SERIKALI imesema kuwa takwimu sahihi zinahitajika katika kufuatilia utekelezaji wa malengo ya maendeleo Endelevu. Hayo yameelezwa na mwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika umoja wa Mataifa Balozi Tuvako Manongi wakati wa mkutano wa 49 wa kamisheni ya Umoja wa Mataifa kuhusu idadi ya watu na maendeleo. Balozi Manongi...
KIONGOZI wa waasi nchini Sudan Kusini, Riek Machar, amerejea nchini humo kwa mara ya kwanza katika kipindi cha zaidi ya miaka miwili kama sehemu ya utekelezwaji wa mkataba wa amani. Atakapowasili mjini Juba, Bwana Machar anatarajiwa kuchukua wadhfa wake wa makamu wa rais. Msemaji wake amethibitisha kwamba bwana Machar alikuwa katika makao makuu ya waasi yaliyo katika mji wa Pagak mpakani na taifa jirani la...
ASKOFU msitaafu wa Jimbo Katoliki la Dodoma, Mhashamu Askofu Mathias Joseph Issuja, amefariki dunia. Askofu isuja ambaye alizaliwa mwaka 1929 alipata daraja hilo Takatifu mwaka 1972 ambapo aliwekwa wakfu na Hayati Kardinali Laurean Rugambwa na kustaafu mwaka 2005 akiwa Askofu wa Jimbo la Dodoma. Efm imezungumza kwa njia ya simu na Katibu mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania-TEC, Padri Raymond saba ambaye amesema kuwa Askofu mstaafu Issuja, amefariki usiku wa kuamkia leo huko katika Hospitali ya...
WAZIRI wa Nchi ofisi ya makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mheshimiwa January Makamba amekutana na kufanya mazungumzo na ujumbe wa kamati ya fedha ya Bunge la Finland. Katika mazungumzo yao yaliyofanyika leo Jijini Dar es salaam, wabunge hao wameipongeza serikali ya Tanzania kwa jitihada inazozifanya za kulinda na kuhifadhi mazingira. Awali akiwakaribisha wabunge hao, Waziri Makamba amesema Tanzania inajivunia uhusiano bora uliopo baina yake na Finland na kuwashukuru wabunge hao kwa kufanya ziara yao...
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, amewataka watanzania wote kutambua kwamba mafanikio na maendeleo yoyote ndani ya jamii na Taifa kwa ujumla hayawezi kupatikana endapo wanawake hawataweza kushirikishwa kikamilifu kwenye vikao vya maauzi. Mheshimiwa Samia ameyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza kwenye ufunguzi wa kongamano la wanawake katika uongozi lililoandaliwa na taasisi ya uongozi na kuwakutanisha wanawake wa kitanzania wenye nyadhifa mbalimbali za uongozi nchini....
JESHI La Magereza nchini na Jeshi la Kujenga Taifa wamepewa jukumu la kutengeneza madawati yenye thamani ya shilingi Bilioni 6 ambayo yatasambazwa katika Mikoa yote ya Tanzania Bara na Zanzibar. Jukumu hilo kwa Vyombo vya Ulinzi na Usalama limetolewa jana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika hafla fupi ya makabidhiziano ya mfano wa hundi ya shilingi Bilioni 6 kutoka Sekretarieti ya Bunge ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania fedha ambazo zimepatikana kufuatia...
WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mheshimiwa Ummy Mwalimu leo amezindua rasmi taasisi ya Basilla Mwanukuzi BMF-yenye lengo la kushirikiana na Wadau ili kuwawezesha Wanawake kiuchumi. Hafla hiyo ya uzinduzi imeenda sanjari na uzinduzi wa mradi wa “Wezesha mama lishe Tanzania” ukiwa na lengo la kuwawezesha mama lishe kupata elimu ya ujasiriamali na upikaji wa chakula bora chenye kuzingatia virutubisho. Akizungumza katika hafla hiyo Waziri Mwalimu amesema kuwa wengi waliopo katika sekta ya mama lishe ni...
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dokta John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mama Anna Kilango Malecella kwa kubaini kuwa alimwambia uwongo kuwa Mkoa wake hauna wafanyakazi hewa wakati wapo wengi. Rais Magufuli amesema kwamba hakuamini kwamba kuna mkoa ambao hauna wafanyakazi hewa, hivyo akatuma kikosi kazi ambacho hadi usiku wa kuamkia leo kimebaini kuwepo kwa wafanyakazi hewa 45 mkoani Shinyanya. Akizungumza baada ya kupokea Ripoti ya TAKUKURU kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru...
SERIKALI nchini imetakiwa kuzingatia kasi ya ongezeko la idadi ya watu katika mipango yake ya maendeleo ikiwemo uwekaji wa mikakati bora na uboreshaji wa sera ili kuweka uwiano sahihi kati ya ongezeko la watu na maendeleo ya Taifa. Hayo yamebainishwa jana Jijini Dar es salaam na wajumbe na mabalozi wa kikundi kazi kinachoundwa na wadau na watetezi wa masuala ya uzazi wa mpango na idadi ya watu-TCDAA– ambapo kwa upande wa mwakilisi mwandamizi wa kikundi kazi hicho Bi. Halima...
WAZIRI MKUU wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa, Kassim Majaliwa amemtaka Mkuu wa Magereza mkoa wa Lindi, kuhakikisha hakuna mtuhumiwa wa dawa za kulevya atakayetoweka katika gereza la mkoa huo. Amesema kuna watuhumiwa wa dawa za kulevya ambao wanahifadhiwa katika gereza hilo, hivyo ni vema akajiridhisha kama ulinzi na usalama wa watuhumiwa hao umeimarishwa. Waziri Mkuu, Majaliwa ameyasema hayo wilayani Ruangwa wakati akipokea taarifa ya maendeleo ya mkoa wa Lindi iliyowasilishwa kwake na Mkuu wa mkoa huo, Godfrey...
WADAU wa Maendeleo ya Elimu nchini wameshauriwa kutoa vifaa vya kujifunzia na kufundishia kwa walimu na wanafunzi wa shule mbalimbali nchini ili kukuza kiwango cha elimu nchini. Aidha wameshauriwa pia kuboresha miundombinu ya shule hali ambayo itaboresha pia mazingira ya kujifunzia. Ushauri huo umetolewa na Mbunge wa Segerea Bonna Kaluwa mara baada ya kukabidhi msaada wa kompyuta kwenye shule ya sekondari ya Binti Mussa iliyopo Manispaa ya Ilala Jijini Dar Es Salaam. ...