TANZANIA kwa kushirikiana na Uturuki inatarajia kujenga kituo kikubwa cha watu wenye ulemavu wa Ngozi- albino, ambacho kitakuwa na huduma mbalimbali muhimu ikiwamo shule na afya. Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe amesema kituo hicho kitawasaidia albino kupata huduma muhimu wakiwa kwenye mikono salama. Alikuwa akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam baada ya kumalizika kwa kikao cha ndani cha mabalozi na wawakilishi wa nchi mbalimbali. Waziri Membe amesema kituo hicho kitakuwa na watalaam...
WATU 35 wamefariki dunia na wengine 55 kujeruhiwa baada ya nyumba zao kuwaangukia na kuwafunika usiku wa kuamkia leo kutokana na mvua kubwa iliyonyesha wilayani Kahama, mkoani Shinyanga. Taarifa zilizothibitishwa na Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Benson Mpesya amesema mvua hiyo kubwa iliambatana na upepo mkali, hivyo nyumba nyingi zilianguka na nyingine kuezuliwa na kuharibiwa kabisa. Mpesya amesema mpaka sasa wamefanikiwa kupata miili ya watu 35 waliopoteza maisha baada ya kufukua nyumba nyingi, na majeruhi wamekimbizwa hospitali ya wilaya kwa...
Mshambuliaji wa klabu ya Sunderland Adam Johnson ametiwa mbaroni kwa tuhuma za kuwa na mahusiano ya kimapenzi na binti mwenye umri wa miaka 15. Polisi wa huko Durham wamethibitisha kuwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 alifikishwa kwenye kituo hicho cha polisi kwa ajili ya mahojiano na baadae aliachiwa. Kwa upande wa klabu ya Sunderland AFC mchezaji huyo kwa sasa amewekwa kando ili kupisha uchunguzi wa polisi, kukamatwa kwa mchezaji huyo wa ligi kuu ya Uingereza kuliripotiwa na gazeti...
VIONGOZI wa nchi za Magharibi wamekubaliana kwamba hatua kali kutoka kwa Jumuiya ya Kimataifa zitahitajika iwapo kutatokea ukiukaji wa utekelezaji wa Mkataba wa kusitisha mapigano nchini Ukraine. Mkataba huo umesainiwa Mjini Minsk nchini Belarus Febrauari 12 mwaka huu kati ya majeshi ya Serikali ya Ukraine na Waasi wanaoiunga mkono Urusi. Rais wa Marekani BARACK OBAMA, mwenzake wa Ufaransa FRANCOIS HOLLANDE, Kansela wa Ujerumani ANGELA MERKEL, Waziri Mkuu wa Uingereza DAVID CAMERON na Waziri Mkuu wa Italia MATTEO RENZI wameshiriki katika...
WAZIRI Mkuu wa Israel BENJAMIN NETANYAHU amelionya Bunge la Marekani kwamba mkataba na Iran uliopendekezwa hautazuia wala kupunguza uwezo wake wa kutengeneza mabomu ya nyuklia. Akilihutubia bunge hilo Bwana NETANYAHU amezikosoa juhudi za Rais wa Marekani BARACK OBAMA kutafuta makubaliano na Iran kuhusu mpango wake wa nyuklia wenye utata. Bwana NETANYAHU ameonya kwamba utawala wa Bwana OBAMA unaifungulia mlango Iran kuelekea kutengeneza bomu la nyuklia. ...
SHIRIKA lisilo la Kiserikali la Save Vulnerable foundation linatarajia kuanzisha mradi utakao wasaidia wananchi wa Mjini na Vijijini wanaoishi katika mazingira magumu,huku waliwalenga Zaidi watu wenye matatizo ya Ulemavu katika suala la Elimu Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es salaam Katibu Mkuu wa Shirika hilo LEONTINE RWECHUNGURA amesema kuwa ripoti ya haki za Binadamu ya mwaka 2010 na Ripoti ya Tanzania ya mwaka 2008 imethibitisha kuwa kiwango cha ...
MENEJA Miradi ya Kinyerezi Mhandisi SIMON JILIMA amesema kuwa mtambo wa Kinyerezi 1 unaojengwa na kampuni ya Yakobsen Elektro ya Norway unatarajia kukamilika mapema Juni mwaka huu. Mhandisi JILIMA ameeleza hayo mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini iliyofanya ziara katika Mtambo huo ili kujionea maendeleo ya ujenzi wake. Kamati hiyo imeanza ziara ya kutembelea Miradi ya umeme iliyopo katika mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma, Singida, Arusha na Kilimanjaro pamoja na kuzungumza na wadau wa...
Kutoka kwenye kundi lililowahi kufanya vizuri Mexcana Lacavela na baadae kuvunjika kimya hivi karibuni kumekuwapo na tetesi za kuwa kundi hilo limerudi tena kwa kuwakutanisha member wake kwenye wimbo mmoja uliopewa jina la biashara ambao kwa mujibu wa vyanzo vya habari wimbo huo umetayarishwa na producer Mr T touch. Swali linalokuja kimsingi tumezoea kusikia kazi za kundi hilo zikifanywa na producer Messsen kwa nini kazi hii imefanywa na Mr T, Je kuna tatizo kati yao na producer Messen au wameamua...
KANSELA wa Ujerumani ANGELA MERKEL ameeleza kuunga kwake mkono mpango mpya wa uwekezaji katika Bara la Ulaya. Mpango huo wa Uwekezaji umependekezwa mwaka jana na Rais wa Halmashauri ya Umoja wa Ulaya JEAN-CLAUDE JUNCKER ambapo ni mpango wa Euro Bilioni 300 wa kuifanya bora miundo Mbinu katika mataifa ya Ulaya. MERKEL ameeleza uungaji wake mkono katika mpango huo , lakini amesema mageuzi zaidi na makubaliano ya Biashara huru na...
WAZIRI wa Mambo ya Kigeni wa Ukraine PAVLO KLIMKIN ameonesha wasiwasi wake kuhusiana na matarajio kwamba makubaliano yanayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa ya kusitisha mapigano na waasi wanaoiunga mkono Urusi yataendelea, wakati akitoa wito wa kuongezeka kwa kikosi cha Kimataifa cha kuangalia makubaliano hayo. Bwana KLIMKIN amewaambia Waandishi Habari mjini Tokyo kwamba hali katika eneo la mapigano ni mbaya na ya wasi wasi licha ya...
IMEELEZWA kuwa Wanawake waliovijijini wanapambana na mifumo zaidi ya mmoja ikiwemo mfumo Dume, Utandawazi, Wizi pamoja na aina nyingine ya Ukandamizi wa Rangi ya Ngozi na Mwili. Akizungumza na EFM Mtafiti Shirikishi Jamii AGNES LUKANGA amesema kuwa mabadiliko katika mfumo Kandamizi na Unyonyaji yanaletwa na Wanaokandamizwa na kunyonywa hasa walio pembezoni wenyewe....