarajia kulihutubia Bunge la Congress March 03, hotuba ambayo haikukubaliwa kabla na Utawala wa Rais BARRACK OBAMA na kuiudhi Ikulu ya...
MAKAMU wa Rais wa Sierra Leone SAMUEL SAM-SUMANA amejiweka mwenyewe katika Karantini kwa siku 21 baada ya mlinzi wake mmoja kufa Jumanne iliyopita kutokana na ugonjwa hatari wa Ebola. SAM-SUMANA anakaimu wadhifa wa Urais baada ya rais Wa nchi hiyo ERNEST KOROMA kuondoka Sierra Leone kwenda Ubelgiji kuhudhuria mkutano kuhusu Ebola utakaofanyika March. SAM-SUMANA anatekeleza majukumu yake kutoka nyumbani kwake na ni Kiongozi wa kwanza wa ngazi ya juu wa Afrika kuwa katika Karantini tangu Mlipuko wa Ugonjwa wa Ebola...
MAHAKAMA moja ya jijini New York, Marekani imemhukumu Khalid al-Fawwaz kwa kuhusika na mashambulizi ya mabomu ya balozi za Marekani nchini Kenya na Tanzania mwaka 1998. Waendesha mashtaka wamemtaja al-Fawwaz kuwa mmoja wa watu waliokuwa karibu zaidi na aliyekuwa kiongozi wa al-Qaida, Osama bin Laden. Baada ya mahakama kumkuta na hatia katika makosa 29, al-Fawwaz mwenye miaka 52 sasa anaweza kuhukumiwa kifungo cha maisha. Raia huyo wa Saudi Arabia alikamatwa jijini London, Uingereza, mwaka 1998 na kukabidhiwa kwa Marekani mwaka...
Maelfu ya wakimbizi kutoka Jamhuri ya Afrika ya Kati waliokimbilia Jamhuri ya Kidmekorasia ya Congo sasa wanakumbwa na balaa la njaa. Shirika la Madaktari Wasio na Mipaka, MSF, limesema wakimbizi hao walioko kaskazini mashariki mwa Congo wanakabiliwa na utapiamlo kwani hawapati chakula na maji ya kutosha na wanategemea tu wahisani kuwapatia mahitaji ya msingi. Katika kipindi cha wiki moja iliyopita, MSF imeshuhudia watoto kumi wakilazwa hospitalini kutokana na utapiamlo....
KATIBU MKUU wa NATO Jens Stoltenberg ameonya kwamba jaribio lolote la kupanua mipaka inayoshikiliwa na wapiganaji wanaotaka kujitenga nchini Ukraine , halitakubalika na kuiambia Urusi kuondoa vifaa 1,000 vya kijeshi kutoka katika ardhi ya nchi jirani ya Ukraine. Akizungumza baada ya mkutano na waziri mkuu wa Italia Matteo Renzi , katibu mkuu wa NATO ameeleza matumaini ya tahadhari juu ya matarajio ya makubaliano tete ya kusitisha mapigano kati ...
KATIBU MKUU wa zamani wa umoja wa mataifa Kofi Annan amewasili nchini Cuba kuhamasisha mazungumzo ya amani kati ya serikali ya Colombia na nchi zenye makundi ya waasi. Mazungumzo hayo yanayofanyika mjini Havana ni mwendelezo wa jitihada za kusaka Amani katika nchi kwa zaidi ya miaka miwili hadi sasa. Hata hivyo katika mazungumzo hayo ya Amani lengo ni kumaliza migogoro iliyodumu kwa zaidi ya miongo mitano....
WAZIRI wa mambo ya kigeni wa Marekani John Kerry amesema Urusi bado haijatimiza masharti ya makubaliano ya Minsk kuhusu usitishaji wa mapigano. Kerry amewaambia wabunge mjini Washington kwamba Urusi na wapiganaji wanaoiunga mkono Urusi hawaheshimu masharti ya makubaliano. Wakati huo huo , rais wa Urusi Vladimir Putin ameonya kwamba Urusi inaweza kusitisha upelekaji wa gesi nchini Ukraine. Kansela wa Ujerumani Angela Merkel ameionya Urusi kwamba vikwazo vinaweza kutekelezwa....
SHIRIKA la afya ulimwenguni WHO limetangaza kwamba maambukizi mapya ya ugonjwa wa Ebola katika mataifa ya Afrika magharibi yamepungua. Wiki iliyopita, kulikuwa na zaidi ya watu 100 walioambukizwa ugonjwa huo nchini Sierra Leone, Guinea na Liberia. Wiki hii , maambukizi mapya ya Ebola yamepungua chini ya watu 100, kwa mujibu wa shirika hilo la afya ulimwenguni. Hata hivyo kituo cha taifa kinachohusika na suala la ugonjwa wa Ebola nchini Sierra Leone ...