JESHI la polisi kanda maalumu ya Dar es salaamu limethibitisha kuundwa kwa timu maalumu kwa ajili ya kuchunguza na kupeleleza kifo cha dada wa bilionea Msuya ambapo tayari wanamhoji aliyekuwa mume wake . Kwa mujibu wa Kamanda wa polisi kanda hiyo, kamishina SIMON SIRRO, Jeshi hilo pia limefanikiwa kutoza faini a magari yanayo kiuka sheria za usalama barabarani ambapo kiasi cha shilingi milino 548 laki 1 na sitini zimeweza kukusanywa. Kamanda SIRRO amewaambia wandishi wa Habari leo kuwa...
RAIS wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dokta John Pombe Magufuli amemteua Jaji shabani Ally Lila, kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani ambaye kabla ya uteuzi huu alikuwa Jaji Kiongozi. Wakati huo huo rais Magufuli amemteua Mheshimiwa Anne Semamba Makinda kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya mfuko wa Bima ya Afya-NHIF. Uteuzi wa Mheshimiwa Makinda ambaye ni spika mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, umeanza Mei 25 mwaka huu. ...
Mahakama ya kijeshi kwenye mji mkuu wa Somalia Mogadishu, imewahukumu kifungo cha maisha wanaume wawili ambao walipatikana na hatia ya kupanga shambulizi dhidi ya ndege ya shirika la Daallo mwezi Februari. Bomu lililipuka ndani ya ndege hiyo muda mfupi baada ya kupaa kutoka uwanja wa ndege wa Mogadishu ikiwa safarini kwenda nchini Djibouti. Shimo lilitobolewa kando mwa ndege hiyo lakini hata hivyo ndege haikusambaratika. Abiria mmoja ambaye alitupwa nje ya ndege hiyo aliaga dunia na wengine wawili wakajeruhiwa. Washtakiwa wengine...
Mauaji ya Sokwe katika mbuga ya wanyama ya Cincinnati nchini Marekani yamezua utata katika mtandao wa Twitter. Sokwe huyo anadaiwa kumuangusha na kumvuruta kijana wa miaka minne. Sokwe huyo alipigwa risasi na kuuawa kufuatia kisa hicho cha kumvuruta mtoto. Watu katika mtandao wamesema sokwe huyo kwa jina Harambe hangestahili kuuawa kwani hakuwa na niya ya kumdhuru mtoto huyo. Wengi walitumia#hakikwaHarambe. Huku wengine wakisema wazazi wa kijana huyo ndio wa kulaumiwa kwa kukosa kumuangalia mwanawe. Maafisa wa shirika la wanyama pori...
Naibu kiongozi wa Chama cha kupambana na uhamiaji nchini Ujerumani amezungumza maneno ya kibaguzi dhidi ya mchezaji nyota wa Ujerumani Jerome Boateng ambaye baba yake ni raia kutoka Ghana. Alexander Gauland,aliliambia Gazeti la Ujerumani la (the Frankfurter Allgemeine) kuwa watu wanafikiri Boateng ni mchezaji mzuri lakini kamwe hatomuhitaji kama rafiki yake. Gauland alilaaniwa vikali na wachezaji mbalimbali,Waziri wa mambo ya ndani pamoja na Rais wa shirikisho la soka nchini Ujerumani ,Reinhard Grindel amesema maneno yake kuwa hayana maana....
Aliyekuwa mshambuliaji wa klabu ya PSG nchini Ufaransa Zlatan Ibrahimovic amesema kuwa alipokea ombi la kujiunga na kilabu moja ya ligi ya Uingereza lakini akakataa kuthibitisha iwapo klabu hiyo ni Manchester United au la. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 34 yuko huru baada ya kuondoka PSG na amehusishwa na uhamisho wa United. Alipoulizwa iwapo ombi hilo linatoka Old Trafford ,alisema :Wacha tuone kitakachofanyika. Aliyekuwa kocha wa Chelsea Jose Mourinho anatarajiwa kutangazwa mkufunzi wa Manchester United na alifanya kazi na...
RAIS wa Zimbabwe Robert Mugabe amesema kuwa yeye sio Mmarekani wala Muingereza wakati akiwahutubia karibu watu elfu 50,000, wafuasi wake kwenye mkutano uliofanyika kwenye mji mkuu Harare kwa heshima yake. Mugabe mwenye umri wa miaka 92 amekana uwezekano wowote wa kuondoka madarakani na kuwashambulia viongozi hasimu ndani ya chama tawala cha ZANU-PAFU kwa kupanga kumrithi. Amesema kuwa yeye anawahudumia watu wa Zimbabwe na kuwa ataondoka tu ikiwa watu wangetaka afanye...
MAHAKAMA mjini Kampala leo inatarajiwa kutoa hukumu katika kesi ambapo wanaume 13 wameshtakiwa kuhusiana na mashambulio ya mabomu yaliyotekelezwa na al-Shabaab mwaka 2010. Watu zaidi ya 70 walifariki kwenye mashambulio hayo yaliyotekelezwa wakati watu wakitazama fainali ya Kombe la Dunia la mwaka 2010. Kesi hiyo imechukua miaka...
WANAWAKE wakazi wa mji wa Kigoma, wamekumbwa na taharuki kufuatia kuibuka mtu asiyefahamika anayewaingilia kinguvu wakati wamelala kwenye nyumba zao usiku huku akitumia panga kuwatisha au kuwakata kata mapanga sehemu mbali mbali za miili yao wale wanaokataa kutekeleza matakwa yake. Mpaka sasa zaidi ya wanawake 10 wanaelezwa kuvamiwa na mtu huyo ambaye kwa sasa ni maarufu kwa jina la Teleza, na inadaiwa kuwa huwafuata Zaidi wanawake wasio na waume na hutumia kisu kuharibu vitasa vya milango kabla ya kuingia ndani....
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli atakuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa Mkutano wa mashauriano wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi Nchini (CRB) unaofanyika leo katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam. Mkutano huo wa mwaka wa mashauriano na wadau wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi unatarajiwa kuhudhuriwa na zaidi ya Makandarasi na wadau wa Sekta ya Ujenzi wapatao elfu 1,000 na utafanyika kwa siku mbili leo na...
WAZIRI wa mipango wa serikali mpya ya Brazil amewekwa pembeni baada ya kukutwa katika mkanda wa video akifanya njama ya kukwamisha uchunguzi mkubwa wa nchi hiyo unaohusu ufisadi. Katika rekodi ya kanda hizo, ambazo zimetolewa na gazeti moja nchini humo, waziri Romero Juca, ameonekana akisema kuwa kuondolewa madarakani kwa Rais Dilma Rousseff, kutazuia kuchunguzwa kwa kampuni ya serikali ambayo ni kubwa katika uzalishaji wa mafuta, Petrobras. Hata hivyo, waziri huyo amesema kauli yake hiyo imeeleweka vibaya na kwamba anaunga mkono uchunguzi...