MAHAKAMA moja ya kijeshi nchini Nigeria imewahukumu kifo askari 54 kwa kukataa kupigana na kundi la wapiganaji wa Kiislamu la Boko Haram. Wanajeshi hao ambao walipatikana na kosa la uasi,walituhumiwa kukataa kuikomboa miji mitatu iliyokuwa imetekwa na Boko Haram mwezi Agosti. Wakili wa wanajeshi hao 54 amesema kuwa watawauwa kwa kupigwa risasi huku wengine watano wakiachiliwa huru. Hata hivyo Wanajeshi hao wamelalamika kuwa hawapewi silaha na mabomu ya kutosha kupigana na kundi hilo la Boko Harm. ...
WABUNGE Nchini Kenya wametofautiana vikali bungeni na kuvuana mashati huku wakirushiana ngumi kufuatia mjadala kuhusu mswaada tatanishi wa usalama ambao wabunge wa upinzani wanasema unakiuka uhuru wa Wakenya. Bunge limelazimika kuahirisha vikao vyake kwa dakika 30 badala ya kujadili mswada tatanishi kuhusu usalama wa nchi. Kikao cha leo kilikuwa kikao maalum ambacho kilipaswa kupitisha mswada huo ambao baadaye utaidhinishwa na Rais kuwa sheria. Mwenyekiti wa kamati ya usalama wa bunge, Bwana Asman Kamama, alijaribu kufaya...
Mabingwa wa Tanzania Bara, Azam FC jana usiku walipokea kichapo cha pili mfululizo katika ziara yao ya huko nchini Uganda. Wanalambalamba hao imechapwa goli 1-0 dhidi ya URA katika mchezo uliochezwa jijini Kampal, Uganda. Kikosi hicho ambacho kipo chini ya kocha Mcameroon Joseph Marius Omog na Mganda, George “Best” Nsimbe imeweka kambi Uganda kujiandaa na Ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara iliyosimama kwa mwezi mmoja, ambayo itarejea wiki ijayo. Katika dirisha dogo la usajili Azam FC imewasajili beki Serge Wawa...
Kiungo wa kimataifa wa England Raheem Sterling aipeleka klabu ya Liverpool katika hatua ya nusu fainali ya kombe la ligi (Capital One Cup) baada ya kufunga magoli mawili katika mchezo dhidi ya klabu ya Bournemouth. Liverpool iliingia katika mchezo huo wa robo fainali ikiwa na jeraha la kuchapwa magoli matatu kwa sifuri dhidi ya mahasimu wao Manchester Unired, ilipata goli la kwanza mnamo dakika ya 20 kupitia kwa Sterling kabla ya Lazar Markovic kuongeza goli la pili mnamo dakika ya...
BAADA ya nusu karne ya siasa za Vita Baridi, hatimaye Marekani na Cuba zimetangaza nia ya kurejesha mahusiano ya kidiplomasia. Hatua hiyo inayochukuliwa kama tukio la kihistoria baina ya mahasimu hao, ilitangazwa jana na Rais Barack Obama wa Marekani, ambaye sasa nchi yake itaacha mtazamo wa kikale ambao kwa miongo kadhaa umeshindwa kuendeleza maslahi ya taifa. Mjini Havana, Rais Raul Castro wa Cuba naye amelihutubia taifa akisema mataifa hayo mawili yamekubaliana kurejesha mahusiano, hata kama bado tatizo kuu lingalipo. Tangazo...
AWAMU ya pili ya Uchaguzi wa rais nchini Tunisia inatarajia kufanyika siku ya Jumapili. Taarifa zaidi zimeeleza kuwa Rais aliyeko madarakani, MONCEF MARZOUKI atapambana na mkongwe wa siasa, BEJI CAID ESSEBSI. Kwa mara ya kwanza Watunisia wataruhusiwa kumchagua Rais wao kwa uwazi tangu nchi hiyo ilipopata Uhuru wake kutoka kwa Ufaransa, mwaka 1956. Awamu ya kwanza ya uchaguzi wa Rais imefanyika Novemba 23, na Bwana ESSEBSI, mwenye umri wa miaka 88, amepata asilimia 39 ya kura, kiwango ambacho hakikutosha kumpa...
KATIBU MKUU wa Chama Cha Mapinduzi-CCM ABDULRAHMAN KINANA amesema kuwa watu wa Kabila la Wamasai ni watanzania halali na kwamba hawana sababu ya kutafuta Uraia kwenye Maeneo mengine. Kinana ameeleza kuwa tatizo la migogoro ya ardhi ikiwa ni pamoja na Wafugaji kuingia kwenye mapori ya Akiba na Hifadhi za Taifa haliwahusu Wamasai pekee bali ni la nchi nzima. Kiongozi huyo wa chama cha Mapinduzi, ametoa kauli hiyo wakati akijibu Malalamiko yaliyotolewa na viongozi wa Mila wa Kabila la Wamasai katika...
WANAFUNZI waliofaulu mtihani wa darasa la Saba wanatarajiwa kupangiwa shule kuendelea na Elimu ya Sekondary muda wowote kuanzia leo. Habari za kuaminika zimeeleza kuwa majina ya Wanafunzi na shule walizopangiwa yatatangazwa leo ikiwa ni maandalizi ya kuanza kidato cha kwanza mwakani. Wanafunzi laki nane na elfu nane mia moja kumi na moja wa shule za msingi nchini wamefanya mtihani wa kumaliza darasa la Saba September 9 mwaka huu idadi ambayo ni pungufu kulinganisha na waliomaliza mwaka jana ambao walikuwa 844,938....
SERIKALI ya uganda imetenga shilingi bilioni 20 kwa ajili ya kuongeza mifugo kwenye eneo la Nile Magharibi katika mwaka wa fedha wa 2014 na 2015. Kwa mujibu wa Kamishna Ofisi ya waziri mkuu anaesimamia mipango ya mifugo Kaskazini mwa Uganda Gonzaga Mayanja, amesema asilimia 97% za fedha hizo zitatumika kwa ajili ya ununuzi wa mifugo na nyingine kwa gharama za uendeshaji . Mayanja amebainisha kuwa watoa huduma hizo tayari wamekwisha kusaini mikataba na ifikapo Januari mwakani ugawaji wa mifugo katika...
KAMPUNI ya simu za Mkononi ya Vodacom, imetangaza kumpata mshindi bora wa ubunifu wa program za simu kupitia shindano la AppStar linaloendeshwa na Kampuni hiyo. Kwa Mujibu wa Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Tanzania, Abigail Ambweni, kupitia program hiyo Mshindi wa kwanza atakwenda India kushiriki katika ngazi ya kimataifa. Mshindi kuyo ni Roman Mbwasi ambaye ameibuka kidedea katika shindano la kutafuta vipaji vya ugunduzi wa program za simu la AppyStar lililoandaliwa na kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania likiwa...
SHIRIKA la Junior Archvment kwa kushirikiana na Citi Benki wamewapongeza vijana wajasiriamali walioshinda katika shindano la bidhaa bora lililofanyika jijini Dar es salaam kwa lengo la kumtafuta mshindi wa bidhaa bora atakayewakilisha katika shindano la Ujasiriamali Afrika. Akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi kwa washindi watatu kati ya makundi 13 walioshiriki, mkurugenzi wa shirika lisilo la serikali la Junior archievement Maria Ngowi amesema shirika hilo limekuwa likidhaminiwa na CITI Benki ili kuweza kutoa mafunzo ya ujasiriamali...