RAIS MAGUFULI ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KWA SPIKA WA BUNGE KUFUATIA KIFO CHA SPIKA MSTAAFU, SAMWEL SITTA
Slider

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa dokta John Pombe Magufuli amemtumia salamu za rambirambi Spika wa Bunge la Tanzania Mheshimiwa Job Ndugai kufuatia kifo cha Spika mstaafu na Mbunge Mstaafu wa Jimbo la Urambo mkoani Tabora Samwel Sitta. Samwel Sitta amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika hospitali ya Technical University of Munich nchini Ujeruman alikokuwa akipatiwa matibabu tangu mwezi uliopita. Katika salamu hizo Rais Magufuli amesema amepokea kwa mshituko na masikitiko taarifa hizo na kwamba Taifa limempoteza...

Like
446
0
Monday, 07 November 2016
MADINI MAPYA YAGUNDULIWA MERERANI, TANZANIA
Slider

Madini mapya yamegunduliwa nchini Tanzania, katika eneo lenye madini ya kipekee la Manyara, na kupewa jina Merelaniite. Jina hilo limetokana na eneo ambalo madini hayo yalipatikana, Merelani (Mererani) katika milima ya Lelatema katika wilaya ya Simanjiro katika eneo la Manyara. Eneo hilo linafahamika sana kwa madini ya Tanzanite. Madini hayo yaligunduliwa na wataalamu kutoka Chuo Kikuu cha Kiteknolojia cha Michigan cha Marekani, makavazi ya historia asilia ya London, chuo kikuu cha Di Firenze cha Italia na makavazi ya historia asilia...

Like
367
0
Wednesday, 02 November 2016
MGOMO WAPELEKEA CHUO CHA MAKERERE KUFUNGWA
Slider

Wanafunzi wameanza kuondoka kutoka Chuo Kikuu cha Makerere baada ya Rais Yoweri Museveni kutangaza kifungwe mara moja Jumanne jioni. Rais alisema amechukua hatua hiyo “kuhakikisha usalama wa watu na mali.” Chuo kikuu hicho kilikuwa kimekumbwa na vurugu kutokana na mgomo wa wahadhiri na wanafunzi. Chama cha wahadhiri Jumatatu kiliamua kuendelea na mgomo hadi wahadhiri walipwe marupurupu ya miezi minane ambayo yamefikia Sh32bn (dola 9.2 milioni za Marekani). Wanafunzi walijiunga na mgomo Jumanne, na walitaka kukutana na Rais Museveni...

Like
324
0
Wednesday, 02 November 2016
MFALME MTEULE WA THAILAND KUTHIBITISHWA DECEMBER
Slider

imetaarifiwa kwamba mfalme mteule mtarajiwa wa Thailand Vajiralongkorn atathibitishwa rasmi kama mfalme ajaye mnamo Desemba mosi. Mwana wa mfalme huyo ambaye pia ni mfalme mtarajiwa alitarajiwa kupakwa mafuta na kutawazwa katika kipindi ama baada ya maziko ya babake , mfalme King Bhumibol Adulyadej, aliyefariki wiki tatu zilizopita, kutokana na yeye mwenyewe kuomba muda wa kumuomboleza babake. Mpaka sasa haijafahamika wazi, ni uhusiano wa namna gani mfalme huyo mtarajiwa atakuwa nao baina yake na vikosi vya jeshi la serikali ambavyo hivi...

Like
206
0
Wednesday, 02 November 2016
TAPELI ATUMIA SAUITI FEKI YA MAKONDA KUWALIZA WACHINA
Slider

Raia wa China wametapeliwa fedha taslimu Sh22.8 milioni wakidai kuwa sauti waliyoisikia kwenye simu ya kiganjani iliyotumiwa na tapeli ilifanana na ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda. Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Simon Sirro alisema jana ofisini kwake kuwa Oktoba Mosi, mwaka huu mfanyakazi wa Kampuni ya Group Six ambaye ni raia wa China, Marco Li (24) alipigiwa simu na mtu aliyejitambulisha kuwa ni Makonda. Sirro alisema tapeli huyo alimtaka raia...

