KATIBU MKUU wa zamani wa umoja wa mataifa Kofi Annan amewasili nchini Cuba kuhamasisha mazungumzo ya amani kati ya serikali ya Colombia na nchi zenye makundi ya waasi. Mazungumzo hayo yanayofanyika mjini Havana ni mwendelezo wa jitihada za kusaka Amani katika nchi kwa zaidi ya miaka miwili hadi sasa. Hata hivyo katika mazungumzo hayo ya Amani lengo ni kumaliza migogoro iliyodumu kwa zaidi ya miongo mitano....
KAMPUNI ya simu ya Obi mobiles imedhamiria kusambaza teknolojia kwa watu wengi zaidi nchini Tanzania lengo ikiwa ni kufanya utendaji wenye tija katika vifaa vya simu za mkononi kwa maendeleo ya nchi na kusaidia kukuza uchumi. Hayo yamebainishwa na mwanzilishi ambaye pia ni mkurugenzi mtendaji wa zamani wa Apple, John Sculley, ambapo amesema kampuni hiyo inalenga kuongeza mauzo kupitia mpango mkakati unaowalenga vijana na watumiaji wanaokwenda na wakati na matumizi ya simu za mkononi. Kampuni ya Obi mobiles imezindua aina...
JESHI la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro linamtafuta PETER MROSO mkazi wa Kijiji cha Ubetu Wilayani Rombo kwa tuhuma za kumuua mkewe kisha kuuzika mwili wake na kubakiza kichwa. Tukio hilo limetokea February 25 mwaka huu nyumbani kwa Marehemu maeneo ya Ubetu ambapo mtuhumiwa alimpiga mkewe JENIPHER PETER sehemu za kichwani. Mashuhuda ambao hawakutaka kutaja majina yao wamedai kuwa mara baada ya mume huyo kumpiga mkewe hadi kufa aliuchukua mwili wake na kwenda kuuzika katika boma la ng’ombe huku kichwa chake...
WAZIRI wa mambo ya kigeni wa Marekani John Kerry amesema Urusi bado haijatimiza masharti ya makubaliano ya Minsk kuhusu usitishaji wa mapigano. Kerry amewaambia wabunge mjini Washington kwamba Urusi na wapiganaji wanaoiunga mkono Urusi hawaheshimu masharti ya makubaliano. Wakati huo huo , rais wa Urusi Vladimir Putin ameonya kwamba Urusi inaweza kusitisha upelekaji wa gesi nchini Ukraine. Kansela wa Ujerumani Angela Merkel ameionya Urusi kwamba vikwazo vinaweza kutekelezwa....
SHIRIKA la afya ulimwenguni WHO limetangaza kwamba maambukizi mapya ya ugonjwa wa Ebola katika mataifa ya Afrika magharibi yamepungua. Wiki iliyopita, kulikuwa na zaidi ya watu 100 walioambukizwa ugonjwa huo nchini Sierra Leone, Guinea na Liberia. Wiki hii , maambukizi mapya ya Ebola yamepungua chini ya watu 100, kwa mujibu wa shirika hilo la afya ulimwenguni. Hata hivyo kituo cha taifa kinachohusika na suala la ugonjwa wa Ebola nchini Sierra Leone ...
MTANDAO wa Kijinsia Tanzania-TGNP umeitaka jamii kuishi kwa kufuata mbinu za kiraghibishi yaani utafiti ili kumuwezesha mtu kutambua nafasi yake na uwezo wa kubadilisha mazingira ili kuleta maendeleo nchini. Akizungumza katika semina ya Uraghibishi,mtafiti Mkuu kutoka TGNP AGNESS LUKANGA amesema kuwa endapo jamii itaweza kuishi kwa kufuata njia za Uraghibishi itaweza kujitegemea ikiwa ni pamojua na kuhamasisha mtu kufanya kitu ambacho kitaleta maendeleo katika jamii. Ameeleza kumekuwa na tabia ya baadhi ya watu kutoa maamuzi ya mambo...
KAMPUNI ya Simu ya Push Mobile imetiliana saini na Serikali ya Tanzania na Umoja wa Mataifa -UN ya kuwafikia watu milioni 10 ikiwahabarisha kuhusu Ugonjwa hatari wa Ebola. Kwa mujibu wa Taarifa ya Umoja wa Mataifa, Kampuni hiyo ya Simu imesema kupitia ushirikiano huo Kampuni hiyo itaunga mkono juhudi za Serikali ya Tanzania na Umoja wa Mataifa wa kutoa Elimu dhidi ya ugonjwa huo ujumbe mfupi utakaoelezea ugonjwa wa ebola. Kama sehemu ya makubaliano, Push Mobile , UN, Serikali na...
Mkongwe katika tasnia ya muziki duniani Madonna amepatwa na mkasa huo wakati anatumbuiza kwenye maonyesho ya ugawaji wa tuzo za Brit kwa mwaka 2015. Katika tuzo hizo Sam Smith na Ed Sheeran wameondoka na tuzo mbili mbili kila mmoja Madonna alikutwa na balaa hilo pale mmoja wa wanenguaji wake alipojaribu kuivua kofia ya msanii huyo iliyounganishwa na vazi kama joho Hata hivyo msanii aliendelea na show yake na kuonyesha hakuathiriwa na tukio hilo Kupitia akaunti yake ya twitter Madonna alitoa...
UINGEREZA inapanga kuwapatia mafunzo wanajeshi wa serikali ya Ukraine. Waziri mkuu wa Uingereza David Cameron amesema mjini London kuwa kundi la wataalamu wa kijeshi watapelekwa katika jamhuri hiyo ya zamani ya Kisovieti wiki ijayo. Kwa mujibu wa shirika moja la habari la Uingereza, kundi hilo litakuwa na wanajeshi 75, japokuwa hakuzungumzia uwezekano wa kupatiwa silaha wanajeshi wa Ukraine....
WAZIRI wa Mambo ya Nchi za Nje wa Libya Mohammed Dayri ameonya kuwa Libya inaweza kugeuka Syria kutokana na kuzidi kupata nguvu makundi ya itikadi kali. Amezitolea wito nchi za magharibi ziwapatie silaha wanajeshi wa Libya ili waweze kupambana na waasi. Awamu nyingine ya mazungumzo ya kusaka ufumbuzi wa amani ilikuwa ifanyike kesho nchini Moroko, lakini yameakhirishwa baada ya bunge la Libya linalotambuliwa kimataifa kusema halitatuma wawakilishi kutokana na mashambulio ya hivi karibuni yaliyoangamiza maisha ya zaidi ya watu 40....