WATU 43 wameuawa katika kipindi cha siku tano zilizopita kutokana na kimbunga maeneo ya kusini na magharibi mwa Marekani. Mafuriko, upepo mkali na barafu vimeharibu mamia ya nyumba na biashara na hivyo kuyumbisha shughuli za uchukuzi. Idara ya taifa ya utabiri wa hali ya hewa nchini humo imetoa tahadhari ya kutokea kwa vimbunga katika majimbo ya Texas, Arkansas, Louisiana, Oklahoma and...
WATU wawili wamefariki na wengine watatu kujeruhiwa baada ya wanajeshi kufyatulia risasi gari moja mjini Mandera katika hali ya kutatanisha. Wanajeshi wamekuwa wakifanya operesheni kali mjini humo baada ya kuripotiwa kwa visa kadha vya mashambulio ya kigaidi siku za hivi karibuni. Maafisa wanne wa polisi wameuawa kwenye mashambulio kadha katika mji huo ulioko kaskazini mashariki mwa Kenya katika kipindi cha wiki...
WAZIRI Wizara ya Maliasili na Utalii Mhe. Prof. Jumanne Maghembe amewasili wizara kwake leo mara tu baada ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ikulu Jijini Dar es salaam. Waziri Profesa Maghembe ni miongoni mwa Mawaziri wanne walioteuliwa hivi karibuni na rais kukamilisha baraza jipya la Mawaziri katika Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dokta John Pombe Magufuli. Kufuatia hafla hivyo, hivi sasa Wizara zote zimekamilika kwa ajili ya utekelezaji wa kauli mbiu ya awamu hii ya...
AKINAMAMA wajawazito na watoto katika hospitali ya wilaya ya maswa Mkoani Simiyu, wamekuwa wakilazimika kulala kitanda kimoja watu wawili na muda mwingine kupeana zamu kutokana na ufinyu wa wodi, na upungufu wa vitanda suala ambalo linaweza kusababisha maambukizi ya magonjwa. Kufuatia hali hiyo, wakizungumza na Efm wameiomba serikali kuyafungua majengo mapya ambayo tayari yameshakamilika ili kuweza kupunguza adha hiyo. Kituo hiki kimeshuhudia akinamama hao wakiwa wamelala wawili wawili wodini, huku baadhi...
Taarifa kutoka Yemen zinasema aliyekuwa mlinzi wa Osama Bin Laden, amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu. Vyanzo vya habari vya kitabibu vinaeleza kwamba Nasser al Bahri ambaye pia alikuwa akijulikana kama Abu Jandal alifariki siku ya Jumamosi, katika Hospitali iliyoko kwenye mji wa Mukalla kusini mwa Yemen. Alirudi nchini humo mwishoni mwa mwaka 2008, baada ya kuachiliwa kutoka katika kizuizi alichowekewa na Marekani huko...
MAZUNGUMZO ya kusuluhisha mzozo wa Burundi yataanza tena leo mjini Kampala, chini ya usimamizi wa rais Yoweri Museveni wa Uganda. Rais Museveni aliteuliwa na Jumia ya Afrika Mashariki kuongoza mchakato wa amani ya Burundi, kufuatia machafuko yaliozushwa na uamuzi wa rais Pierre Nkurunziza kupigania muhula wa tatu, kinyume cha maana ya mapatano ya Arusha na katiba ya Burundi inayoruhusu mihula miwili. Baada ya kuzinduliwa rasmi mjini Kampala leo, mazungumzo hayo yatahamishiwa Arusha...
WAZIRI wa wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye amekanusha taarifa ambazo kwa takribani siku mbili zilizopita zilienea juu ya katazo rasmi la mavazi ya nguo fupi ambalo ilisemekana limetolewa na Wizara hiyo. Akizungumza na EFM kwa njia ya simu, Mheshimiwa Nnauye amesema Wizara imesikitishwa na Taarifa hizo na kwamba sheria zinazosimamia makosa ya kimtandao ziko wazi, hivyo anaamini mamlaka zinazohusika zitatekeleza wajibu...
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dokta John Pombe Magufuli amewaapisha mawaziri wapya wanne na Naibu waziri mmoja aliowateua Tarehe 23 Desemba, mwaka huu. Mawaziri hao wapya ni Waziri wa Maliasili na Utalii Profesa Jumanne Maghembe, Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Gerson Lwenge, Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Dkt. Joyce Ndalichako na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mheshimiwa Hamad Yusuf Masauni. Rais Magufuli pia alifanya uhamisho wa Waziri mmoja ambaye ni...
Arsenal yaanza mazungumzo kumwaga wino na kiungo wa Basel Mohamed Elneny Mchezaji huyo wa Egypt, 23 alijiunga na klabu ya Uswiz mwaka 2013, na kushinda mataji ya ligi ya katika misimu yake mitatu Kiasi cha pound milioni tano kinatajwa kuwa ada ya usajili kwa mchezaji huyu ambae atahitajika kupatiwakibali cha kazi. Moja ya rekodi bora kwa nyota huyu ni ushindi wa nyumbani akiwa na klabu yake ya Basel dhidi ya Chelsea katika michuano ya mwaka 2013-14 Meneja...
Wachezaji wa Manchester United wanajitahidi kwa kila hali kunusuru kibarua cha Van Gaal, kauli ya Carrick Kiungo wa klabu ya Manchester United Michael Carrick amesema kuwalaumu wachezaji wa klabu hiyo kuwa hawaonyeshi juhudi za kutosha kwa meneja wa klabu hiyo Louis van Gaal ni kukosewa heshima. Carrick ameongeza kuwa kauli hizo zinazokuja kufuatia kufanya vibaya kwa klabu yao zinawaumiza kwa sababu hawapo tayari kuona meneja wao anakuwa kwenye wakati mgumu, hatuwezi kuficha tupo kwenye hali mbaya na tunahitaji kutoka kwenye...
Kituo bora cha radio 2015 E-fm leo kimekabidhi zawadi ya makapu yaliyosheheni bidhaa za vyakula kuelekea sikukuu ya Christmas Zoezi hili liliwataka wasikilizaji wa E-fm kusikiliza mlio wa Jingle Bells uliokuwa ukizunguka kwenye vipindi tofauti kisha kutambua muda ambao mlio huo umesikika, jina la kipindi husika na mtangazaji/watangazaji wa zamu waliokuwa studio muda huo. Akizungumza mara baada ya kukabidhi makapu hayo kwa washindi Meneja wa vipindi E-fm Bwana Dickson Ponela (Big Dad Dizzo) ameeleza kuwa, E-fm imekuwa ikishirikisha wasikilizaji...