MAMLAKA ya Mapato Tanzania-TRA-kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi wamekamata Makontena tisa ambayo bado haijafahamika yana vitu gani ndani katika eneo la Tangibovu Mbezi Beach Jijini Dar es salaam yaliyosafirishwa kinyume na utaratibu usiku wa manane. Akizungumza na Waandishi wa habari katika eneo la tukio Mkurugenzi wa huduma na elimu kwa Mlipa kodi kutoka-TRA-Richard Kayombo amesema Mamlaka imebaini kuwa Muagizaji wa makontena hayo ni Heritage Empire Company Limited na wakala wa Forodha aliekuwa akishughulikia ni Napock Africa Company...
ZAIDI ya kaya Elfu 18 katika kata nane za Halmashauri ya wilaya ya IGUNGA mkoani Tabora zitanufaika na mpango wa ruzuku za pembejeo katika msimu huu wa mwaka 2015-2016. Afisa Maendeleo ya Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika wa wilaya ya Igunga, Hossea Samaruku ameeleza hayo wakati akizungumzia hali halisi ya upatikanaji wa pembejeo za ruzuku katika wilaya hiyo. Samaruku amesema vijiji 43 vya wilaya hiyo vitashiriki kutekeleza mpango huo na kata zitakazonufaika na ruzuku ni pamoja na Nyandekwa, Nkinga na...
WATANZANIA leo wanaungana na watu wote duniania kuadhimisha siku ya Ukimwi ikiwa ni sehemu ya kupanua ufahamu kuhusu maafa yanayoletwa na ugonjwa huo. Kama ilivyo katika maadhimisho ya Uhuru, Maadhimisho ya leo hayatafanyika kama ilivyozoeleka na badala yake fedha ambazo zingetumika katika siku hiyo zitatumika kununulia dawa za kupunguza makali ya Ukimwi- ARV. Hatua hii inafuatia Agizo lililotolewa hivi karibuni na rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta John Pombe Magufuli ambapo Katika uamuzi wake baada ya...
SHULE ya sekondari Kimani iliyopo kisarawe mkoani Pwani inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo uhaba wa maji safi na salama kutokana na kuchangia kunywa maji na wanyama katika kisima kilichpo shuleni hapo. Hayo yamebainishwa na mkuu wa shule Nazarius Hongoa wakati alipokuwa akizungumza katika mahafali ya tatu ya kidato cha nne yaliyofanyika shuleni hapo ambapo amesema kuwa wapo hatarini kukubwa na maradhi kutokana na maji kutokuwa...
BAADA ya kukaa zaidi ya miaka miwili mahabusu hatimaye mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa morogoro leo imemwachia huru katibu wa taasisi na jumuiya za kiislamu Tanzania Shekhe Ponda Issa Ponda baada ya kuonekana hana hatia kwa makosa yaliyokuwa yakimkabili. Hukumu hiyo imesomwa na hakimu wa mahakama hiyo bi Mary Moyo amesema baada ya kupitia ushahidi uliotolewa pande zote mbili yaani upande wa mashitaka na upande wa mshitakiwa mahakama imemuona mtuhumiwa hana hatia na kumwachia huru kutokana na kifungu...
SIKU chache baada ya Rais Dokta John Magufuli kuiagiza bohari ya dawa nchini-Msd-kufungua maduka ya dawa kwenye Hospitali za kanda na Taifa, tayari agizo hilo limeanza kufanyiwa kazi ambapo bohari hiyo wiki ijayo inatarajia kufungua duka kubwa la kisasa ndani ya hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Mkurugenzi wa MSD, Laurean Bwanakunu amesema tayari maandalizi ya kufungua duka hilo yamekamilika nalinatarajia kufunguliwa wiki ijayo huku akibainisha kuwa litatumia mfumo maalum wa kielektroniki ili kuhakikisha dhima ya kuwezesha upatikanaji wa dawa...
WAZIRI MKUU mheshimiwa Majaliwa Kasim Majaliwa awasimamisha kazi kamishna wa kodi Tiagi Masamaki na Habibu Mpozya kitengo cha huduma kwa wateja kutokana ubadhilifu wa fedha kwa makontena zaidi ya 300 yaliyopotea. Waziri Mkuu pia ameamuru kukamatwa kwa maafisa kadhaa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania –TRA, na wengine kufukuzwa kazi baada ya kufanya ziara ya kushutukiza Bandarini hapo leo. Maafisa hao wametakiwa pia kusalimisha pia hati zao za...
VYOMBO vya habari nchini vimetakiwa kuwa na madawati ya habari za Mahakamani, ili kuboresha uandishi wa habari hizo. Hayo yamebainishwa na Jaji kiongozi wa Mahakama kuu ya Tanzania Shaaban Lila alipokuwa akizungumza na wanahabari wakati wa kufunga semina ya mafunzo ya uandishi wa habari za mahakamani ambapo amesema pindi mtuhumiwa anapopandishwa kizimbani vifungu vya sheria ndivyo vinavyotumika kwa kuzingatia aina ya makosa ya mtuhumiwa. Amewataka wanahabari kutoa taarifa kwa kuzingatia hukumu iliyotolewa badala ya wao kuhukumu...
ASKOFU MKUU wa jimbo kuu la Tabora Mhashamu Paulo Ruzoka anaongoza ujumbe wa Tanzania kwenye ziara ya Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki duniani Baba Mtakatifu Francis nchini Uganda leo. Papa Francis anatarajia kuwasili nchini Uganda leo kwa ziara ya siku mbili akitokea Kenya kabla ya kuelekea Afrika ya Kati. Katibu wa Baraza la Maaskofu Tanzania–TEC, Padre Raymond Saba amesema Mabaraza ya Maaskofu ya Kenya na Uganda kwa pamoja yalitoa mwaliko kwa TEC kushiriki katika ziara ya Baba Mtakatifu...
WIZARA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwa kushirikiana na Wizara ya Kazi na Ajira imeandaa warsha ilinayolenga kuandaa Mkakati wa Kitaifa wa miaka 10 wa kuendeleza stadi za kazi kwa miaka mitano ya kwanza. Akizungumza na Wanahabari jijini Dar es salaam leo Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Elimu ya juu kutoka Wizara hiyo Dokta Jonathan Mbwambo amesema kuwa takwimu zinaonesha Tanzania ina watu wenye ujuzi wa chini na stadi za kazi ambazo zinahitaji kukuzwa ili nchi iweze kufikia matarajio...
KATIBU Mkuu kiongozi Balozi Ombeni Sefue amepiga marufuku utengenezaji na uchapishaji wa kadi za Christimas na mwaka mpya kwa kutumia gharama za serikali kwa mwaka huu. \Katika taarifa yake Balozi Sefue ameeleza kuwa yeyote anayetaka kutengeneza au kuchapisha kadi hizo ni vyema akafanya hivyo kwa gharama zake mwenyewe. Balozi Sefue ameagiza kuwa fedha zilizopangwa kutumika kutengenezea na kuchapisha kadi hizo zitumike kupunguza madeni ambayo wizara, Idara na Taasisi zinazodaiwa na wananchi au wazabuni...