MKUU wa Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es salaam Mh. Ally Hapi leo amewatembelea wananchi maeneo ya Bunju na Mbweni waliokuwa na kero mbalimbali. Katika eneo la Bunju Kilungule, baadhi ya wananchi nyumba zao zimezungukwa na maji kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha. Akijibu maombi ya wananchi hao, Mheshimiwa, Hapi amewaagiza mainjinia wa manispaa kuhakikisha kuwa wanafanya utaratibu wa kupata pampu kubwa ya kuvuta maji hayo, huku akiwataka wananchi kuwa wale wote waliojenga katika eneo hatarishi ambalo ramani inaonesha kuwa ni eneo...
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dokta John Pombe Magufuli, ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania-TIC, Bi Juliet Kairuki. Kwa mujibu wa Taarifa kwa vyombo vya Habari iliyotolewa leo na kusainiwa na Katibu Mkuu, Biashara na Uwekezaji, Profesa Adolf Mkenda, Uteuzi wa Bi Kairuki umetenguliwa kuanzia April 24 mwaka huu. Taarifa hiyo imeeleza kuwa, hatua hiyo imechukuliwa na Mheshimiwa Rais baada ya kupata taarifa kwamba Mkurugenzi huyo amekuwa hachukui mshahara wa Serikali tangu alipoajiriwa mwezi April...
MGOMO wa wafanyakazi wa sekta ya umma umevuruga shughuli za kawaida nchini Ujerumani hii leo. Wanachama wa chama cha wafanyakazi wa sekta ya umma Verdi wamegoma kufanya kazi kutokana na madai ya nyongeza ya mshahara. Viwanja vya ndege vya Frankfurt, Dusseldorf na Munich vimeathirika na mgomo huo ikiwa ni pamoja na usafiri wa mjini katika miji mbali mbali, lakini uwanja wa ndege wa mjini Berlin unafanyakazi kama ...
SALAH ABDESLAM , anayetuhumiwa kuchukua nafasi ya juu katika mashambulizi ya mjini Paris ambayo yamesababisha watu 130 kuuwawa, anafikishwa mahakamani nchini Ufaransa leo, kwa mtazamo wa kuwekwa chini ya uchunguzi rasmi. Hatua hiyo inakuja baada ya Abdeslam kupelekwa nchini Ufaransa kutoka Ubelgiji mapema leo Jumatano. Mtuhumiwa huyo aliwasili nchini Ufaransa mapema leo...
IMEBAINISHWA kuwa kwa mwaka 2012/2015 kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom imechangia zaidi ya shilingi bilioni 3 katika pato la taifa ambayo ni sawa na asilimia 2 ya pato la Tanzania. Hayo yamebainishwa leo jijini Dar es Salaam katika tathmini iliyofanywa na KPMG juu ya mchango mpana wa kiuchumi na kijamii ikiwamo ukuzaji wa uchumi,ajira,na kupunguza umaskini,tathmini iliyofanyika kuhusu mtaji na shughuli za uwekezaji kwa kipindi cha mwaka wa fedha wa 2012/...
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dokta John Pombe Magufuli, amewaapisha Maafisa Tawala wapya kumi aliowateua April 25, mwaka huu na kuwapangia vituo vyao vya kazi. Makatibu Tawala hao wapya, wameapishwa leo Ikulu jijini Dar es salaam na kuweka saini ya ahadi ya uadilifu kwa Viongozi wa Umma, Zoezi lililoendeshwa na kamishna wa maadili Sekretarieti ya maadili ya Viongozi wa Umma, Mheshimiwa Jaji Salome Kaganda mbele ya Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John...
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limemteua Alfred Lucas kuwa Afisa Habari na Mawasiliano mpya wa shirikisho kuanzaia leo Aprili 27, 2016. Alfred anachukua nafasi ya Baraka Kizuguto aliyehamishiwa katika Kurugenzi ya Mashindano kuwa Afisa Mashindano na Meneja wa Mifumo pepe ya Usajili (TMS). Alfred ana uzoefu kutoka vyombo mbalimbali alivyovitumikia kama mwandishi wa habari na mhariri.Kadhalika Alfred kitaaluma amesomea uandishi wa habari, uhusiano wa kimataifa na diplomasia pamoja na...
Timu ya Taifa ya Tanzania inatarajiwa kucheza mchezo wa kirafiki wa kimataifa na timu ya Taifa Kenya Mei 29, jijini Nairobi. Mchezo huo utachezwa jijini Nairobi Mei, 29 mwaka huu, ikiwa ni sehemu ya maandalizi kwa timu zote mbili kujiandaa na michezo ya kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa Afrika mwezi Juni, 2016 ambapo Taifa Stars itacheza dhidi ya Misri Juni 04, mwaka huu katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. TFF kwa kushirkiana na FKF zimekubaliana kuwepo kwa...
NCHINI Marekani, tajiri Donald Trump amesema kuwa anajihisi sasa kama mgombea mteule wa urais wa chama cha Republican. Amesema hayo alipokuwa akiwahutubia wafuasi wake baada ya vyombo vya habari kutangaza kuwa amepata ushindi katika majimbo yote matano kaskazini mashariki mwa Marekani. Katika shughuli za upigaji kura wa mchujo kwenye majimbo hayo, mtafuta nafasi katika chama cha Democratic Bi Hillary Clinton alimpiku muwaniaji mwenzake Bernie Sanders, ambaye alishinda katika jimbo moja tu la Rhode...
SERIKALI ya Venezuela imebuni mikakati ambayo itapelekea wafanyakazi wapatao milioni mbili wa serikali, kufanya kazi kwa siku mbili pekee kwa wiki katika kipindi cha majuma mawili. Hatua hii inalenga kusaidia kukabiliana na uhaba wa umeme ambao unayumbayumba nchini humo. Wafanyakazi hao wa umma na wale wanaofanya kazi katika sekta zinazomilikiwa na serikali watafika kazini siku za Jumatatu na Jumanne pekee hadi matatizo hayo ya nguvu za umeme...
WANANCHI katika halmashauri zote mkoani mara wametakiwa kushiriki katika kuchAngia maendeleo na kuachana na dhana zinazoendelezwa na baadhi ya viongozi katika serikali wanaotoa kauli zakuwapinga wananchi kuchangia maendeleo ya elimu na kulitumia vibaya neno Elimu bure. Yamesemwa hayo na mwenyekiti wa halmashauri ya BUTIAMA Magina Magesa alipokuwa akizungumza katika uhamasishaji wa kuchangia maendeleo ya elimu hususani ujenzi wa maaabara na madawati katika wilaya hiyo ....