CHAMA cha Mapinduzi-CCM-mkoa wa Kigoma kimewafukuza wanachama wake 25 baada ya kukisaliti chama wakati wa Uchaguzi mkuu uliofanyika oktoba 25 mwaka jana. Akitoa taarifa kwa vyombo vya Habari, Katibu wa chama hicho mkoa wa Kigoma Naomi Kapambala amesema kuwa uamuzi huo umetolewa katika kikao cha Halmashauri kuu ya Chama kilichofanyika machi 2 mwaka huu. Naomi amesema baada ya kufanyika kwa Uchaguzi mkuu chama kilianza kufanya tathimini na changamoto walizokutana nazo wakati wa Uchaguzi na kugundua kuwa wanachama hao ni miongoni...
RAIS wa Jamhuri ya Kisoshalisti ya Vietnam Truong Tan Sang anatarajiwa kufanya ziara rasmi Tanzania tarehe 9 Machi mwaka huu na kufanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania dokta John Pombe Magufuli Ikulu Jijini Dar es salaam. Madhumuni ya ziara hiyo ni kukuza uhusiano baina ya Vietnam na Tanzania ambao umedumu kwa zaidi ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwake pamoja na Kufungua maeneo mapya ya Ushirikiano wa kiuchumi baina ya Tanzania na Vietnam. Hiyo ni ziara ya...
UTABIRI wa Hali ya Hewa kwa mvua za masika zinazoanza wiki hii nchini umeonesha kuwa zitakuwa za wastani hadi juu ya wastani katika maeneo mengi ya nchi huku baadhi ya maeneo zikiwa chini ya wastani. Hayo yamesemwa jana Jijini Mwanza na Mkurugenzi mkuu wa malaka ya Hali ya Hewa Tanzania dokta Agnes Kijazi ambapo amesema katika maeneo ya ukanda wa ziwa Viktoria, Nyanda za juu, Kaskazini Mashariki pamoja na maeneo machache ya mkoa wa Tanga mvua zitanyesha hadi juu...
WAZIRI MKUU wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mheshimiwa Kassim Majaliwa ameiagiza Kamati ya Uchumi ya Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi ikutane na wafanyabiashara wote ili wajadiliane na kupanga kiwango cha ushuru kinachopaswa kutozwa kwenye mazao ya wilaya hiyo. Waziri Mkuu ametoa agizo hilo jana wakati akizungumza na mamia ya wananchi waliofika kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa michezo wa Dutwa Wilayani Bariadi mkoani Simiyu. Waziri mkuu Majaliwa mefikia uamuzi huo baada ya kuona bango lililoshikwa...
WAZAZI na Walezi nchini wametakiwa kutoa taarifa kwenye mamlaka husika juu ya vitendo vya ukatili vinavyofanywa na ndugu au wanafamilia dhidi ya watoto wa kike na hata wa kiume ili wachukuliwe hatua. Akizungumza na Efm Mwanasheria Msaidizi wa Jaji kutoka Chama cha Majaji Wanawake Tanzania-TAWJA-Koku Mwanemile ameeleza kuwa kufumbia macho vitendo hivyo kunachangia kuongezeka kwa matukio ya unyanyasaji kwa watoto. Koku amebainisha kuwa endapo wazazi, walezi na jamii wataungana pamoja kwa kufichua vitendo hivyo vinavyosababisha athari kubwa kwa...
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano na Mazingira, January Makamba ameitaka kamati ya kitaifa ya matumizi salama ya bioteknolojia ya kisasa kutengeneza mpango kazi utakaosaidia kuharakisha shughuli zao za kuisaidia serikali. Makamba ametoa wito huo wakati akizindua kamati hiyo mpya katika Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Mikocheni (MARI) jijini Dar es Salaam. Makamba amesema kamati hiyo ni muhimu katika utoaji wa maamuzi kuhusu masuala ya matumizi salama ya bioteknolojia ya kisasa na kukuza uelewa kwa wajumbe...
BENKI ya Bacley’s Tanzania imekanusha taarifa ambazo sio sahihi juu ya kusitishwa kwa huduma zake kwa madai kuwa Benki hiyo imeuzwa kwa nchi za Afrika. Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijni Dar s salaam jana wakati wa kutoa ripoti ya Benki hiyo kwa kipindi cha mwaka mmoja kwa niaba ya mkurugenzi mkuu wa benki hiyo, mkuu wa idara ya masoko wa Bacley’s JOE BENDERA amesema kuwa Benki hiyo inaendelea kutoa huduma kwa wateja wake kwa ufasaha na inaendelea kuboresha zaidi....
JAMII nchini imeombwa kuwasaidia watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi ili kupunguza vitendo vya ukatili wanavyofanyiwa watoto hao. Hayo yamebainishwa Jijini Dar es Salaam na Afisa Ustawi wa jamii Neema Mambosho wakati alipokuwa akizungumza na E FM juu ya ongezeko la watoto wa mtaani. Amesema kuwa watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi wanakabiliwa na changamoto mbalimbali za ukatili na kunyanyapaliwa hivyo jamii inapaswa kuelimishwa ili kuzuia vitendo...
MAMLAKA ya Mapato Tanzania-TRA-kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi imefanya ukaguzi wa stempu za kodi kwenye kazi za wasanii na kufanikiwa kukamata CD na DVD za Muziki na filamu 7, 780 ambazo hazina stempu za kodi. Mkurugenzi wa huduma na Elimu kwa mlipa kodi Richard Kayombo ameyasema hayo jana alipokuwa akizungumza na waandishi wa Habari ofisini kwake. Kayombo amesema kuwa msako huo ulioanza Februari 26 katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Dar es salaam umebaini ukiukwaji wa sharia kutoka kwa...
JUMLA ya Wagonjwa wapya 473 wamegundulika kuwa na vimelea vya Ugonjwa wa kipindupindu huku Watu 9 wakipoteza maisha kutokana na ugonjwa huo katika kipindi cha wiki iliyoanza Februari 22 hadi 28 huku ripoti ikionesha kuwa ugonjwa huo bado umeendelea kusambaa kwa kasi. Akizungumza na Wanahabari Jijini Dar es salaam Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dokta Hamisi Kigwangala amewata Wananchi kuongeza juhudi za usafi wa afya zao na mazingira kwa kuhakikisha kuwa wanazingatia kanuni za...
WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa amezitaka taasisi zote zilizo chini ya wizara hiyo kufanya kazi kwa uwazi, weledi na uaminifu ili kuongeza mapato na kutimiza adhma ya Serikali ya kufikia uchumi wa kati ifikapo 2025. Prof. Mbarawa ametoa wito huo mkoani Kilimanjaro katika majumuhisho ya ziara yake ya mikoa ya Manyara, Arusha na Kilimanjaro iliyolenga kukagua miradi ya ujenzi wa barabara, viwanja vya ndege, Posta, TTCL, TBA na TEMESA. Waziri Mbarawa amewataka mameneja na...