WAZIRI wa ujenzi, uchukuzi na mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amesema Serikali bado ina mashaka na watendaji wa shirika la ndege la taifa ATCL na ili kuondoa dukuduku hilo inaendelea na uchunguzi wa kuwabaini watendaji wote waliohusika kulihujumu shirika hilo. Profesa Mbalawa ameyasema hayo jijini Mwanza kwenye mkutano wa sita wa sekta ya uchukuzi katika ukanda wa Afrika ya kati kwa lengo la kutathmini maendeleo katika sekta hiyo pamoja na changamoto zake uliowakutanisha mawaziri wa sekta hiyo kutoka nchi tano za...
UONGOZI wa Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Njombe umepewa muda wa siku 90 kurekebisha mapungufu ya utoaji wa huduma za afya, vinginevyo hospitali hiyo itafungwa. Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla wakati akizungumza na viongozi, Mganga Mkuu wa Mkoa, Samwel Mgema na Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Imelda Mwenda na watumishi wa hospitali hiyo. Dkt. Kigwangalla alitoa agizo kufuatia ziara yake ya ukaguzi wa hospitali, vituo vya afya...
NAIBU Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee Dk. Hamisi Kigwangalla amesema kwamba wao kama viongozi wataendelea kumsaidia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, MheshimiwaDkt. John Pombe Magufuli kutumbua majibu yanayokwamisha kutokupatikana kwa huduma bora za afya ,bila kuogopa wala kumwonea mtu kwa ajili ya maslahi ya taifa. Dokta Kigwangala ameyasema hayo wakati wa maadhimisho ya 24 ya ibada maalum ya kuwaombea wagonjwa Duniani ambayo Kitaifa yamefanyika katika jimbo Kuu la Tabora na baadae kwenye...
MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imefanikiwa kukamata bidhaa za magendo kwenye maeneo mbalimbali ya Ukanda wa Bahari ya Hindi, Ziwa Victoria na mipakani. Taarifa hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi (TRA) Bw. Richard Kayombo katika mahojiano maalum yaliyofanyika ofisini kwake Jijini Dar es Salaam kuhusu juhudi za operesheni ya kutokomeza bidhaa za magendo nchini. Amesema kuwa katika operesheni hiyo, TRA imefanikiwa kukusanya kodi ya zaidi ya shilingi milioni kumi kutoka katika bidhaa zilizokuwa...
WIZARA ya afya maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto imewataka wananchi kuhakikisha wana wapeleka watoto wote kwenye vituo husika vya Afya ili wapatiwe Chanjo na kinga ya kichocho ili kuwanusuru na ugonjwa wa kichocho. Rai hiyo imetolewa keo jijini Dar es salaamu na mratibu wa magonjwa yasiyopewa kipaumbele Pendo Mwingira ambapo amesema wizara ya afya kwa kushirikiana na shirika la afya duniani WHO limeaamua kutoa chanjo ya kumkinga mtoto dhidi ya Ugonjwa wa kichocho kwa kuwa huwaathiri zaidi watoto....
SERIKALI imejipanga kuhakikisha inaboresha zaidi mpango wa kunusuru Kaya masikini nchini ujulikanao kama TASAF kwa awamu ya tatu kwa kutengeneza miundombinu mizuri ya kutambua Kaya zinazolengwa. Akijibu swali la Mheshimiwa Magdalena Hamisi Sakaya Mbunge wa Kaliua (CUF), leo Bungeni mjini Dodoma Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mheshimiwa Angella Kairuki amesema mpango wa kunusuru Kaya masikini hutambulishwa kijijini na wataalam kutoka Halmashauri husika. Aidha Mheshimiwa Kairuki amesema kuwa...
WIZARA ya Fedha na Mipango leo imewasilisha mapendekezo ya Mpango wa maendeleo ya Taifa pamoja na mwongozo wa kuandaa mpango na bajeti ya serikali ya mwaka 2016/2017 unaolenga utekelezwaji wa vipaumbele mbalimbali vya kuleta maendeleo. Akiwasilisha mapendekezo ya mpango na mwongozo huo Bungeni Mjini Dodoma, Waziri wa Fedha na Mipango dokta Philip Mpango amesema kuwa mpango huo unalenga kuinua kwa kiasi kikubwa uchumi wa Taifa. Awali mpango huo haukuweza kujadiliwa siku chache zilizopita kutokana na serikali kuuwasilisha kimakosa hali...
ZAIDI ya wafanyakazi 800 wa kampuni ya ujenzi ya chiko ya Jamuhuri ya china inayojenga barabara kuu ya Dodoma Babati eneo la mayamaya mpaka mela wamegoma wakishinikiza uongozi wa kampuni hiyo uboreshe maslahi yao kwa kuwapatia mikataba pamoja na kuongeza mishahara huku wakitaka serikali kuwafukuza wafanyakazi wa kigeni ambao wanapora ajira zinazoweza kufanywa na wazawa huku wakilipwa mamilioni ya fedha. Wakizungumza mbele ya waziri wa ujenzi uchukuzi na mawasiliano profesa Makame mbarawa wafanyakazi hao wamesema wamechoshwa na...
Efm Radio,katika harakati zakufanikisha ahadi ya kujenga madarasa, imekabidhiwa michoro ya ramani ya madarasa ya sekondari wilaya ya Kinondoni kata ya Kimara, Makabidhiano yaliyofanyika katika ofisi za Kituo hicho cha Utangazaji kupitia masafa ya 93.7 leo asubuhi. Mkurugenzi Mkuu wa Efm Radio, Francis Siza akipokea ramani ya michoro ya madarasa kutoka kwa Afisa elimu wa wilaya ya Kinondoni Bwana Rogers J. Shemwelekwa. Afisa elimu wa wilaya ya Kinondoni Bw. Rogers J. Shemwelekwa katika picha ya pamoja na uongozi wa Efm...
IMEELEZWA kuwa zaidi ya raia laki 126,000 wa Burundi wamekimbilia nchini Tanzania tangu mwezi Aprili, 2015, kufuatia machafuko ya kisiasa nchini humo. Huku tayari wakimbizi elfu 64,000 kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC) wakiwa tayari nchini. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ametoa dola za Marekani milioni 100, sawa na shilingi za Tanzania bilioni 220 kutoka katika Mfuko Mkuu wa Kushughulikia Dharura wa Umoja wa Mataifa -CERF kwa shughuli za misaada katika maeneo tisa yenye dharura duniani...
RAIS wa Jamhuri ya Mmuungano wa Tanzania Dokta John Pombe Magufuli amesema amesikitishwa na kitendo cha kuuawa kwa rubani Mwingereza aliyekuwa akisaidiana na maafisa wa Tanzania kupambana na ujangili. Rubani wa helkopta Kapteni Roger Gower, alifariki baada ya majangili kuifyatulia risasi na kuidondosha helkopta aliyokuwa akiiendesha wakati alipoungana na askari wanyamapori waliokuwa wakikabiliana na majangili katika pori la akiba lililopo katika wilaya ya Meatu Mkoani Simiyu. Askari mmoja wa Tanzania alijeruhiwa wakati wa tukio hilo ambapo...