Local News

AU: MKUTANO WA KUKOMESHA NDOA ZA UTOTONI KUANZA LEO ZAMBIA
Local News

UMOJA wa Afrika leo unaanza mkutano wa siku mbili utakaofanyika Zambia kukomesha ndoa za utotoni barani humo. Inakadiriwa kwamba mwanamke mmoja kati ya watatu barani Afrika ameolewa kwa ruhusa ya wazazi, walezi na viongozi wa kidini katika umri wa miaka 18. Idadi hiyo inatarajia kuongezeka ifikapo mwaka 2050. Nyingi ya ndoa hizo za mapema hufanyika vijijini, ambako utamaduni bado...

Like
184
0
Thursday, 26 November 2015
VIPODOZI HARAMU VYAKAMATWA BANDARI KUU MALINDI ZANZIBAR
Local News

BODI ya Chakula, Dawa na Vipodozi imekamata vipodozi haramu katika Bandari Kuu ya Malindi Zanzibar ambavyo vimepigwa marufuku kuingizwa nchini.   Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari Ofini kwake Mombasa Mkaguzi wa Bodi hiyo Nassir Buheti amesema vipodozi hivyo haramu vimepigwa marufuku kuingizwa nchini kutokana na kuwa na Viambata vyenye kemikali vinavyoweza kuleta madhara kwa Mtumiaji ikiwemo Kansa.   Amevitaja vipodozi hivyo kuwa ni pamoja na Movet Crèame kutoka Itali na Medical Fade Crème kutoka Marekani vyenye uzito wa tani...

Like
424
0
Thursday, 26 November 2015
HUKUMU YA ZUIO LA KUAGA MWILI WA MAREHEMU MAWAZO KUTOLEWA LEO
Local News

  MAHAKAMA Kuu Kanda ya Mwanza inatarajiwa kutoa hukumu dhidi ya kesi ya kupinga tamko la kamanda wa polisi mkoani humo la kuzuia shughuli ya kuuaga mwili wa marehemu Alphonce  Mawazo iliyofunguliwa na baba mdogo wa marehemu. Kesi hiyo iliyokuwa ikisikilizwa na jaji mkuu katika Mahakama hiyo  Lameck Mlacha ambapo mawakili wapande zote mbili  upande wamlalamikaji na upande wawalamikiwa wamewasilisha hoja zao katika mahakama hiyo, na itatolewa hukumu yake leo saa saba mchana. Hukumu hiyo ya leo inatarajiwa pia kuamua...

Like
266
0
Thursday, 26 November 2015
SERIKALI YAOMBWA KUBORESHA MITAALA YA ELIMU KATIKA SHULE ZA MSINGI
Local News

SERIKALI imeombwa kuboresha mitaala ya Elimu katika shule za misingi ikiwa ni pamoja na kuwepo kwa vipindi vya jinsia huku serikali ikishirikiana kikamilifu na  Mashirika yasiyokuwa ya kiserikali ambayo yamekuwa mstari wa mbele katika kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia ikiwemo Ukeketaji, Ndoa za Utotoni pamoja na Mimba za utotoni ili kuweza kutokomeza vitendo hivyo. Hayo yamebainishwa na baadhi ya walimu wa shule za misingi kupitia  Shirika la jukwaa la utu wa mtoto- CDF, walipokuwa wanatoa Elimu ya kupinga vitendo...

Like
291
0
Wednesday, 25 November 2015
IKULU YAKANUSHA KUTOA RATIBA YA MAADHIMISHO YA SIKU YA UHURU
Local News

OFISI ya Rais Ikulu, imekanusha taarifa zilizoenezwa katika mitandao ya kijamii kuwa Kurugenzi ya Mawasiliano ya rais Ikulu, imetoa ratiba ya maadhimisho ya siku ya Uhuru Tarehe 9 Disemba 2015. Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa leo na Kurugenzi ya Mawasiliano ya rais, imeeleza kuwa taarifa hizo hazina ukweli wowote na kuwataka wananchi wazipuuze. Tayari Katibu Mkuu kiongozi Ombeni Sefue ameshatoa maelekezo kwa viongozi wa mikoa na Wilaya zote juu ya namna bora ya utekelezaji wa maagizo ya Rais wa Jamhuri...

