IMEELEZWA kuwa vitendo vya Ukatili wa Jinsia kwa Watoto vimeongezeka katika Mkoa wa Dar es salaam katika kipindi cha January hadi September mwaka huu. Taarifa iliyotolewa na Chama Cha Waandishi wa Habari wanawake Tanzania-TAMWA imeeleza kuwa katika miezi tisa Pekee vitendo hivyo vimefikia 519. Zanzibar imeshika nafasi ya Pili kwa kuwa na ongezeko kubwa la vitendo vya ukatili wa Jinsia ikiwa na idadi ya 219, ikifuatiwa na Shinyanga 69, Mara 62,Tabora 55,Morogoro 36, Kagera 32 na Pwani...
Bingwa namba moja katika mchezo wa Tennis, Novak atawazwa kuwa mshindi wa michuano ya ATP World Tour Finals huko jijini London baada ya Roger Federer kushindwa kucheza mchezo wa fainali kutokana na maumivu ya mgongo. Federer aliyeshinda kwa seti 4-6 7-5 7-6(8-6) ndani masaa mawili na dakika arobaini na nane siku ya jumamosi dhidi ya Wawrinka ameomba radhi kutokana na kitendo hicho. Huu ni ubingwa wan ne kwa MSerbia Djokovic ikiwa ni mara yake ya tatu mfululizo kutwaa taji hilo...
Kiungo wa timu ya taifa ya Uholanzi na klabu ya Manchester United, Daley Blind anaweza kukaa nje ya uwanja kwa muda wa wiki sita baada ya kupata jeraha la goti katika mchezo wa kuwania kuingia michuano ya Ulaya mwaka 2016 huko nchini Ufaransa. Katika mchezo huo ambao timu ya Taifa ya Uholanzi iliibuka na ushindi mnono wa magoli 6-0 dhidi ya Latvia, Blind aliumia mnamo dakika ya 20 ya mchezo kwa kugongana na mchezaji Eduards Visnakovs. Kuumia kwa kiungo huyo...
HELIKOPTA ya kijeshi ya Nigeria imeanguka katika eneo la Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo , ikiwa ni Helikopta ya pili kupata ajali kwa muda wa chini ya wiki mbili . Ajali ya hivi karibuni imetokea katika viunga vya mji wa Yola, mji mkuu wa jimbo la Adamawa ambako kwa sasa jeshi linahangaika kukabiliana na Uasi wa wanamgambo wa Jihad. Kuna taarifa kutoka jimbo hilo kuwa wapiganaji wa Boko Haram wamekuwa wakiwasukuma wanajeshi nje ya mji muhimu uliopo karibu na mpaka...
RAIS BARACK OBAMA wa Marekani amesema kuna haja ya Mageuzi zaidi nchini Myanmar katika kuelekea kuipata Demokrasia. Akizungumza katika mji mkuu wa nchi hiyo Yangon leo, Rais OBAMA amekosoa jinsi watu wa dini za walio wachache wanavyotendewa na pia hatua ya kumzuia kiongozi wa upinzani, AUNG SAN SUU KYI, kutogombea Urais. SUU KYI aliyeachiwa huru miaka minne iliyopita baada ya kuwekwa kwenye kifungo cha nyumbani kwa takribani miongo miwili, sasa ni mjumbe katika Bunge la nchi hiyo, ingawa anashindwa kugombea...
WATANZANIA wametakiwa kuelekeza nguvu katika kuendeleza taaluma ya sayansi, tekinolojia na mawasiliano ili kuinua uchumi wa nchi kupitia ukuaji wa tekinolojia unaoendelea kwa kasi duniani. Hayo yamesemwa leo na Waziri wa mawasiliano sayansi na tekinolojia Profesa MAKAME MBARAWA alipokuwa mgeni rasmi katika mkutano wa kutathmini mafanikio ya miaka minne yatokanayo na mpango wa maendeleo ya tekinolojia kwa msaada wa serikali ya Italia. Aidha Profesa Mbarawa amesema katika kipindi hicho cha miaka mine, Tanzania imeshatengeneza wataalamu wengi...
BUNGE la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limepitisha Azimio kuhusu Tanzania kuridhia itifaki ya kuanzisha tume ya utafiti wa Afya katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa lengo la kuiwezesha Jumuiya kupata ushauri wa masuala ya kiafya hali itakayoimarisha huduma hiyo kwa wananchi. Akitoa Hoja rasmi ya Azimio hilo leo Bungeni mjini Dodoma Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dokta SEIF RASHID amesema umuhimu wa azimio katika utekelezaji wa Utafiti huo utakuwa katika kiwango cha kuridhisha katika...
MAREKANI na India zimesema zimepata muafaka juu ya mzozo uliohusu ruzuku ya chakula nchini India, ambayo mwaka jana ilikwamisha makubaliano ya kibiashara katika Shirika la Kimataifa la Biashara, WTO. India imekataa kutia saini makubaliano hayo muhimu Julai mwaka jana, ikitaka kwanza kuhakikishiwa hazina kubwa ya chakula nchini humo. Kulinagana na makubaliano yaliyofikiwa, hazina ya chakula ya India haitakabiliwa na changamoto zozote kutokana na kanuni za WTO, hadi pale suluhisho la kudumu kuhusu suala hilo litakapokuwa...
MVUA kubwa ya mawe iliyoambatana na upepo mkali imenyesha na kusababisha maafa katika Wilaya ya Bunda mkoani Mara ikiwa ni pamoja na watoto wawili kujeruhiwa na mmoja kuvunjika mkono kutokana na kuangukiwa ukuta wa nyumba. Katika tukio la kwanza Mvua ya mawe iliyoambatana na upepo mkali imenyesha katika kijiji cha Nyabehu Kata ya Guta ambapo watoto wawili wamejeruhiwa na mmoja kuvunjika mkono. Kwa mujibu wa Diwani wa Kata ya Guta MWITA MWANGIERA amebainisha kuwa Mvua imenyesha kwa zaidi ya saa...
NAIBU Waziri wa Ustawi wa Jamii Dokta STEVEN KEBWE amesema Tanzania ni nchi ya Nane kati ya nchi 10 zinazoongoza kwa kuwa na watu wanaougua sukari Barani Afrika. Dokta KEBWE ameeleza hayo alipokuwa akitoa tamko kuhusu siku ya Kisukari inayoadhimishwa leo Duniani. Amebainisha kuwa nchini Maadhimisho hayo yanafanyika yakiwa na Kauli Mbiu isemayo ULAJI UNAOFAA HUANZA NA MLO WA...
moja kati ya vitu ambavyo watu wengi wanaogopa duniani ni kusimama mbele ya umati alafu ukafanya kitu kinyume na taratibu zake yani ukakosea. basi hii ni orodha ya nyota wa dunia na matukio yao waliyowahi kukosea kwenye matamasha...