Like
266
0
Tuesday, 01 November 2016
RAIS MAGULI: KENYA NI MSHIRIKA WETU MKUBWA AFRIKA
Slider

Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli amesema kuwa Kenya ndio mshirika nambari moja wa Tanzania katika uwekezaji na biashara barani Afrika. Akizungumza katika ikulu ya rais jijini Nairobi mda mfupi baada ya kuwasili nchini Kenya,Rais Magufuli amesisitiza kuwa hakuna taifa jingine ambalo limewekeza nchini mwake kama Kenya. Amesema kuwa kulingana na rekodi za uwekezaji nchini Tanzania kuna takriban kampuni 529 nchini humo kutoka Kenya ambazo zinaingiza takriban dola bilioni 1.7 kila mwaka huku takriban Watanzania 57,260 wakiwa wameajiriwa. Rais...

Like
271
0
Monday, 31 October 2016
ITALIA: MAELFU YA WAKAAZI WALALA NJE KUFUATIA KIMBUNGA KIKALI
Slider

Maelfu ya watu katikati mwa Italia wamelala katika magari na mahema ikiwa ni kama makazi ya muda mfupi baada ya kimbunga kikali kupiga katika eneo hilo tokea kile cha mwezi Agosti. Wakaazi katika eneo lililoathirika zaidi la Norcia wamesema walikuwa na hofu sana kuendelea kukaa ndani mwa nyumba zao. Takriban watu 20 wamejeruhiwa na kimbunga hicho kilichotokea siku ya Jumapili, lakini inasemekana mtu mmoja amepoteza maisha. Mkuu wa eneo hilo Luca Ceriscioli amesema zaidi ya watu laki moja watahitaji...

Like
211
0
Monday, 31 October 2016
GARETH BALE AMWAGA WINO KUENDELEA KUKIPIGA REAL MADRID
Slider

Real Madrid imemsainisha mkataba mpya winga wake Gareth Bale na kumfanya aendelee kudumu klabuni hapo mpaka 2022. Bale mchezaji wa zamani wa Southampton alijiunga na klabu hiyo akitokea Tottenham Hotspur mwaka 2013. Tiyari ameisaidia Madrid kushinda vikombe vitano katika misimu mitatu ya nyuma ikiwemo ligi ya mabingwa Ulaya mara 2 huku akifunga magoli 62 katika michezo 135. Viungo wawili wa timu hiyo Luka Modric na Toni Kroos nao pia walisaini mikataba mipya mwezi huu. Mkataba wa Bale unatajwa kuwa wa...

Like
236
0
Monday, 31 October 2016
AHEL YAILIZA NSSF BIL. 270
Slider

Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) limekiri kuingia mkataba wa ujenzi wa mji wa kisasa wa Dege Eco Village, Kigamboni na kampuni ya Azimio Housing Estates (AHEL) ambayo haikuwa na mtaji hali iliyolazimu kusitisha mradi huo huku likihofia kupata hasara ya Sh270 bilioni. Machi mwaka huu, Mwananchi liliandika “NSSF yaliwa mchana kweupe” likifafanua ufisadi katika mradi huo na mingine ya Mwanza, Pwani, Mtwara na Arumeru, Arusha ambako ekari moja ya ardhi ilithaminishwa kwa Sh1.8 bilioni. Jana, Mkurugenzi Mkuu...

Like
303
0
Thursday, 27 October 2016
WATUMISHI 10 WATIMULIWA MVOMERO
Slider

Watumishi 10 wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro, wamefukuzwa kazi kutokana na makosa mbalimbali yakiwamo ya ubadhirifu wa fedha na utoro kazini. Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Florent Kyombo alisema jana kwamba watumishi hao wamefukuzwa kutokana na kushindwa kusimamia ukusanyaji wa mapato, utoro na uzembe. Kyombo alisema watumishi hao wamefukuzwa kwa kuzingatia kanuni na utaratibu wa utumishi wa umma kwenye vyombo husika na kuidhinishwa na vikao vya...

Like
254
0
Thursday, 27 October 2016
MAN UTD YAINYOA MAN CITY
Slider

Manchester United walifika hatua ya robo fainali katika Kombe la EFL baada ya kuwalaza mabingwa watetezi Manchester City kwenye debi iliyochezewa uwanja wa Old Trafford. Juan Mata alifunga bao la pekee mechi hiyo baada ya kupata mpira kutoka kwa mshambuliaji Zlatan Ibrahimovic. Paul Pogba alikuwa amegonga mlingoti kwa kombora kali awali na kusisimua mechi hiyo kipindi cha pili. Kipindi cha kwanza kilikuwa kikavu bila upande wowote kupata kombora la kulenga goli. Manchester United sasa watakutana na West Ham ambao waliwalaza...

Like
208
0
Thursday, 27 October 2016
« Previous PageNext Page »