Like
382
0
Wednesday, 25 November 2015
WANANCHI WAMETAKIWA KUITUMIA SIKU YA UKIMWI KUPIMA AFYA ZAO
Local News

WITO  umetolewa kwa wananchi kote nchini kuyatumia maadhimisho ya Siku ya UKIMWI duniani ambayo huadhimishwa kila ifikapo Desemba Mosi ya kila mwaka kupima afya zao ili kudhibiti maambukizi mapya ya VVU.   Akizungumza na waandishi wa Habari leo jijini Dar es salaam Mwenyekiti Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti UKIMWI nchini Tanzania Dkt. Fatma Mrisho amesema  Siku ya Ukimwi Duniani nchini itaadhimishwa kwa  kuwahimiza wananchi kujitokeza kwa wingi  kupima afya zao na kupata elimu ya kujikinga  na maambukizi ya...

Like
249
0
Wednesday, 25 November 2015
IDADI YA WAGONJWA WA KIPINDUPINDU YAPUNGUA DAR
Local News

IDADI ya wagonjwa wa kipindupindu jijini Dar es salaam imeelezwa kupungua  kufikia wagonjwa kumi na mbili kwa mkoa mzima, huku wilaya ya Temeke pekee ikiwa na wagonjwa saba, Kinondoni wagonjwa wanne na Ilala ikiwa na mgonjwa mmoja   Mratibu wa Magonjwa  ya kuambukiza wa Jiji la Dar es salaam  Bw. Alex Mkamba ameyasema hayo ofisini kwake ambapo ameeleza pia ni  jinsi gani mkoa umefanikisha kupambana na kipindupindu kwa kuzingatia usafi katika jiji.   Mpaka sasa jumla ya watu 55 wamefariki...

Like
348
0
Wednesday, 25 November 2015
SERIKALI IMESEMA HAINA KUHATARISHA USALAMA WA WANAHABARI
Local News

SERIKALI imesema haijawahi, haina na haitokuwa na nia yeyote ile ya kuhatarisha usalama wa Wanahabari na kuwa ni jambo la maana kujenga mahusiano mazuri ya kuaminiana baina ya Serikali na Wadau wa habari kwa kuwa pale ambapo uaminifu unakosekana ndipo hisia na dhana potofu zinapojitokeza. Akizungumza na Efm leo jijini Dar es salaam  Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana Utamaduni na Michezo Elisante Olegabriel amesema kuwa sekta ya habari ni  muhimu  kwa kuwa inabeba sekta zingine zote za Taifa...

Like
269
0
Wednesday, 25 November 2015
BODI YA SUKARI IMETAKIWA KUSHUGHULIKIA MADAI YA WAKULIMA WADOGO WA MIWA KILOMBERO
Local News

KATIBU Mkuu Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika Bi. Sophia Kaduma ameiagiza Bodi ya Sukari nchini, kushughulikia haraka madai ya wakulima wadogo wa miwa katika Kiwanda cha Sukari cha Kilombero Mkoani Morogoro ili kuleta usawa. Katika Agizo hilo, Katibu Mkuu huyo ameiagiza Bodi hiyo kukutana na Uongozi wa Kiwanda  cha Sukari cha Kilombero na  ule wa wakulima wadogo wa miwa ili kupata ufumbuzi wa kudumu kuhusu soko la miwa wanayozalisha.   Aidha, Katibu Mkuu ametoa muda wa siku saba kwa...

Like
278
0
Tuesday, 24 November 2015
MAKAMU WA RAIS MH. SAMIA SULUHU HASSAN AKUTANA NA UONGOZI WA MTANDAO WA WANAWAKE NA KATIBA LEO
Local News

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan leo amekutana na uongozi wa Mtandao wa Wanawake na Katiba Tanzania na kuzungumzia dhamira ya serikali katika kuyatafutia ufumbuzi matatizo yanayowakabili wanawake na watoto wa kike nchini.   Katika mazungumzo hayo Makamu wa Rais ameueleza ujumbe huo kuwa wakati wa kampeni aliahidi pamoja na kazi za kumsaidia Rais bado kama mama atafuatilia kwa karibu utekelezaji wa ahadi ya kupatikana kwa maji safi na salama, kuboresha afya ya...

Like
754
0
Tuesday, 24 November 2015
DOLA 150000 ZATOLEWA KATIKA KIJIJI CHA MACHALI KUKABILIANA NA MABADILIKO YA TABIA YA NCHI
Local News

KIJIJI cha Manchali kilichopo wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma, kimekabidhiwa mradi wenye thamani ya dola za Marekani 150,000 kwa lengo la kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.   Akikabidhi mradi huo Mratibu wa mashirika ya Umoja wa mataifa nchini na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Alvaro Rodriguez amesema mradi huo umelenga kuisaidia jamii inayoishi katika kijiji hicho kukabiliana na changamoto mbalimbali za kimaisha zinazotokana na mabadiliko hayo.   Mradi huo pia umelenga kutatua tatizo...

Like
321
0
Tuesday, 24 November 2015