UTATA umetanda miongoni mwa wananchi nchini Marekani kutaka kujua ni askari yupi hasa aliyefyatua risasi iliyomuua Osama Bin Laden, zaidi ya miaka mitatu baada ya kifo cha kiongozi huyo wa kundi la kigaidi la al-Qaeda, baada ya kuibuka madai mbalimbali. Askari wa zamani wa kikosi cha Seal cha wanamaji wa Marekani, Robert O’Neill, mwenye umri wa miaka 38, ameliambia gazeti la Washington Post katika mahojiano mapya kuwa ndiye alifyatua risasi iliyomuua Osama. Maelezo hayo yanapingana na yale ya Matt Bissonnette,...
TAKWIMU zinaonyesha kuwa ukame umekuwa na madhara makubwa katika mji mkubwa nchini Brazil wa Sao Paulo. Dokta ANTONIO NOBRE ambaye ni Mtaalamu wa hali ya Hewa amesema vyanzo vya maji vinaweza kutoweka na kusababisha madhara kwa zaidi ya watu Milion 20 iwapo hali hiyo ya uharibifu katika msitu wa Amazon hautadhibitiwa. Baada ya kuwa ndani ya ukame kwa zaidi ya miaka nane mfululizo kina cha maji kwa sasa mjini Sao Paulo kipo katika hali ya hatari. Serikali nchini humo...
TANZANIA imesema ipo tayari kuendeleza juhudi za kimataifa za kupunguza kuendelea kuliwa kwa tabaka la ozone kwa kuhakikisha kwamba inatunza misitu na kuwaelimisha wananchi juu ya menejimenti ya misitu hiyo. Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Mazingira , Mheshimiwa Binilith Mahenge wakati wa kufungua kikao cha 13 cha wadau wanaotekeleza program ya kutunza misitu ya Umoja wa Mataifa kinachofanyika Ngurdoto mjini Arusha. Amesema ingawa Tanzania kwa sasa ina hekta milioni 48.1 za misitu...
SERIKALI ya Tanzania imesema imeshtushwa na Ripoti inayoelezea biashara haramu ya meno ya tembo kati ya baadhi ya viongozi wa nchi hiyo na China Serikali imesema imesikitishwa na ripoti iliyotolewa na taasisi ya uchunguzi ya mazingira inayodai kwamba majangili wa Kichina wakishirikiana na baadhi ya viongozi wa serikali ndio wanaoangamiza idadi ya tembo kutokana na biashara haramu ya meno ya tembo. Inadaiwa kwamba raia wa China walitumia ziara ya Rais wao nchini kusafirisha kimagendo maelfu ya kilo za pembe za...
Wachezaji wa Tennis Nchini watakutana mjini Arusha siku ya Jumamosi tayari kwaajili yamichuano ya kupandisha viwango vyao ilikujiwekatayari kwa mashindanombalimbali ya kimataifa Kocha wa mchezo huo Kiango Kipingu ameiambia E.sport kuwa wachezaji hao wanaianza safari yao leo kuelekea Arusha huku chama cha Tennis taifa kikiwakimegharamia safari hiyo...
Wanachama Yanga waibuka na kukosoa mfumo wakocha Mbrazil Maxio Maxmokuendelea kuwatumia wachezaji wa kigeni – Jaja na Countinhokatika kila mechi hatakamawachezaji haowanaonekana hawapo vizuri kimchezo Akizungumza na E.sport mwanachama aliyewahi kuwania nafasi ya Mwenyekiti klabu hiyo ya Jangwani John Jambele amesema mfumo huo wa kocha maximo pamoja nakuchelewa kufanyamaamuzi kubadilisha wachezaji kutokana na ugumu wamechi husika umechangia kupoteza mechi zao mbili tangu ilipoanzakutimuaVumbi Msemaji wa Yanga Baraka Kizuguto ameipinga kauli...
Kamati ya utendaji ya Klabu ya Simba imekutana jana kuzungumzia suala la Wachezaji watatu waliowasimamishwa kutokana naUtovu wa nidhamu, Lakini kikao hicho kimeshindwa kutoamajibu kuhusu hatima ya wachezaji hao Wachezaji hao ni pamoja na Shabani Kisiga, Haroun Chanongona, Amry Kiemba ambao wamesimamishwa mara baada ya mchezo wa kati ya Simba dhidi ya Tanzania prison uliopigwa katika dimba la Sokoine huko mkoani mbeya na timu hizo kwenda sare ya kufunganabao 1-1 Msemaji wa Simba Hamphrey Nyasio, Amezungumza na E.sport na kuthibitisha...
CECAFA yakuna kichwa kumpata mwenyeji wa mashindano ya Challenge mwaka huu ni baada ya Ethopia kujitoa dakika ya mwisho Afisa habari wa CECAFA Rodgers Mulindwaalipozungumza n E.sport kutoka mjini Kampala nchini Uganda amesema baraza hilo kwa sasa lipo katika mazungumzo mazito na nchi YaSudani kuona uwezekano wakubeba jukumu hilo la uenyeji wa challenge...
RAIS BARACK OBAMA wa Marekani ameliomba Bunge la nchi hiyo Dola Bilioni 6 nukta 2 kwa ajili ya Mfuko wa Dharura wa kupambana na maradhi ya Ebola katika eneo la Magharibi mwa Afrika, na kuzuia uwezekano wa Ugonjwa huo kusambaa hadi Marekani. Sehemu ya mfuko huo Dola Bilioni Mbili zinatarajiwa kukabidhiwa kwa Shirika la Marekani la Msaada wa Kimataifa – USAID, huku Dola Bilioni 2 nukta 4 zikienda Idara ya Afya na Huduma za Binadamu nchini humo. Taarifa zaidi zimebainisha...
WASIMAMIZI wa Vyuo Vikuu nchini Kenya wameagizwa kufungua Mitandao ya Twitter na Facebook ambayo wanafunzi watatumia kutoa malalamiko yao kwa lengo la kuzuia machafuko katika Taasisi hizo. Waziri wa Elimu nchini Kenya JACOB KAIMENYI amesema kuwa vifaa hivyo vya mawasiliano vitawasaidia wanafunzi kutoa malalamiko yao mbali na kupata majibu kutoka kwa Wasimamizi. Waziri KAIMENYI ameshtumu mbinu zinazotumiwa na Vyuo Vikuu kukandamiza upinzani mbali na kudhibiti masuala ya wanafunzi kama vile Uchaguzi wao na kuwasingizia katika masuala ya utovu wa...
JAMII imetakiwa kushirikiana na serikali kutoa taarifa za wanafunzi wanaopata ujauzito wakiwa shuleni. Wito huo umetolewa na Katibu mkuu Wizara ya Elimu Dokta SIFUNI MCHOME wakati akizungumza na EFM na kusema kuwa hali hiyo itasaidia kujua idadi ya wanafunzi ambao hawahudhurii masomo pamoja na kuwachukulia hatua wahusika wakuu waliosababisha tatizo. Amebainisha kuwa watoto wa kike wanatakiwa kupewa Elimu juu ya masuala ya Uzazi ili iweze kuwasaidia katika kujitambua pamoja na kuepuka kupata Mimba wakiwa Shuleni....