SIKU baada ya kuuita Uislamu kuwa ni sehemu ya Ujerumani, Kansela ANGELA MERKEL amesema serikali yake itatumia njia zote ilizonazo kupambana na ukosefu wa uvumilivu na ubaguzi, akitaja kutoshirikishwa kwa baadhi ya makundi ya kijamii kuwa ni jambo la kulaumiwa. Matamshi yake yamekuja siku moja baada ya waandamanaji 25,000 wanaoupinga Uisilamu kuandamana katika mji wa Mashariki wa Dresden kutaka sheria kali zaidi za uhamiaji na kukomesha sera ya kukubali utamaduni...
GAZETI la Charlie Hebdo leo limeanza kusambaza toleo la gazeti lake ambalo limechapisha kibonzo cha Mtume MOHAMMAD kwenye ukurasa wake wa mbele. Imeelezwa kuwa zaidi ya Nakala Milioni za gazeti hilo zimeanza kusambazwa na nyingine zitafuata iwapo wanunuzi wataongezeka....
SERIKALI imeombwa kuhakikisha kuwa shule Maalum za watoto wenye Ulemavu zinapatiwa vifaa vya kufundishia na kujifunzia ili kuondoa changamoto zinazozikabili shule hizo. Rai hiyo imetolewa jijini Dar es salaam na baadhi ya Walimu na Wanafunzi wa shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko shule ambayo ina wanafunzi wenye Ulemavu na wasio na Ulemavu ....
KAMATI ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa-LAAC imebaini kuwepo kwa Ufisadi na uzembe katika Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam. Hali hiyo imesababisha wajumbe kuwaomba Watendaji akiwemo Meya wa jiji hilo DIDAS MASABURI kupisha Kamati hiyo kwa muda ili kujadili taarifa zao. Hatua hiyo imetokana na baadhi Wajumbe wa Kamatihiyo kuhoji ni kwa nini jiji wamekataa kumpatia Simon Group Akaunt kwa ajili ya kufanya malipo ya Hisa zilizokuwa zikiuzwa na jiji la Dar es salaam....
Meneja wa timu ya taifa ya England Roy Hodgson amejikuta akilazimika kufuta ratiba ya kukutana na wachezaji wake na kupata chakula cha usiku pamoja kufuatia ratiba kuwabana wachezaji hao. Roy Hodgson alikuwa na lengo la kukutana na wachezaji hao mwishoni mwa mwezi wa kwanza ili kuweza kujadili pamoja ikiwemo ushindi dhidi ya Scotland. Shirikisho la mpira wa miguu nchini humo limeeleza kuwa timu hiyo pia ilikuwa ipo kwenye utayari wa kikao hicho ila kufuatia kile kilichotokea wamejikuta wakiahirisha kukutana na...
Fainali za kombe la mapinduzi zimemalizika jana katika uwanaja wa Amani mjini Unguja huko zanzabar kwa kuwakutanisha vinara wa ligi kuu ya bara mtibwa sugar na wekundu wa msimbazi Simba Ambapo imeshuhudiwa katika fainali hiyo Simba wakilibeba kombe kwa kuifunga mtibwa kwa mikwaju 4 – 3 baada ya kwenda suluhu kwa sare tasa katika dakika 90 za mchezo Ushndi huo wa simba ni mwanzo mzuri kwa kocha wao mpya kabisa Mserbia Goran kopunorvic ambae amejiunga na club hiyo hivi karibuni...
Kiungo mshambuliaji kutoka Colombia Radamel Falcao anaepokea kiasi cha paundi 265,000 kwa wiki kuna uwezekano wa kutochezea tena katika klabu ya Man Utd Hii imekuja mara baada ya wakala wa mchezaji huyo kusema Falcao ataichezea moja kati ya klabu kubwa duniani katika msimu ujao Hayo yamesemwa na Jorge Mendes. Ambae ndie wakala...
Chris brown hataki tena kufanya show za kwenye Club kufuatia mfululizo wa matukio ya kuponea chupuchupu mara kadhaa risasi zinapofyatuliwa na makundi ya wahuni kwenye Club hizo. Imeelezwa kuwa Cris Brown ameitisha kikao cha dharura na meneja wake pamoja na timu yake nzima kuwataarifu juu ya maamuzi yake ya kufuta show zote za club zilizokuwa kwenye ratiba zake ili kwa sababu za kiusalama mara baada ya tukio la mwisho lililotokea huko San Jose Kwenye tukio la San Jose watu watano...
KANSELA wa Ujerumani ANGELA MERKEL anajiandaa kujiunga na Jamii ya Waislamu katika maandamano ya Maridhiano na Kuvumiliana nchini Ujerumani na kulaani mashambulio yaliyofanywa na vijana wenye itikadi kali mjini Paris nchini Ufaransa wiki iliyopita. Maandamano hayo pia yamelenga kutuma ujumbe wa kupinga vuguvugu lililooongezeka nchini Ujerumani dhidi ya Waislamu....
SERIKALI ya Uganda imeeleza kuwa Kamanda wa Kundi la Waasi la Lord Resistance Army-LRA DOMINI ONGWEN amejisalimisha Jamuhuri ya Afrika ya Kati, hivyo atakabidhiwa kwa Mahakama ya Kimataifa ya ICC. Kamanda huyo ni miongoni mwa watu wa kundi la LRA wanaosakwa na viongozi wa Mashitaka katika Mahakama ya Kimataifa ya ICC kwa kutenda uhalifu dhidi ya...
VIJANA WA MKOANI Kilimanjaro wameziomba Halmashauri zao kuhamasisha vijana kuanzisha SACCOSS za Wilaya zitakazowawezesha vijana kuwekeza na kuwasaidia kuomba mkopo wa Mfuko wa Maendeleo ya Vijana utakaopitishiwa katika SACCOSS hizo ili waweze kujiajiri. Hayo yamesemwa na Vijana wakati wa kufunga Semina ya Uhamasishaji kwa vijana kuhusu Mfuko wa Maendeleo ya Vijana na kuiomba Wizara yenye dhamana na vijana kujitolea kutoa Elimu kwa vijana mara kwa mara itakayowawezesha vijana kujitambaua na kuwajengea...