WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa, leo anatarajia kuzitembelea kaya zaidi ya 145 zilizoathiriwa na mafuriko katika kata ya Pawaga, wilayani Iringa kwa lengo la kuzifariji. Katika ziara hiyo Waziri Mkuu anatarajiwa kuambatana na Mbunge wa Jimbo la Isimani ilipo kata hiyo, William Lukuvi ambaye pia ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, ambao kwa pamoja watajionea hali halisi ya maisha ya kaya hizo zinazoendelea kusaidiwa ili zirudi katika maisha yake ya kawaida. Hata hivo mkuu wa wilaya ya Iringa,...
MATOKEO ya awali yaliyotangazwa hii leo nchini Uganda yanaonyesha rais wa muda mrefu wa nchi hiyo amempita mpizani wake mkuu katika uchaguzi wa rais nchini humo. Kwa mujibu wa matokeo ya awali yaliyotangazwa na tume ya uchaguzi ya Uganda, rais Yoweri Kaguta Museveni amejipatia takriban asilimia 62 ya kura, akimpita mpinzani wake mkubwa Kizza Besigye aliyejipatia asili mia 33 ya kura. Matokeo hayo yanahusu asili mia 23 ya vituo vyote vya kupiga kura nchini humo ambapo Matokeo ya...
TUME ya Vyuo Vikuu Tanzania TCU leo imevifuta vyuo vikuu vishiriki viwili vya Sayansi za Kilimo na Teknolojia, pamoja na Teknolojia ya Habari vya Chuo cha Mtakatifu Yosefu Tanzania kutokana na kuwepo kwa matatizo ya muda mrefu ya ubora wa elimu, uongozi, ukiukwaji wa sheria na taratibu za uendeshaji wa chuo kikuu ambao hauzingatii matakwa ya Sheria ya Vyuo Vikuu. Katibu Mtendaji wa TCU Profesa Yunus Mgaya amesema kuwa kifungu cha 5(1)cha Sheria ya Vyuo Vikuu , sura ya...
BARAZA la mitiani Tanzania NECTA limetangaza Matokeo ya kidato cha nne mwaka 2015 , ambapo ufaulu unaelezwa kushuka kwa asilimia 1.85 kutoka asilimia 69.75 mwaka 2014 hadi asilimia 67.91 kwa mwaka 2015. Katibu Mtendaji wa NECTA Dokta Charles Msonde ameeleza kuwa takwimu za matokeo zinaonesha kuwa bado ufaulu wa masomo yaliyomengi upo chini ya asilimia hamsini na idadi ya watahiniwa waliopata daraja la kwanza, daraja la pili na daraja la tatu ni takribani robo ya watahiniwa waliofanya mtihani. Aidha, Dokta Msonde...
KAMPUNI ya Apple imesema itapinga amri ya mahakama ya kuwasaidia wachunguzi wa shirika la kijasusi nchini Marekani FBI kuchukua habari katika simu ya muuaji wa watu 14 katika eneo la San Bernadinho nchini Marekani. Kampuni hiyo ilikuwa imeamrishwa kulisaidia shirika hilo la FBI kuifungua simu ya aina ya iphone ya Farook Syed ambayo wanasema ina habari muhimu. Katika taarifa yake mkurugenzi mkuu wa Apple Tim Cook amesema Serikali ya Marekani inaitaka Apple Kuchukua hatua kama hizo ambazo zinatishia...
WIZARA ya Elimu Sayansi Teknolojia na Ufundi imemtaka Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu ya Watu wazima kuwasimamisha kazi Wakufunzi wakazi wa tatu, kwa kukiuka utaratibu wa kuchagua wanafunzi wa kidato cha kwanza kufuatia upotoshaji uliofanywa kwa makusudi wa kuwadanganya Wanafunzi kuwa wamechaguliwa katika shule ya Serikali jambo ambalo sio kweli. Hatua hiyo imefikiwa kufuatia kuwepo kwa Wakufunzi wakazi katika baadhi ya Mikoa kutangaza kuwa Wanafunzi hao wamechaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza kama Wanafunzi wa chaguo la pili na...
SERIKALI imeombwa kufuatilia na kukagua maeneo yaliyotolewa kwa ajili ya shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo shule, hospitali na zahanati ili kuwaletea maendeleo wananchi. Rai hiyo imetolewa Jijini Dar es salaam na Diwani wa kata ya Buguruni Adam Fugame alipokuwa akizungumza na wanahabari kwa lengo la kumuomba mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Said Meck Sadik kuukabidhi uongozi wa kata kiwanja alichowahi kukikabidhi mwaka 2011 kwa ajili ya ujenzi wa shule ya sekondari ambacho kimekodishwa kwa kampuni ya Yasser General...
MWENYEKITI wa chama cha waendesha pikipiki Mkoa wa Mwanza, Makoye Kayanda, amewatahadharisha wakazi wa jiji hilo kuwa makini wawapo barabarani ili kuepukana na vitendo vya ukwapuaji mikoba na mabegi vinavyofanywa na baadhi ya wahalifu kwakutumia pikipiki maarufu Boda boda. Kayanda ametoa tahadhari hiyo jijini Mwanza baada ya kupokea malalamiko ya kukithiri kwa vitendo hivyo vinavyofanywa na baadhi ya watu wanaojifanya waendesha pikipiki jambo linalochafua taswira ya waendesha pikipiki wa...
JESHI la Polisi mkoa wa Kipolisi Temeke limewaomba wakazi wa maeneo hayo kutoa taarifa juu ya watu wanaohusika na uuzaji wa dawa za kulevya kwakuwa kimekuwa ni chanzo cha vijana kushindwa kujishughulisha. Akizungumza na EFM Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Temeke Andrew Satta amesema kuwa kutokana na oparesheni inayoendelea ya kupambana na matumizi ya dawa za kulevya, jeshi hilo limegundua wauzaji wakubwa wa dawa hizo kukimbia na kwenda kujificha katika maeneo ya nje ya mkoa huo wa...
WAZIRI wa afya maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mheshimiwa Ummy Mwalimu amewasimamisha kazi wakurugenzi wanne kutoka Bohari ya Dawa ya Taifa-MSD- kwa tuhuma za ubadhilifu wa fedha takribani shilingi Bilioni 1.5. Akizungumza na waandishi wa Habari Jijini Dar es salaam leo katika kitengo cha Afya ya mama na mtoto baada ya kupokea vifaa kutoka Bohari kuu ya Taifa ya dawa, waziri Ummy amesema amefanya maamuzi hayo kufuatia kupokea taarifa ya uchunguzi ofisini kwake juu ya ubadhilifu wa...
93.7 Efm Radio,kuadhimisha tamasha kubwa la Mchizi wangu lililofanyika siku ya wapendanao tarehe 14/02/2016, likiongozwa na mziki wa mchiriku na singeli. Tamasha hilo lilisheheni Wasani kibao wakitumbuiza huku wakiongozwa na msaga sumu na skide mtoto wa mama shante. Umati wa watu ukisheheni katika tamasha la mchizi wangu concert Raisi wa singeli Suleiman Jabir a.k.a Msaga Sumu akitumbuiza mashabaki waliofika kwenye tamasha la Mchizi Wangu. Amsha amsha kutoka kwa baadhi ya mashabiki wakionyesha nyuso za furaha wakati wakipata burudani....